CHADEMA yamwekea Pingamizi Mohammed Raza uchaguzi Zanzibar

OSOKONI

JF-Expert Member
Oct 20, 2011
10,965
5,336
MGOMBEA wa kiti cha uwakilishi wa Jimbo la Uzini, mjini Zanzibar kupitia tiketi Chadema, Ali Mbaruku,amewasilisha pingamizi akipinga kuteuliwa kwa Mohammed Raza wa CCM, kuwania nafasi hiyo.

CCM imemteua mfanyabiashara huyo, upeperusha bendera yake katika uchaguzi mdogo wa kiti hicho unaotarajiwa kufanyika Februari 12 mwaka huu.

Hata hivyo jana, mgombea wa Chadema, aliwasilisha pingamizi dhidi ya Raza.Pingamizi hilo lililowasilishwa kwa Msimamizi wa Uchaguzi katika Jimbo la Uzini ambaye ameombwa kutengua uteuzi wa Raza kuwa mgombea wa nafasi hiyo kupitia chama kinachotawala.Kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari,pingamizi hilo linatokana na hati ya kiapo cha Raza cha kumruhusu kuwania nafasi hiyo.

Mgombea wa Chadema, amesema kuteuliwa kwa mwanachama huyo wa CCM kinapingana na Sheria ya uchaguzi namba 11/1984 Kifungu cha 46 (3) kwa madai kuwa Raza hakidhi vigezo.
Taarifa hiyo ilifafanua kwamba sababu za kumwekea pingamizi mgombea huyo ni kiapo cha muombaji au mgombea huyo wa CCM kushindwa kukidhi matakwa ya kisheria za viapo.
Ilisema pamoja na mambo mengine, hakuna kumbukumbu za namba zinaonyesha stakabadhi halali za malipo.

Taarifa hiyo pia ilisema mlaji kiapo hakulipa malipo halali kwa mujibu wa sheria na wala hakuomba nafuu.
“Kiapo cha muombaji kwa nafasi hii ni kinyume cha sheria za viapo Zanzibar pamoja na kukosa stempu
halali, lakini pia ni kinyume na matakwa ya sheria ya Uchaguzi ya Zanzibar,” ilisema.
MWANANCHI.
 
Loading.................due to the fact that this thread lacks enough clarification.
 
Hata nafasi yenyewe ya kushinda kwa chama cha kususa na kuandamana ni dogo sana,huo ndio ukweli.

MAJIRA NA ZAMA ZINABADILIKA HUO UKWELI WA KUJIHAKIKISHIA KUSHINDWA KWA CDM UMEUTOA WAPI WEWE MUNGU? ACHA UNAFIKI MWEHU WEWE!.
 
je hilo Jimbo lina sifa kama jina lake lilivyo? Uzini! fu.... huyu raza ni Mhindi! na si nilisikia kuwa si raia wa zenji!
 
Hivi kumbe tuna Sheria mbili za uchaguzi? Yaani ile ya Muungano (Na 1 ya mwaka 1985) na ya Zanzibar (Na 11 ya mwaka 1984)! Sijui zinafanyaje kazi kwa pamoja!
 
Una uhakika gani wa hicho unachokisema, umefanya uchunguzi ama unaendeshwa na historia?

Achana na magamba hawana vision,hebu mwulize ni lini waliota kuipoteza Mwanza?ila muda ulipowadia waliipoteza na hawajui ni kwanini na Zanzibar hili haliko mbali
 
....Hakuna hati miliki ya majimbo kwa vyama vya siasa kwa hiyo kushinda CDM inawezekana popote na wakati wowote.
 
Hivi kumbe tuna Sheria mbili za uchaguzi? Yaani ile ya Muungano (Na 1 ya mwaka 1985) na ya Zanzibar (Na 11 ya mwaka 1984)! Sijui zinafanyaje kazi kwa pamoja!

Umesahau kuwa Zenji ni nchi nyingine mbali na Tanzania?
 
hawa wazanzibar walioko jf wananifurahisha sana.
bado wako kama watoto wadogo chako chetu,changu changu.

mtakoma mwaka huu na vijiba vyenu7 vya roho,kim kardashian na priory of zion wasalimu barubaru,faiza fox,ritz na rejao.
 
Hivi huko Zanzibar kuna jimbo la UZINI? Inaelekea asili ya neno hilo inawezekana kuwa limetokana
na wananchi wa huko walikuwa na tabia hiyo (.....)!

Hakuna uwezeakano wa kulbadilisha jina hilo hasa kama wannchi wa huko wameaacha hako ka-tabia?!
 
Back
Top Bottom