Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 117,815
- 218,478
Hii ndiyo taarifa ya haraka ambayo imesambazwa kwa vyombo vya habari asubuhi ya leo.
Kwamba John Mnyika ataongea na waandishi wa habari, leo tarehe 10/11/2022, kwenye Makao Makuu ya Chama, nje ya jiji huko Kinondoni, mtaa wa Ufipa kuanzia saa 5 asubuhi.
Bado haijafahamika kitakachozungumzwa, wote mnakaribishwa.
Katibu Mkuu CHADEMA -John Mnyika
Chombo kinachoitwa Tume ya Kurekebisha Sheria ambacho kipo chini ya Wizara ya Katiba na Sheria, natoa wito kwa Mamlaka za Serikali, Ofisi ya Rais, Ofisi ya Waziri Mkuu kusitisha mchakato huo na kwa upande wa CHADEMA tumeshatoa maelekezo kutoshiriki vikao hivyo.
Sekretariati ya chama kwa niaba ya chama tumefikia uamuzi huo kwa kuzingatia uzoefu wetu, maoni ya wananchi na uhalisia wa mambo, kwamba matatizo yetu ya kiuchaguzi msingi wake ni mapungufu yaliyopo kwenye Katiba ya sasa ya Tanzania ambayo inazalisha mapungufu mengi zaidi kwenye sheria mbalimbali. Kwahiyo huwezi kuanza mchakato kwa kurekebisha sheria za uchaguzi bila kufanya mabadiliko kuondoa mapungufu yaliyopo kwenye katiba.
Baadhi ya mambo yanayotakiwa kufanyiwa marekebisho kabla ya kuanza mchakato huo ni:
Kwenye eneo la Sheria ya Vyama vya Siasa matatizo yetu pia yanasababishwa na uendeshaji wa vyama vya siasa hasa mianya ya kutungwa kwa sheria ambazo zimetoa mamlaka makubwa yanayotumika vibaya na Msajili wa Vyama vya Siasa nayo ni ya kikatiba.
Hiki kinachotaka kufanywa na Tume ya Marekebisho ya Sheria kina nia mbaya ya kupenyeza mambo mawili;
1) Wanataka kumpa mamlaka makubwa zaidi Msajili wa Vyama vya Siasa kuingilia vyama.
2) Wana nia ovu kwa kile wanachokiita kuweka utaratibu wa vyama kudhibitiana yenye nia ovu kimsingi kuweza kutumia wingi wa baadhi ya vyama kuwatawala, kuwadhibiti vyama vya upinzani wenye msimamo wa kusimamia maswala ya demokrasia, uhuru, haki za wananchi na mambo mengine ya msingi ya mabadiliko nchini.
Kama Tume inataka kufanya mambo yake kitaalamu basi ijitokeze na kuwaeleza wananchi ni kwanini mpaka sasa imekuwa kimya haijwahi kujiunga kwenye sauti ya kuitaka serikari kuondoa zuio haramu la mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa ambalo ni kinyume na Katiba, Sheria ya Vyama vya Siasa na Sheria ya Jeshi la Polisi?
Tunakemea utaratibu huu uliyotumiwa na Tume ya Marekebisho ya Sheria kuruka ngazi za taifa za vyama na kurukia kwenda kukutana na viongozi wa chini katika mambo ambayo walipaswa kuwasiliana na vyama ngazi ya taifa.
Tunasisitiza kupatikana kwa katiba mpya ambayo itawezesha mabadiliko, Tume Huru ya Uchaguzi na kuchochea uwajibikaji.
Jambo lingine, Serikali na Bunge wasitishe hatua ambazo wanataka kuendelea nazo za kuupitisha mswada wa Bima ya Afya kwa wote pamoja na mapungufu makubwa yaliyopo kwenye mswada huo.

- Tume ya Uchaguzi - katiba ya sasa haijaunda tume huru ya uchaguzi.
- Mfumo mzima wa mzima wa watumishi wa tume, kikatiba wanapaswa kuwekewa mfumo ambao tume huru ya uchaguzi ndiyo itawezesha upatikanaji wa watumishi hao.
- Matokeo ya Urais Tanzania yamezuiliwa kwa katiba kupingwa mahakani.
- Katiba imekataza wagombea binfsi.
- Katiba haijaweka utaratibu wa chaguzi za chini kusimamiwa moja kwa moja na tume huru ya uchaguzi.
- Katiba haijaweka utaratibu ambao kura ya maoni ya katiba kuweza kusimamiwa na tume huru ya uchaguzi.
- Katiba haijaweka utaratibu kwa maamuzi ya tume kuweza kupingwa au kuhojiwa katika hatua mbalimbali.
- Katiba haijaweka utaratibu mgombea wa mbunge akiwa peke yake aweze kura ya ndiyo au hapa.