wakuu kama kawaida cdm imekionyesha uwezo chama cha magamba baada ya mgombea wa sisiemu kupigwa chini mahakamani na kuvuliwa uenyekiti alioiba.
Wote tunakumbuka uchaguzi wa serikali za mitaa ulioisha hivi majuzi.
Huku kwetu mikocheni michezo michafu ya sisiemu iliendelea pale mgombea wa cdm aliposhinda katika vituo viwili ambavyo vyote vilikua ni madarasa ya shule ya msingi Ushindi....
Kila mtu alibaki kinywa wazi baada ya matokeo ya jumla kumtangaza mgombea wa sisiemu Bwana Sixbet kuwa ndio mshindi wa kiti hicho cha uenyekiti.
Katika hali ya kuhamaki na kila mtu akiwa Haelewi kinachoendelea polisi walipiga mabomu na kutokomea na mabox ya kura.
Mahakama imemthibitisha mgombea wa cdm kuwa ndiye mshindi halali wa kiti hicho.
Kwa makamanda tulio karibu na mikocheni....karibuni tusherehekee ushindi apa viwanja vya shule ya msingi ushindi...mida ya saa tisa alasiri...