CHADEMA yatangaza kutoshiriki mapitio ya marekebisho ya sheria ya uchaguzi na sheria ya vyama vya siasa

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
117,194
217,151
Hii ndiyo taarifa ya haraka ambayo imesambazwa kwa vyombo vya habari asubuhi ya leo.

Kwamba John Mnyika ataongea na waandishi wa habari, leo tarehe 10/11/2022, kwenye Makao Makuu ya Chama, nje ya jiji huko Kinondoni, mtaa wa Ufipa kuanzia saa 5 asubuhi.

Bado haijafahamika kitakachozungumzwa, wote mnakaribishwa.



Katibu Mkuu CHADEMA -John Mnyika
Chombo kinachoitwa Tume ya Kurekebisha Sheria ambacho kipo chini ya Wizara ya Katiba na Sheria, natoa wito kwa Mamlaka za Serikali, Ofisi ya Rais, Ofisi ya Waziri Mkuu kusitisha mchakato huo na kwa upande wa CHADEMA tumeshatoa maelekezo kutoshiriki vikao hivyo.

Sekretariati ya chama kwa niaba ya chama tumefikia uamuzi huo kwa kuzingatia uzoefu wetu, maoni ya wananchi na uhalisia wa mambo, kwamba matatizo yetu ya kiuchaguzi msingi wake ni mapungufu yaliyopo kwenye Katiba ya sasa ya Tanzania ambayo inazalisha mapungufu mengi zaidi kwenye sheria mbalimbali. Kwahiyo huwezi kuanza mchakato kwa kurekebisha sheria za uchaguzi bila kufanya mabadiliko kuondoa mapungufu yaliyopo kwenye katiba.

Baadhi ya mambo yanayotakiwa kufanyiwa marekebisho kabla ya kuanza mchakato huo ni:

  • Tume ya Uchaguzi - katiba ya sasa haijaunda tume huru ya uchaguzi.
  • Mfumo mzima wa mzima wa watumishi wa tume, kikatiba wanapaswa kuwekewa mfumo ambao tume huru ya uchaguzi ndiyo itawezesha upatikanaji wa watumishi hao.
  • Matokeo ya Urais Tanzania yamezuiliwa kwa katiba kupingwa mahakani.
  • Katiba imekataza wagombea binfsi.
  • Katiba haijaweka utaratibu wa chaguzi za chini kusimamiwa moja kwa moja na tume huru ya uchaguzi.
  • Katiba haijaweka utaratibu ambao kura ya maoni ya katiba kuweza kusimamiwa na tume huru ya uchaguzi.
  • Katiba haijaweka utaratibu kwa maamuzi ya tume kuweza kupingwa au kuhojiwa katika hatua mbalimbali.
  • Katiba haijaweka utaratibu mgombea wa mbunge akiwa peke yake aweze kura ya ndiyo au hapa.
Lengo ni kusisitiza kwamba tukitaka kutibu tatizo la kukosekana kwa uchaguzi wa uhuru na haki lazima tuanzie kwenye Katiba, kinachoenda kufanyika Tume ya Kurekebisha Sheria ni matumizi mabaya ya fedha za walipa kodi.

Kwenye eneo la Sheria ya Vyama vya Siasa matatizo yetu pia yanasababishwa na uendeshaji wa vyama vya siasa hasa mianya ya kutungwa kwa sheria ambazo zimetoa mamlaka makubwa yanayotumika vibaya na Msajili wa Vyama vya Siasa nayo ni ya kikatiba.

Hiki kinachotaka kufanywa na Tume ya Marekebisho ya Sheria kina nia mbaya ya kupenyeza mambo mawili;
1) Wanataka kumpa mamlaka makubwa zaidi Msajili wa Vyama vya Siasa kuingilia vyama.
2) Wana nia ovu kwa kile wanachokiita kuweka utaratibu wa vyama kudhibitiana yenye nia ovu kimsingi kuweza kutumia wingi wa baadhi ya vyama kuwatawala, kuwadhibiti vyama vya upinzani wenye msimamo wa kusimamia maswala ya demokrasia, uhuru, haki za wananchi na mambo mengine ya msingi ya mabadiliko nchini.

