CHADEMA yateketeza CCM Kwimba

CHADEMA yateketeza CCM Kwimba

Molemo

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2010
Posts
14,620
Reaction score
13,361
Chama cha Mapinduzi CCM kiko katika hali mbaya katika Jimbo la Kwimba baada ya maelfu ya wanachama wake pamoja na viongozi kadhaa kuhamia CHADEMA.

CHADEMA imezoa wanachama 15000 katika mikutano mikubwa sita iliyopigwa katika kata kadhaa za wilaya hiyo.

Mikutano hiyo ilihutubiwa na kiongozi mkuu wa M4C Kanda ya Ziwa Alphonce Mawazo.Kiongozi huyo alisema wananchi wameamua kuhama kutoka kwenye siasa za CCM za Analogia na kuhamia siasa za CHADEMA za Digitali.

Wachunguzi wa kisiasa wilayani Kwimba wanasema CCM ina hali mbaya wilayani humo na kuna uwezekano mkubwa uchaguzi ujao CHADEMA kuzoa ubunge na madiwani wote wilayani humo.

Source:Tanzania Daima.
 
Safi sana CDM,endelea kuchanja mbuga kwa spidi ya ajabu!
 
but i doubt hizo figure hapo juu, 1500 or 15000?

Ni Elfu kumi na Tano mkuu devson.Na kukuthibitishia zaidi hilo kadi 5000 zilitolewa papo hapo kwenye mikutano na wanachama wengine 10000 wamejiandikisha kwenye madaftari wakisubiri kadi zifike kwani kadi wilayani zimeisha.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Molemo,
Mwaka 2010 nilienda Kyela baada ya uchauzi Mkuu, nilikuta watu bado wana imani sana na CCM.
Lakini habari nilizopata hivi karibuni, ni kwamba uchaguzi wa kujaza nafasi za uwakilishi ngazi za vijiji na vitongoji huko Kyela, kimeonyesha mabadiliko ya kasi ya ajabu.
Pamoja na mizengwe na rafu za CCM, CHADEMA imezoa vijiji vitano kati ya 13 vilivyogombaniwa, na vitongoji 11 kati ya 61 vilivuogombaniwa. Hii kwangu ni mafanikio ya Kimbunga katika wilaya ambayo miaka miwili iliyopita ilikuwa ni aibu kujiita mpinzani.
Hivyo, mwaka 2013, kama CHADEMA itasimama imara na kuwafukuziloa mbali wale Masalia wanaolipwa na Magamba , 2014 itakuwa turning point ya CCM kizikwa rasimi!
Tumwombw Mungu CHADEMA waisambaratishe CCM iliyomo ndani ya CHADEMA ikiongozwa na kina SHibuda, Zitto na kwa mbali ARFI
 
Masali wakisikia hali hii matumbo yanawauma>
 
Kazi nzuri,ccm iwarubuni na kuwanunua madiwani na hata wabunge wanaothamini zaidi matumbo yao,lakini wananchi zaidi wako imara kwa mabadiliko.
 
Kamanda MAWAZO umetoka CCM kwa kazi moja tu, nayo ni kuwatumikia WATANZANIA na sio tumbo lako kama ambavyo umekuwa ukisema. MUNGU akujalie tupo pamoja ila kila mmoja na upande wake ila mwisho wake tunakutana sehmu moja nayo ni KUIWEKA PEMBENI CCM katika UTAWALA wa nchi. Ahsante MUNGU.
 
Back
Top Bottom