CHADEMA yatangaza maandamano Kigoma | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CHADEMA yatangaza maandamano Kigoma

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Quinine, Mar 25, 2011.

 1. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #1
  Mar 25, 2011
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 10,866
  Likes Received: 11,982
  Trophy Points: 280
  Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimetangaza kufanya maandamano makubwa ya amani mkoani Kigoma mwezi ujao kupinga hali ngumu ya maisha kutokana na mfumuko wa bei na malipo ya fidia ya Sh. bilioni 94 kwa kampuni ya kufua umeme ya Dowans Tanzania Limited. Mpango huo ulitangazwa juzi na Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Willibrod Slaa, kwa mujibu wa Dk. Slaa, maandamano hayo ambayo yatahudhuriwa na viongozi wa kitaifa, wabunge na madiwani wa chama hicho, yatafanyika Aprili 6, mwaka huu.

  Je agizo la Shekh Mkuu kuwakataza waislamu kuandamana litatekelezwa na waumini wake au watampuuza.
   
 2. amba.nkya

  amba.nkya JF-Expert Member

  #2
  Mar 25, 2011
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 431
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 45
  Je agizo la Shekh Mkuu kuwakataza waislamu kuandamana litatekelezwa na waumini wake au watampuuza.[/QUOTE]

  Shekh Mkuu, hajafanya utafiti kuhusu maandamano ya CHADEMA, hivyo, waumini wake watampuuza tu.
   
 3. d

  dotto JF-Expert Member

  #3
  Mar 25, 2011
  Joined: Sep 29, 2010
  Messages: 1,720
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135

  na kupinga wezi kuchapisha pesa haramu na kuweka kwenye mzunguko na kutetea kuwa hii hata duniani inakubalika maana haizuiliki.
   
 4. Mpaka Kieleweke

  Mpaka Kieleweke JF-Expert Member

  #4
  Mar 25, 2011
  Joined: Feb 27, 2007
  Messages: 4,137
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Kwamba katibu mkuu alitangaza maandamano Kigoma tarehe 6 April, sio tuu kuwa ni uongo ila pia ni upotoshaji.

  Nilikuwa naye Kigoma ,hakuna tangazo kama hilo.
   
 5. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #5
  Mar 25, 2011
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 10,866
  Likes Received: 11,982
  Trophy Points: 280
  Ulikuwanaye wapi watu wengine, soma habari hii ya gazeti la Nipashe.

  25th March 2011

  [​IMG]
  Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Willibrod Slaa

  Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimetangaza kufanya maandamano makubwa ya amani mkoani hapa mwezi ujao kupinga hali ngumu ya maisha kutokana na mfumuko wa bei na malipo ya fidia ya Sh. bilioni 94 kwa kampuni ya kufua umeme ya Dowans Tanzania Limited.

  Mpango huo ulitangazwa juzi na Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Willibrod Slaa, wakati akizungumza katika semina ya madiwani wa chama hicho wa Manispaa ya Kigoma/ Ujiji.Kwa mujibu wa Dk. Slaa, maandamano hayo ambayo yatahudhuriwa na viongozi wa kitaifa, wabunge na madiwani wa chama hicho, yatafanyika Aprili 6, mwaka huu.

  Aidha, alisema maandamano hayo yana lengo la kupinga unyanyasaji wa vyombo vya dola dhidi ya raia na kushinikiza kutumika vizuri kwa rasilimali za taifa badala ya kuporwa na mafisadi.Katibu huyo alisema pia, maandamano hayo yana lengo la kuishinikiza Serikali ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kutekeleza ahadi zake ilizotoa kwa muda mrefu ili kuleta maendeleo katika Mkoa wa Kigoma.

  "Hayo ndiyo tunayotaka kuyasema kwa serikali ya CCM," alisema na kuongeza kuwa serikali imeshindwa kupeleka maendeleo katika Mkoa wa Kigoma kwa muda wa miaka mingi na kusisitiza kuwa Chadema inataka mabadiliko mkoani humo.

  Akizungumzia kuhusu ujambazi, alisema umekithiri mkoani humo kutokana na askari wa Jeshi la Polisi kulipwa mishahara midogo.
  Kuhusu wastaafu wa iliyokuwa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), alisema wanaidai Serikali Sh. bilioni 140 kwa zaidi ya miaka minane sasa, lakini pamoja na kuandamana hadi Ikulu imeshindwa kuwalipa.

  "Leo anajitokeza huyo Dowans fedha iko nje nje, Kamati Kuu ya CCM inasema watalipwa," alisema na kuongeza: "Ni jambo la kusikitisha sana kuwaona wazee wamelitumikia taifa kwa muda wa miaka mingi halafu wanaishia kunyanyasika."

