CHADEMA yashinda uchaguzi Mbeya Vijijini | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CHADEMA yashinda uchaguzi Mbeya Vijijini

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Molemo, Mar 13, 2012.

 1. M

  Molemo JF-Expert Member

  #1
  Mar 13, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,256
  Likes Received: 380
  Trophy Points: 180
  WANANCHI wa Kijiji cha Ndola, Kata ya Nsalala wilaya ya Mbeya Vijijini, wamekikataa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa kutomchagua mwenyekiti wa kijiji hicho aliyesimamishwa na chama hicho.

  Hali hiyo ilijidhihirisha juzi wakati wa uchaguzi wa viongozi wa kijiji hicho ambapo mgombea wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Difasi Mwakisale, alitangazwa kuwa mshindi wa nafasi hiyo.

  Akitangaza matokeo ya uchaguzi huo, msimamizi msaidizi wa uchaguzi huo, Malongo Sumuni, ambaye pia ni Ofisa Mtendaji wa Kijiji cha Mbalizi, alisema kuwa Mwakisale alipata kura 513 dhidi ya mgombea mwenzake wa CCM Gilbert Mwanjela ambaye alipata kura 292.

  Awali uchaguzi ulipofanyika Desemba 11 mwaka jana, Mwakisale alipata kura 405 na Mwanjela alipata kura 288, hivyo serikali ikapata kigugumizi kumtangaza na kuitisha uchaguzi upya ambao umefanyika baada ya wananchi hao kutishia kuandamana.

  Wakizungumza na Tanzania Daima, wananchi wa Kijiji cha Ndola walisema kuwa uchaguzi huo ulifanyika kutokana na kugawika kwa Kata ya Utengule Usongwe baada ya serikali kuongeza kata katika wilaya hiyo.

  Walisema katika uchaguzi huo wagombea wote kutoka CHADEMA walishinda katika nafasi zao ambapo ilimlazimu msimamizi msaidizi wa uchaguzi huo ambaye ni Kaimu Ofisa Mtendaji wa kata hiyo, John Mwanampasi, kukataa kumtangaza mgombea wa nafasi ya uenyekiti kutoka chama hicho.

  Source:Tanzania Daima
   
 2. M

  Molemo JF-Expert Member

  #2
  Mar 13, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,256
  Likes Received: 380
  Trophy Points: 180
  Hakika Mbeya ni ngome kuu ya CDM kwa sasa
   
 3. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #3
  Mar 13, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,950
  Likes Received: 366
  Trophy Points: 180
  Hongera CHADEMA
  Hongera Wananchi wa Ndola
  Mapambano yanaendelea
   
 4. andrewk

  andrewk JF-Expert Member

  #4
  Mar 13, 2012
  Joined: Apr 13, 2010
  Messages: 3,084
  Likes Received: 40
  Trophy Points: 145
  huu moto utasambaaa mpaka Iringa
   
 5. brightrich

  brightrich Senior Member

  #5
  Mar 13, 2012
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 138
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Viva CHADEMA viva!
   
 6. L

  LAT JF-Expert Member

  #6
  Mar 13, 2012
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,524
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  mpaka malawi chadema ipo na inashinda chaguzi
   
 7. Mzee wa Rula

  Mzee wa Rula JF-Expert Member

  #7
  Mar 13, 2012
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 8,176
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  LAT bana,
   
 8. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #8
  Mar 13, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,082
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 0
  Ni ushindi mkubwa sana huu kwa magwanda na wanahitaji kila pongezi, Mwenyekiti wa kijiji ni mtu muhimu sana. Hongera CHADEMA.

  Ngoja tuone Arumeru, mtaweza?
   
 9. Encyclopaedia

  Encyclopaedia Member

  #9
  Mar 13, 2012
  Joined: Feb 27, 2012
  Messages: 60
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hongera sana wapambanaji huko Mbeya, ALUTA CONTINUA...........tujipange zaidi for 2014/2015 kwa chaguzi kubwa za Serikali za Mitaa na Urais, Ubunge na Udiwani
   
 10. AdvocateFi

  AdvocateFi JF-Expert Member

  #10
  Mar 13, 2012
  Joined: Jan 15, 2012
  Messages: 10,548
  Likes Received: 368
  Trophy Points: 180
  ha ha ha! Usinichekeshe bhana, yani na malawi tena! Kweli JF ni kisima cha burudani.
   
 11. s

  sirghanam JF-Expert Member

  #11
  Mar 13, 2012
  Joined: May 29, 2009
  Messages: 289
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Ukiona mpaka ngazi ya kijiji inataka mabadiliko. ujue hali ya chama tawala ni mbaya sana
   
 12. B

  BASIASI JF-Expert Member

  #12
  Mar 13, 2012
  Joined: Sep 20, 2010
  Messages: 2,546
  Likes Received: 114
  Trophy Points: 160
  all the best
   
 13. Gwankaja Gwakilingo

  Gwankaja Gwakilingo JF-Expert Member

  #13
  Mar 13, 2012
  Joined: Jan 26, 2012
  Messages: 1,961
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Ni hatua nyingine Muhimu kabisa kuelekea ukombozi wa Kweli na sasa tunaelekea kilichukua jimbo la arumeru East
  Hongera CDM
  Hongera wana Mbeya Vijijini
   
 14. mgt software

  mgt software JF-Expert Member

  #14
  Mar 13, 2012
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 10,217
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  safi sana mbeya c jui Dar tumekunywa maji ya bendera?
   
 15. 1800

  1800 JF-Expert Member

  #15
  Mar 13, 2012
  Joined: Dec 27, 2010
  Messages: 2,217
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Mkiambiwa wafuasi wa magamba ni malumpen mnaona mmetukanwa,wakati wenzenu wanakwenda shule nyie mlikua wapi?nani kakuambia Ndola ipo Malawi?rudi darasani mkuu!hata kufuta ujinga kidogo itatosha
   
 16. Duble Chris

  Duble Chris JF-Expert Member

  #16
  Mar 13, 2012
  Joined: May 28, 2011
  Messages: 3,490
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  walio sema CDM ni chama cha watu wa Kaskazini waseme sasa je huku ni kaskazini

  Lakini hii propaganda imesha kufa tunasubiri nyingine

  HONGERA SANA CHADEMA wakuu kumbukeni kuwa huku ni kwa Shitambala

   
 17. M

  Molemo JF-Expert Member

  #17
  Mar 13, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,256
  Likes Received: 380
  Trophy Points: 180
  Mkuu unayemwambia ni mpambanaji mwenzako.
   
 18. M

  Molemo JF-Expert Member

  #18
  Mar 13, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,256
  Likes Received: 380
  Trophy Points: 180
  Ni kweli mkuu inaleta raha sana.
   
 19. Duble Chris

  Duble Chris JF-Expert Member

  #19
  Mar 13, 2012
  Joined: May 28, 2011
  Messages: 3,490
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  juzi nilikuwepo hapo Dar niliona mlivyo busy na CUF hadi mkafunga barabara
   
 20. N

  Ntuya Senior Member

  #20
  Mar 13, 2012
  Joined: Jan 18, 2011
  Messages: 112
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  CDM, chama kubwa! big up
   
Loading...