CHADEMA yashinda uchaguzi Mbeya Vijijini

CHADEMA yashinda uchaguzi Mbeya Vijijini

WANANCHI wa Kijiji cha Ndola, Kata ya Nsalala wilaya ya Mbeya Vijijini, wamekikataa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa kutomchagua mwenyekiti wa kijiji hicho aliyesimamishwa na chama hicho.

Hali hiyo ilijidhihirisha juzi wakati wa uchaguzi wa viongozi wa kijiji hicho ambapo mgombea wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Difasi Mwakisale, alitangazwa kuwa mshindi wa nafasi hiyo.

Akitangaza matokeo ya uchaguzi huo, msimamizi msaidizi wa uchaguzi huo, Malongo Sumuni, ambaye pia ni Ofisa Mtendaji wa Kijiji cha Mbalizi, alisema kuwa Mwakisale alipata kura 513 dhidi ya mgombea mwenzake wa CCM Gilbert Mwanjela ambaye alipata kura 292.

Awali uchaguzi ulipofanyika Desemba 11 mwaka jana, Mwakisale alipata kura 405 na Mwanjela alipata kura 288, hivyo serikali ikapata kigugumizi kumtangaza na kuitisha uchaguzi upya ambao umefanyika baada ya wananchi hao kutishia kuandamana.

Wakizungumza na Tanzania Daima, wananchi wa Kijiji cha Ndola walisema kuwa uchaguzi huo ulifanyika kutokana na kugawika kwa Kata ya Utengule Usongwe baada ya serikali kuongeza kata katika wilaya hiyo.

Walisema katika uchaguzi huo wagombea wote kutoka CHADEMA walishinda katika nafasi zao ambapo ilimlazimu msimamizi msaidizi wa uchaguzi huo ambaye ni Kaimu Ofisa Mtendaji wa kata hiyo, John Mwanampasi, kukataa kumtangaza mgombea wa nafasi ya uenyekiti kutoka chama hicho.

Source:Tanzania Daima

Chama chochote pinzani cha siasa kikishafikia kushinda hadi hatua za vijiji na vitongoji dhidi ya chama tawala, ni ishara kuwa, chama husika kimekomaa kisawasawa, kinafaa kuchukua nchi na kujenga Serikali maana support ya umma ipo hadi grass-roots, ngazi ya chini. Hii ni ishara nyingine ya kufa kwa CCM na ufisadi wake wa miaka 50 na kuibuka kwa ukombozi mpya, taifa jipya kuundwa. Kama Watendaji walikuwa wanaogopa kutangaza matokeo, Umma ndio unayo mamlaka. Vivyo hivyo kwa Kigamboni na katika Ubunge Arumeru.! Wanaweza kugoma kutangaza watakaposhindwa, Umma lazima ujiandae kuingia mitaani kwa Maandamano ya Haki na ustawi!

HONGERA SANA CDM MBEYA, HONGERA CDM YOTE! HONGERA WAPIGA KURA KWA KUCHAGUA CHAGUO LILILO NA HADHI!
 
shida bado iko kyela na rungwe tu.....which is surprising kwani kila mtu angetegemea ndiko kuwe chimbuko la mabadiliko!

Watch your fingers and lips young feller Kyela na Rungwe na Mbeya kwa ujumla siyo manazi, huwa hawaangalii vyama kwa kiwango utakacho, bali huangalia mtu.
Naonya chama chochota ambacho wagombea wake wameshinda katika mkoa ule wahahakikishe kuwa viongozi waliochaguliwa wanasimamia utekelezaji wa ahadi na mipango yao, vinginevyo ni ujinga kufungua matawi na kujidhania kuwa ni ngome kwani 2015 wanaweza kushangazwa.
 
ppppppppeeeeeeeeeeeooooooooopppppppppplllllllllllleeeeeeeeeeeesssssssssssss,ppppppppppoooooooooowwwwwwwwweeeeeeeeerrrrrrrrrrrrrr
 
magwanda komalieni huko vijijini kwani ndo magamba huwa wanazoa kura nyingi, mkiwakamata huko then 2015 mko magogoni with new govt.

hakuna kusinzia ila laleni.
 
juzi nilikuwepo hapo Dar niliona mlivyo busy na CUF hadi mkafunga barabara
Raha ya CUF ni maandamano na kuona fusso zimejaza watu hawajui kumbe chama ndio kinakufa, wao ni Lipumba na Seif tu huwaambii kitu.
 
Hakika vita hii tutashinda ya kumng'oa mkoloni mweusi CCM,Mbeya ni ngome yetu CHADEMA.
 
WANANCHI wa Kijiji cha Ndola, Kata ya Nsalala wilaya ya Mbeya Vijijini, wamekikataa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa kutomchagua mwenyekiti wa kijiji hicho aliyesimamishwa na chama hicho.

Hali hiyo ilijidhihirisha juzi wakati wa uchaguzi wa viongozi wa kijiji hicho ambapo mgombea wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Difasi Mwakisale, alitangazwa kuwa mshindi wa nafasi hiyo.