  Alisema alikwenda Kigoma kwa ajili ya kuwapa semina madiwani wa Chadema ili kuwaelekeza namna ya kuiongoza Manispaa hiyo na kuwaletea wananchi maendeleo katika kata zao. Alisema madhumuni ya semina hiyo ni kuhamasisha ushirikiano kati madiwani na Meya ili kuhakikisha mabilioni ya fedha za Watanzania yanaelekezwa kwenye ujenzi wa zahanati, shule za sekondari, barabara, daraja la Mto Malagarasi na reli ili kubadilisha mkoa wa Kigoma kimaendeleo. "Na ndiyo sababu tumeamua pia kufanya maandamano haya ya amani ili kuibana Serikali kutekeleza haya ambayo imeshindwa kufanya kwa muda mrefu," alisisitiza Dk. Slaa.

  Fabruari mwaka huu, viongozi wakuu wa Chadema pamoja na wabunge walifanya ziara ya wiki moja katika mikoa ya Kanda ya Ziwa na kuongoza maandamano makubwa sambamba na mikutano ya hadhara katika makao makuu ya mikoa na wilaya kwa lengo hilo.Maandamano hayo yalifanyika katika mikoa ya Mwanza, Mara, Shinyanga na Kagera.

  Akizungumzia kuhusu fedha wanazotumia kwa ajili ya maandamano, alisema zimechangwa na wabunge na viongozi wa Chadema na si kama ilivyodaiwa na Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Sophia Simba.
  Slaa alisema Chadema wanamtaka Simba awaeleze Watanzania ni nani aliyepewa fedha hizo kati ya viongozi wa chama hicho, nchi na wapi makabidhiano hayo yalifanyika.

  Alisema waliposema watatembea nchi zima kufanya maandamano walianza kusema Chadema inafadhiliwa na mabalozi wa kigeni kutoka nchi za nje jambo ambalo si kweli."Chadema inafanya kazi za siasa kwa kuchangiwa na wabunge na viongozi wake na si vinginevyo," alisema.

  Alisema wabunge wao waliwachangia Sh. milioni 19.2 wakati wa ziara ya Kanda ya Ziwa kwa ajili ya shughuli mbalimbali yakiwamo maandamano. "Hakuna serikali ya nje hata moja iliyochangia Chadema fedha ... tumeamua katika Kamati Kuu Waziri Simba aliyetoa kauli hiyo tunataka athibitishe," alisistiza.

  Alisema katika maandamano yao, watakuwa wakimuuliza mtu mmoja mmoja kama kuna mtu anapewa fedha kwa ajili ya kushiriki maandamano ili kupata ushahidi na kama hakuna Rais Jakaya Kikwete amwajibishwe waziri huyo kwa sababu anawaongopea Watanzania.
   
 6. Mpaka Kieleweke

  Mpaka Kieleweke JF-Expert Member

  #6
  Mar 25, 2011
  Joined: Feb 27, 2007
  Messages: 4,137
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Mwandishi nafikiri alipitiwa ,ila ukweli ni kuwa aliwauliza wananchi wa kigoma kuwa ni wangapi wapo tayari kuandamana siku maandamano yakifika kigoma? wakajibu .
   
 7. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #7
  Mar 25, 2011
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 10,866
  Likes Received: 11,982
  Trophy Points: 280
  Wakajibu nini malizia...........anyway kweli sijajua unachobisha ni kuwa Chadema haijatangaza maandamano au jinsi yalivyotangazwa.
   
 8. Ehud

  Ehud JF-Expert Member

  #8
  Mar 25, 2011
  Joined: Feb 12, 2008
  Messages: 2,696
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  Kazi ipo navyojua Kigoma walivyo wanazi wa chadema. Natamani niwepo Mwanga Centre najua mambo yote yatakuwa hapo wakitokea Ujiji...
   
 9. Kagemro

  Kagemro JF-Expert Member

  #9
  Mar 25, 2011
  Joined: Jan 11, 2010
  Messages: 465
  Likes Received: 50
  Trophy Points: 45
  Dr Slaa naomba utujuze,tuliokuwapo uwanjani hatukuyasikia haya.halafu ndugu zangu wa kigoma nimepita mwandiga leo nimeona maandishi yanasema hamuungi maandamano mkono kwakuwa JK amewafanyia mengi na amewaahidi kigoma kuwa Dubai,sasa inakuwaje?
   
 10. Kagemro

  Kagemro JF-Expert Member

  #10
  Mar 25, 2011
  Joined: Jan 11, 2010
  Messages: 465
  Likes Received: 50
  Trophy Points: 45
  walijibu ndiyo tuko tayari ila zitto alishatuzuia kwakuwa JK ni rafiki yake na anamwandaa awe raisi 2015.ila mzee kwa hoja zako tutaandamana.
   
 11. Rugaijamu

  Rugaijamu JF-Expert Member

  #11
  Mar 25, 2011
  Joined: Jul 10, 2010
  Messages: 2,832
  Likes Received: 556
  Trophy Points: 280
  huu mpango wa kuwafunda madiwani ni mzuri mno,ni vema pia utekelezwe maeneo yote nchini ili madiwani watimize wajibu wajibu wao ipasavyo na kufanya halmashauri wanazoziongoza ziwe mfano wa kuigwa.PEOPLES ....
   
