Mimi FABIAN L. SKAUKI, mgombea
ubunge wa uchaguzi mdogo jimbo la
CHALINZE ,ninamwekea Pingamizi mgombea wa chama cha demokrasia na
Maendeleo (CHADEMA) kwamba
amepoteza sifa za kuwa mgombea kwa
sababu zifuatazo.
1. Ndugu MATHAYO. M. TORONGEY
amejaza Taarifa za uongo kwenye Fomu yake kwamba kazi anayoifanya ni
BIASHARA. Sio kweli, kwa sababu
hajaweka vielelezo vya yeye kufanya hiyo
kazi. Hajulikani anafanya kazi gani.
2. Ndugu MATHAYO .M. TORONGEY
amejaza katika fomu kwamba anajua kusoma na kuandika Kiswahili na
kiingereza. Taarifa hizi ni za uongo,
mgombea huyu hajui kusoma wala
kuandika Kiswahili wala kiingereza, na
kwamba amedanganya na amepoteza
sifa za kuwa mgombea. 3. Ndugu MATHAYO .M.TORONGEY
amedanganya kwa kughushi/kufoji
sahihi za wadhamini,ambao
amewaorodhesha kwenye fomu ya
kuomba kuthibitishwa kuwa mgombea.
Ambapo katika fomu hizo wadhamini wote sahihi zao zimefojiwa na hazifanani
na zile zilizokuwepo kwenye daftari la
kudumu la wapiga kura na kwamba
sahihi zote hizi zimesainiwa na mtu
mmoja ambaye sio muhusika. Hivyo
anapoteza sifa ya kuendelea kuwa mgombea. 4. Ndugu MATHAYO.M.TORONGEY
ameshindwa kutimiza mahitaji ya
kisheria ya kuwa na wadhamini
wasiopungua 25, badala yake
amedhaminiwa na wadhamini 28 ambao
kati yao wadhamini 7 sio wapiga kura halali wa jimbo la CHALINZE, na kwamba
Taarifa zao na namba zilizojazwa
hazifanani. Hivyo anabakiwa na wadhamini halali 21
ambao kisheria hawatoshi kutimiza
matakwa ya kisheria.
Majina ya wadhamini hao ambao
hawakidhi matakwa ya kisheria na
namba zao ni JINA LA MDHAMINI NAMBA YA KADI KURA 1. HABIBU ALLY SAIDI * 16886275*
2. MOHAMMED RAMADHANI *30376567*
3. ABDULKADIR ALLY *49264905*
4. SHABANI SULEYMAN *16984045*
5. JUMA MRISHO *48759563*
6. RAJABU ALLY *16872368*
7. MANENO MIRAJI *16872059* Wananchi wenye namba na majina hayo
hapo juu waliojazwa kama wadhamini
kuanzia namba 1 hadi 7 kwenye fomu
yake hawana sifa za kupiga kura kwenye
maeneo ambayo wamejazwa
wanatokea. Hii ni kutokana na ukweli kwamba idadi
halali ya wadhamini wanaobaki
ukiwaondoa hao saba watabaki 21,
hawakizi vigezo vya kuwa wadhamini. 5. Ndugu MATHAYO.M.TORONGEY
amedanganya Uraia wake, na kwamba
yeye si Mtanzania wa kuzaliwa ndio
maana hana vielelezo halali vinavyohusu
uraia wake. Hivyo anakosa sifa ya kuwa
mgombea. Hivyo ninaomba Tume ya Uchaguzi
kutengua uteuzi wa mgombea wa
chama cha demokrasia na maendeleo
(CHADEMA) ndugu MATHAYO.M.TORONGEY
kwa kuwa anakosa sifa za yeye
kuendelea kuwa mgombea. Wako katika ujenzi wa Taifa FABIAN LEONARD SKAUKI
.. MGOMBEA UBUNGE JIMBO LA CHALINZE. THE CIVIC UNITED FRONT
+255 786 189 070/+255 754 849 450