Kama kuna lolote la dhalura linajitokeza kabla ya miaka mitano sheria imeweka njia nyingine ya demokrasia wakilishi ambayo kupitia kwake Raisi au Waziri Mkuu anaweza kuondolewa madarakani. Wabunge ambao ni wawakilishi wa wananchi wamepewa nguvu hizo kwa utaratibu maalumu kama kiongozi wa nchi anakosa maadili ya kuongoza nchi au kumuondoa Wziri Mkuu na hatimaye Cabinet yake kama hana uwezo wa kuongoza nchi.
Umeniuliza umri, mimi nakimbilia miaka 34.
To George Jinasa kwa umri ulionao nilitegemea uwe na busara kidogo japo bado una-qualify kuwa UVCCM. Pia umenifurahisha maana unaongonea kama Membe siku ile alipoongea ITV
Mimi huwa napenda kuandika kwa mifano. Tanzania na Ivory Coast ninaweza kusema zina mfumo unaofana kama ulivyoeleza hapo juu. Kubadilisha viongozi kila baada ya miaka ya mitano through a ballot box, ambao wewe umeiita "demokrasia".
The catch 22 hapa ni je kweli demokrasia hiyo inatendeka? Tofauti ya Tanzania na Ivory Coast ni kwamba.
Tume ya uchaguzi ya Ivory Coast ilikuwa na brave enough ya kumtangaza mshindi aliyeshinda uchaguzi, lakini incumbet president Gbabo amekataa kutoka madarakani.
Tume ya uchaguzi ya Tanzania haikuwa na gut ya kumtangaza mshindi, hence ikamtangaza ALIYESHINDWA kuwa ndiye MSHINDI. Sasa hiyo demokrasia ya kubadilisha viongozi iko wapi wakati NEC ndiyo iliyotuchagulia kiongozi.
Kwa umri wako huwezi kufahamu lakini kabla ya mapinduzi ya ZNZ, kila ulipfanyika uchaguzi ASP ilikuwa ikishindwa kwenye ballot box, kwasababu ya sheria mbovu za uchaguzi zilizokuwepo.
Sasa kama hayati Abed Amani Karume angekuwa na AKILI kama zako basi hadi hii leo ZNZ ingekuwa chini ya utawala wa sultan.
Hayo yote uliyoeleza yanawezekana tu pale ambapo kuna free and fairly election and more important TUME YA UCHAGUZI IKO HURU vitu ambavyo Tanzania hatuna. Mwisho usivae miwani ya mbao au kujitia upofu kwamba Mubara na Ben Ali walikuwa hawafanyi huo unaoita uchaguzi kama Tanzania?![/QUOTE]
Nashukuru kwamba tumerudi katika mstari na pia sioni tatizo kama nitakuwa nimeonga kama Mh. Membe ili mradi tu alichokiongea nakubaliana naye.
Kwamba kuna matatizo katika Sheria ya Uchaguzi, mimi nakubaliana nawe kwa sehemu fulani. Naongezea kusema kwamba matatizo katika sheria ya uchaguzi yamekuwepo toka tulipoingia mfumo wa vyama vingi na baadhi yameshapunguzwa kutokana na marekebisho mbalimbali. Licha ya mapungufu yote, sikubaliani nawe kwamba aliyetangazwa mshindi katika Uraisi hakuwa mshindi. Hata kama tukitumia mantiki ya kawaida tu haiwezekani huyu aliyeshindwa kwa asilimia zaidi ya 60 katika uchaguzi wa wabunge na zaidi ya asilimia 70 kwenye cchaguzi wa serikali za mitaa akalalamikia matokea ya uraisi tu huku ya ubunge na serikali za mitaa yakawa sawa.
Nikirudi katika matatizo ya sheria za uchaguzi, utakubaliana nami kwamba toka kipindi cha kampeni hata baada ya matokeo ya uchaguzi kumekuwa na mijadala inayoendelea ya kutaka kubadilisha sheria zetu za uchaguzi na katiba kwa ujumla ili tuondoe dosari zilizopo. Utakumbuka kwamba kwa kipindi kirefu katika maisha ya nchi tumekuwa na mfumo wa chama kimoja. Katiba na sheria yetu iliathirika vya kutosha na mfumo huo kiasi kwamba hata tulipoingia mfumo wa vyama vingi mwaka 1992 hatukuweza kuondoa athari hizo. Yamefanyika marekebisho mbali mbali ya sheria na katiba lakini tatizo liko pale pale. Sasa baada ya shinikizo kubwa la wanasiasa na wanaharakati wa haki za binaadamu, serikali imeafiki iwepo katiba mpya itakayousuka mfumo wetu wa sheria na katiba upya ili uendane na wakati tulio nao. Nilitegemea kwamba tungetumia nafasi hiyo ili kutoa dosari katika mfumo wetu wa sheria na katiba. Kama serikali wangekuwa hawakubali uwepo wa dosari katika mfumo wetu na hawako tayari kufanya mabadiliko labda tungesema hamna alternative.
Mfano wa Zanzibar nisingependa kuuzungumzia sana kutokana na hali ya utulivu iliyopo Zanzibar sasa. Vurugu zote ambazo zimekuwepo Zanzibar kwa muda mrefu chimbuko lake ni histroria ya Zanzibar pamoja na mapinduzi. Utakumbuka kwamba muda mfupi kabla na baada ya ulioitwa uhuru wa Zanzibar mwaka 1963 (kama sikosei) vyama vya siasa Zanzibar viliundwa katika msingi wa asili. Wazanzibar wenye asili ya kiarabu kwa sehemu kubwa walikuwa na chama kimoja tu. Kwa upande mwingine Wazanzibar wenye asili isiyo hiyo walikuwa na vyama tofauti vikiegemea katika maslahi mengine ya kijamii. Haukupita muda mrefu baadhi ya Wazanzibar bila kujali asili yao waliona uhuru waliopewa na Waingereza ulikuwa wa bandia wenye lengo la kuwafanya Waingereza kuendelea kutawala kupitia kwa makundi walioyataka.