 12. Rugaijamu

  Rugaijamu JF-Expert Member

  #12
  Mar 25, 2011
  Joined: Jul 10, 2010
  Messages: 2,832
  Likes Received: 556
  Trophy Points: 280
  Acha kuwa kuwadi wa ufisadi...ata mseme nini hamuwezi kuzuia huu upepo!
   
 13. Bill

  Bill JF-Expert Member

  #13
  Mar 25, 2011
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 4,161
  Likes Received: 1,249
  Trophy Points: 280
  Coming slowly, hatimaye kutapambazuka.
   
 14. Mr.Professional

  Mr.Professional JF-Expert Member

  #14
  Mar 25, 2011
  Joined: Oct 4, 2010
  Messages: 1,602
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  " When men carry the same ideas in their hearts, nothing can isolate them neither prison walls nor the sod of cementries". by Fidel Alejandro Castro.
  Idea iliyopo mioyoni mwa watz ni kupata mabadiliko ya uongozi watakayoyaamini na yatakayo wapunguzia ukali wa maisha unaowaandama.
   
 15. only83

  only83 JF-Expert Member

  #15
  Mar 25, 2011
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 5,252
  Likes Received: 445
  Trophy Points: 180
  Tumualike na Mufti Idd Simba....
   
 16. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #16
  Mar 25, 2011
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Nani amekwambia Sheikh mkuu ana waumini? waumini wote ni wa Allah Subhanna hu, yeye ni kama kiongozi aliyepotea njia na kutofautiana njia na anaowaongoza na mwisho wa safari atajikuta yupo peke yake maana kishapoteza sifa ya kuongoza watu wanaojua njia ipi ni sahihi, kwa lugha nyingine tunasema kaingia chaka
   
 17. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #17
  Mar 25, 2011
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 10,866
  Likes Received: 11,982
  Trophy Points: 280
  Yeye matatizo ya Tanzania hayamhusu anadeal na kwanza na ya Libya akimaliza anaanza ya Syria then Yemen kwake hao ndio muhimu.
   
 18. G

  George Jinasa JF-Expert Member

  #18
  Mar 31, 2011
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 393
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Suala la Chadema kuandamana au kutoandamana lenyewe kama lenyewe si tatizo mradi katiba na sheria za nchi zinazingatiwa. Tunachopigia kelele sisi wadau wa haki na amani ni maandamano yenye lengo la kuleta uchochezi au kubadilisha matokea ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010. Vinginevyo, Chadema kama watanzania wana haki ya kuonesha hisia zao kwa njia ya maandamano. Ila ningewashauri viongozi wa Chadema wawe makini na kauli zao wahakikishe hawatoki nje ya mstari wa sheria na katiba. Wakumbuke kwamba katika kampeni za uchaguzi mkuu walitumia muda mwingi sana kujadili umhimu wa kutii na kuheshimu sheria na katiba katika maisha ya nchi yietu. Nitashindwa kuwashangaa kama watakuwa ndio wa kwanza kukiuka sheria na katiba.

  Halafu, nawakumbusha wanajamii forum na wananchi kwa ujumla juu ya mjadala unaoendelea wa mabadiliko ya Katiba. Tumejisahau sana katika maandamano na masuala ya babu wa Loliondo na Bibi wa Unyanyembe. Nguvu zetu nyingi tulizozitumia kudai katiba mpya tuzithamini. Nilitegemea kwenye maandamano mngekisanya maoni ya wananchi juu ya katiba mpya na kuwaelimisha juu ya namna wanavyoweza kushiriki katika mabadiliko ya katiba. Mwaka mmoja karibu unaisha. Miaka minne itaisha na katiba mpya itatungwa bila watu kushiriki inavyotakiwa.

  Suala la sheikh mkuu mimi naona tunamuonea. Kwa namna nilivyomsikia kupitia vyombo vya habari yeye anapinga maandamano yenye lengo la kuvuluga amani. Hata mimi napinga kwakuwa ni kinyume cha sheria na desituri za nchi. Kama maandamano ya Kigoma hayana lengo hilo kosa la sheikh mkuu ni lipi? Kuna utafiti gani alipaswa kufanya kwenye jambo lilowazi kiasi hicho?
   
 19. CAMARADERIE

  CAMARADERIE JF-Expert Member

  #19
  Mar 31, 2011
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 4,427
  Likes Received: 158
  Trophy Points: 160
  Please be sneered, booed and jeered at for this.........:bored:
   
 20. CAMARADERIE

  CAMARADERIE JF-Expert Member

  #20
  Mar 31, 2011
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 4,427
  Likes Received: 158
  Trophy Points: 160
  Ndugu,

  Hebu soma agenda za mkutano huo kabla ya kulaumu na kuelekeza....

  Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimetangaza kufanya maandamano makubwa ya amani mkoani hapa mwezi ujao kupinga hali ngumu ya maisha kutokana na mfumuko wa bei na malipo ya fidia ya Sh. bilioni 94 kwa kampuni ya kufua umeme ya Dowans Tanzania Limited.

   
Loading...