Kama Tume inataka kufanya mambo yake kitaalamu basi ijitokeze na kuwaeleza wananchi ni kwanini mpaka sasa imekuwa kimya haijwahi kujiunga kwenye sauti ya kuitaka serikari kuondoa zuio haramu la mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa ambalo ni kinyume na Katiba, Sheria ya Vyama vya Siasa na Sheria ya Jeshi la Polisi?

Tunakemea utaratibu huu uliyotumiwa na Tume ya Marekebisho ya Sheria kuruka ngazi za taifa za vyama na kurukia kwenda kukutana na viongozi wa chini katika mambo ambayo walipaswa kuwasiliana na vyama ngazi ya taifa.

Tunasisitiza kupatikana kwa katiba mpya ambayo itawezesha mabadiliko, Tume Huru ya Uchaguzi na kuchochea uwajibikaji.

Jambo lingine, Serikali na Bunge wasitishe hatua ambazo wanataka kuendelea nazo za kuupitisha mswada wa Bima ya Afya kwa wote pamoja na mapungufu makubwa yaliyopo kwenye mswada huo.
 
Fanya wewe maboresho ya akili yako maana ukilala ni uchwa na ukiamka ni uchawa. Mumeo unamhudumia saa ngapi muda wote unaiwaza Chadema tu?
Naona umeshindwa kujibu hoja mkuu na kubaki kuongea maneno ya kuokoteza, Nauliza huo mkutano mnakwenda kuwalundika waandishi wa habari mle kwenye Ile ofisi iliyokosa hata madirisha ya kupitishia hewa au mtaomba nyumba ya mwanachama wenu Ndio mkae kibarazani
 
Naona umeshindwa kujibu hoja mkuu na kubaki kuongea maneno ya kuokoteza, Nauliza huo mkutano mnakwenda kuwalundika waandishi wa habari mle kwenye Ile ofisi iliyokosa hata madirisha ya kupitishia hewa au mtaomba nyumba ya mwanachama wenu Ndio mkae kibarazani
Haukuhusu wewe ngojea kuteuliwa tu haya ya kiumeni tuachie wenyewe
 
Hii ndio Taarifa ya haraka ambayo imesambazwa kwa vyombo vya Habari asubuhi ya Leo .

Kwamba Mh John Mnyika ataongea na Waandishi wa habari , leo tarehe 10/11/2022 , Kwenye Makao Makuu ya Chama , Nje ya Jiji huko Kinondoni , Ufipa Street kuanzia saa 5 Asubuhi .

Bado haijafahamika kitakachozungumzwa

Wote mnakaribishwa



Mapungufu ya katiba iliyopo yanataka kutumiwa na CCM katika uchaguzi mkuu wa ngazi zote 2025


Wakuu wa mikoa kuanza kukusanya maoni kinyemele kuhusu usimamizi wa uchaguzi mkuu

Kikosi Kazi kimetumia vibaya fedha kwa kukusanya maoni yasiyikubalika na raia wengi

Ofisi ya msajili wa vyama vya inatumika vibaya, pia ofisi hiyo haina uhuru wa kisheria kupitia katiba hivyo kuburuzwa na serikali

Vyama vingi vya kwenye makaratasi rejista ya usajili ya msajili wa vyama vya siasa kutumiwa na serikali kuvidhibiti vyama makini


TUME YA KUREKEBISHA SHERIA kuanza kuwahoji ma RC, Ma DC , Ma DED kuhusu nafasi ya wateule hao wa serikali ya CCM kyhusu namna mpya ya kusimamia uchaguzi ulio huru na wa haki.

Muswada wa bima za afya usitishwe

Bunge la Wananchi linasema kuna nia ovu kufifisha mchakato wa katiba mpya ....
 


Wakuu wa mikoa kuanza kukusanya maoni kinyemele kuhusu usimamizi wa uchaguzi mkuu

Muswada wa bima za afya usitishwe

Bunge la Wananchi linasema kuna nia ovu kufifisha mchakato wa katiba mpya ....

Endelea kutupa udates.
 
Chama cha Matamko na Domo-kula-asia!

Lini mtafika kwenya solution!
 
Back
Top Bottom