CHADEMA yasambaratisha CCM Kilombero | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CHADEMA yasambaratisha CCM Kilombero

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Molemo, Jul 25, 2012.

 1. M

  Molemo JF-Expert Member

  #1
  Jul 25, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimepokea wanachama wapya 256 kutoka vyama vya CCM, Cuf, na TLP kutoka katika Kata nne za Wilaya ya Kilombero mkoani Morogoro. Hayo yalibainishwa na Katibu wa Chama hicho Wilaya ya Kilombero , Moses Kisenime katika taarifa yake aliyoitoa kwa vyombo vya habari.

  Kisenime alisema wanachama hao walipokelewa na Mwenyekiti wa Baraza la Vijana la Taifa (Bavicha), John Heche wakati akizungumza katika mkutano wa hadhara jimboni humo.

  Alisema Mwenyekiti huyo wa Bavicha taifa aliwapokea wanachama hao katika mikutano minne aliyofanya katika Kata ya Ifakara, Mang’ula, Msolwa na Mkamba.

  “Kutokana na mikutano yetu tunayoifanya mkoani Morogoro tumeweza kupokea wanachama 214 kutoka CCM, Cuf 28 na TLP wanachama 14,” alisema Kisenime.

  Akizungumza kwa niaba ya wenzake aliyekuwa balozi wa nyumba kumi katika Kata ya Mkamba, Mussa Katanduki alisema ameamua kuhama kutoka chama cha CCM kwa madai kuwa chama hicho kimekosa mueleko na maadili ya uongozi.

  “Sijalazimishwa na mtu kuhamia Chadema lakini kutokana na mambo yalivyo ndani ya CCM kwa ihari yangu nimeamua kuungana na chama hiki ili kuweza kuendeleza mapambano ya kutetea haki za wanyonge,” alisema Katanduki.

  Source:Mwananchi
   
 2. KV LONDON

  KV LONDON JF-Expert Member

  #2
  Jul 25, 2012
  Joined: Jul 18, 2012
  Messages: 904
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 45
  'aluta continue'
   
 3. mashami

  mashami Senior Member

  #3
  Jul 25, 2012
  Joined: May 8, 2012
  Messages: 183
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  mapambano yanaendelea
   
 4. C

  CHUAKACHARA JF-Expert Member

  #4
  Jul 25, 2012
  Joined: Jun 3, 2011
  Messages: 12,200
  Likes Received: 3,810
  Trophy Points: 280
  The most "unruly horse" is the public policy, you will never know where it will take you!!!! Hawa watu wa vijijini usiwaamini, kesho akija mwingine watageuka, bendera hufuata upepo! Naipenda CDM lakini they should not bank on these unprincipled people! Nawaheshimu sana ndugu zangu wa vijijini, lakini nachelea misimamo yao, Kweli wameingia CDM kwa dhamira ya kuona superiority ya CDM policies over the other parties au ni bendera..........
   
 5. Rejao

  Rejao JF-Expert Member

  #5
  Jul 25, 2012
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 9,239
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Kahabari kenyewe kadogo lakini mnakakuuuza....wanachama 256??????????? duh!
   
 6. M

  Molemo JF-Expert Member

  #6
  Jul 25, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Ndiyo inakuzwa kwa sababu Kilombero iko Kaskazini
   
 7. KOMBAJR

  KOMBAJR JF-Expert Member

  #7
  Jul 25, 2012
  Joined: Nov 15, 2011
  Messages: 5,848
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Karibu Sana naona siku hizi unachungulia kwa mbali au wamekutoa kwenye payral nini?:wacko: Udogo unaousema ni upi wale 60 mliwapata kigoma na hao 265 ni ipi ndogo?
  Mytake: Kama heche anaweza kurejesha wanachama 256 wakati Delegation ya Nape,Mwigulu na mawaziri wapatao 6 wamerudisha wanachama 60 ni Picha gani unapata hapo?
   
 8. TUKUTUKU

  TUKUTUKU JF-Expert Member

  #8
  Jul 25, 2012
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 11,852
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Kaka chama ni watu,chama bila watu ni sawa debe tupu! usiwe kama
  Muhammad Saeed al-Sahhaf aliyekuwa waziri wa habari wa serikali ya Sadam Hussein,siku zote alitoa taarifa za kutia moyo kwa wairaki ilihali alijua fika hali si shwari hata kidogo.
   