Akitangaza matokeo ya uchaguzi huo, msimamizi msaidizi wa uchaguzi huo, Malongo Sumuni, ambaye pia ni Ofisa Mtendaji wa Kijiji cha Mbalizi, alisema kuwa Mwakisale alipata kura 513 dhidi ya mgombea mwenzake wa CCM Gilbert Mwanjela ambaye alipata kura 292.

Awali uchaguzi ulipofanyika Desemba 11 mwaka jana, Mwakisale alipata kura 405 na Mwanjela alipata kura 288, hivyo serikali ikapata kigugumizi kumtangaza na kuitisha uchaguzi upya ambao umefanyika baada ya wananchi hao kutishia kuandamana.

Wakizungumza na Tanzania Daima, wananchi wa Kijiji cha Ndola walisema kuwa uchaguzi huo ulifanyika kutokana na kugawika kwa Kata ya Utengule Usongwe baada ya serikali kuongeza kata katika wilaya hiyo.

Walisema katika uchaguzi huo wagombea wote kutoka CHADEMA walishinda katika nafasi zao ambapo ilimlazimu msimamizi msaidizi wa uchaguzi huo ambaye ni Kaimu Ofisa Mtendaji wa kata hiyo, John Mwanampasi, kukataa kumtangaza mgombea wa nafasi ya uenyekiti kutoka chama hicho.

Source:Tanzania Daima

Musoma tuko CHADEMA,Mwanza tuko CHADEMA,Shinyanga sote tuko CHADEMA,Kigoma tuliwakataa mafisadi wa CCM,Mbeya tumeamuka tuko CHADEMA,Wachaga wote hatutaki UOVU WA CCM,Arusha wote tuko CHADEMA Isipokuwa washamba wa Morogoro,Mtwara,Dodoma,Ruvuma,Lindi na Kagera ndo wanatetemeka kukitema chama cha matapeli wa SISIEMU.
 
huu uchaguzi wa mitaa huwa sioni kama unamaana saaaaana kwa watz. Wala huwa hauna uhusiano wa moja kwa moja na uchaguzi mkuu so ashinde wa chama chochote huwa hainishughulishi.
 
Hapo umenikumbusha ule usemi unaosema 'hakuna watu wavivu kufikiria ambao wanapata maendeleo' Watu na maeneo uliyotaja mwishoni mwa comments zako (Ukiondoa Kagera), ndio ukanda wa wavivu ambao mara wakishavuna mavuno mwaka mzima hawana kazi tena lolote linayowafanya wafikirie, bali 'ngoma' na sherehe za unyago! Tusisahau wenzetu ulaya wamefanya ugunduzi katika mengi, Kenya nao wamejitahidi fedha na utalii vipo juu, sisi wa-swahili, tumegundua 'nazi' toka 'mlingotini' tunaifuata! ....Fikra pevu, akili za mbayuwayu...mpembue wenyewe!
 
Mkuu umenifurahisha sana.
 
huu uchaguzi wa mitaa huwa sioni kama unamaana saaaaana kwa watz. Wala huwa hauna uhusiano wa moja kwa moja na uchaguzi mkuu so ashinde wa chama chochote huwa hainishughulishi.

Huelewi unachokisema.Huna tofauti na wale wanaojenga nyumba wanaanza na paa kabla ya msingi.
 
CHADEMA hoyeee,kama mtoto wa kachwamba aliyemuwezesha karamagi kushinda Bukoba vijijini alihamia CDM ujue kitaeleweka tu..maana huyu kachwamba alikua kama yule mzinzi wa magamba..
 
Hongera sana wana ndola kwa kuinua chama chetu cha cdm, toka shinani, Big up.
 
Ali ruka mkojo ,anaelekea kukanyaga mavi. Dayz are numbered. Hata huku kata ya Kirumba mwanza wana hali ngumu pamoja na kutumia pesa chafu. Kali iliyopo ni kuwa kula ccm ,lala cdm. Ipo cku kitaeleweka makamanda wangu.
 
CHADEMA kwa mtindo huu sasa watu mmegundua siri kuelekea 'ushindi wa kishindo' kwa kukipokonya CCM kilichoaminiwa kuwa ni gala ya kura bwerere vijijini kwa chama tawala.

Wala si ajali kuona Mzee Mkapa kafika mahala analia CHADEMA mchana mchana majukwaani kwani hii mbinu mpya ya kukamata mtandao wa kura vijijini wanafahamu sana maana yake.

BAVICHA na BAWACHA hakika umuhimu wa kazi yenu vijijini sasa si siri tena kwa kasi ya ajabu. Moto mkubwa zaidi wakuu!!
 
Hongera sana,,, kidogo kidogo mwisho magamba yote itakuwa kweshney
 
walio sema cdm ni chama cha watu wa kaskazini waseme sasa je huku ni kaskazini

lakini hii propaganda imesha kufa tunasubiri nyingine

hongera sana chadema wakuu kumbukeni kuwa huku ni kwa shitambala

vivaaa cdm 2015
 
Back
Top Bottom