 9. TUKUTUKU

  TUKUTUKU JF-Expert Member

  #9
  Jul 25, 2012
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 11,852
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Acha urongo kilombero haipo kaskazini na kamwe hatakuwa kaskazini mbaka mwisho wa dunia!
   
 10. Biohazard

  Biohazard JF-Expert Member

  #10
  Jul 25, 2012
  Joined: Aug 21, 2011
  Messages: 2,002
  Likes Received: 286
  Trophy Points: 180
  Kwa kata 4 inatosha.... Mbona kwenye ziara za Nape cjawahi kuona hata wawili wakivua Gwanda na Kuvaa uzalendo?
   
 11. KakaKiiza

  KakaKiiza JF-Expert Member

  #11
  Jul 25, 2012
  Joined: Feb 16, 2010
  Messages: 10,541
  Likes Received: 2,237
  Trophy Points: 280
  Wewe hapo ulichokielewa nini???
   
 12. M

  Molemo JF-Expert Member

  #12
  Jul 25, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Mkuu nilikuwa namuumbua huyo kibaraka wa magamba
   
 13. WA-UKENYENGE

  WA-UKENYENGE JF-Expert Member

  #13
  Jul 25, 2012
  Joined: Oct 1, 2011
  Messages: 2,904
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 160
  Mkuu salama hapo Kipalapala! neno "kaskazini" limetajwa tu lakini lililenga kupitisha ujumbe fulani tofauti na ulivyoelewa.
   
 14. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #14
  Jul 25, 2012
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Lazima kakuzwe maana tangia ccm wakose mwelekeo sijawahi sikia wamepokea wanachama toka upinzani zaidi ya kuwapoteza na bado wanazidi kuwapoteza
   
 15. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #15
  Jul 25, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,196
  Likes Received: 1,977
  Trophy Points: 280
  Ule mtaji wenu wa wanachama milion 5 bado upo pale pale ukiondoa hapo 200 mbona mwaka huu mtabakia na mafisadi tuu
   
 16. Manyanza

  Manyanza JF-Expert Member

  #16
  Jul 25, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,446
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  jipe moyo mkuu lakini katika wanachama milioni moja wa CCM wakiondoka 100, watabako milioni moja?
   
 17. Kirode

  Kirode JF-Expert Member

  #17
  Jul 25, 2012
  Joined: Mar 25, 2011
  Messages: 3,573
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  umekurupuka kumjibu, tulia tafakari ndipo umjibu mtu,.. maana yake ilikuwa kina rejao wanadaigi cdm ni cha kaskazini sasa ilikuwa tu ni kama swali kwa rejao je moro pia ni kaskazini hivi ndivyo nilivyoelewa mimi......kutoka kwa molemo...tafadhali molemo njoo unisahihishe
   
 18. Remmy

  Remmy JF-Expert Member

  #18
  Jul 25, 2012
  Joined: Jun 9, 2009
  Messages: 4,718
  Likes Received: 146
  Trophy Points: 160
  Good move!
  Best of luck Kilombero!
   
 19. Advocate J

  Advocate J JF-Expert Member

  #19
  Jul 25, 2012
  Joined: May 24, 2012
  Messages: 3,880
  Likes Received: 101
  Trophy Points: 160
  huo ndio mwanzo wa harakati za ukombozi tanzania ,chama tawala kinameguka na wafuas wake kujiunga na CHADEMA,peopless
   
 20. Remmy

  Remmy JF-Expert Member

  #20
  Jul 25, 2012
  Joined: Jun 9, 2009
  Messages: 4,718
  Likes Received: 146
  Trophy Points: 160
  La muhimu hapa sasa ni kutoa elimu ya uraia kwa mantiki kuwa hawa wanachama wajue umuhimu wa kupiga kura. Kuwa na mwanachama asiyepiga kura haina maana.
  Nawajua vizuri sana vijana wa Kilombero ni washabiki wazuri sana.
   
Loading...