CHADEMA yamvua nafasi ya uongozi Diwani Joseph Nzala Ryata, yeye atangaza kuhamia CCM

32644be2bed6d3454b5c78a55b7b95e3.jpg
Amechelewa dirisha dogo la usajili lilifungwa 31/12/2017, mwanasiasa wa mwisho kusajiliwa alikuwa Wema Sepetu kutoka Chadema ambaye baada ya sintofahamu fulani lakini alifanikiwa kusajili kabla dirisha halijafungwa!
 
Sasa nimeamini Ni kweli wananunuliwa, Aiwezekan haiwezekani wawe wanahama kwa wingi ktk zile halmashaur zinazoongozwa na wapinzani tu et ndo wawe wanahama kwa wingi.
 
CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO
CHADEMA – KANDA YA NYASA 02.01.2017

TAARIFA KWA UMMA

YAH: KUMVUA NAFASI ZA UONGOZI DIWANI JOSEPH NZALA RYATA

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Kanda ya Nyasa kinapenda kuutaarifu Umma kuwa kikao cha Sekretariet ya CHADEMA Kanda ya Nyasa kilichokaa Jumatatu tarehe 01 Januari 2018 ambacho kililenga kujadili masuala kadhaa ya utendaji ikiwemo suala la uwajibikaji kwa viongozi mbalimbali wa Chama kilifikia maamuzi ya kumvua nafasi za uongozi Joseph Nzala Ryata (Diwani wa Kata ya kwa Kilosa – Iringa Manispaa) ambazo ni Katibu wa Madiwani Kanda ya Nyasa na Katibu wa Kamati ya Wagombea Kanda ya Nyasa kutokana na uwajibikaji hafifu na kukiuka maadili ya chama.

Aidha kikao pia kilitoa maagizo kwa Viongozi wa ngazi mbalimbali za Chama kufuatilia na kutoa ripoti za utendaji wa kazi na pia kilisisitiza viongozi wake kuendelea na utekelezaji wa shughuli za Chama kwa mwaka 2018 kama ilivyo kwenye kalenda ya chama na maagizo mbalimbali yaliyomo katika waraka wa Katibu Mkuu.

Imetolewa na:

Afisa Habari

Kanda ya Nyasa

======

UPDATES; 1300HRS

======

View attachment 667280
Aliyekuwa Diwani wa kata ya Kwakilosa manispaa ya Iringa, katibu wa madiwani Kanda ya Nyasa, Joseph Ryata amejivua uanachama wa Chadema na kujiunga na CCM.
Na aende akatafute fursa Kama wenzake.
 
Back
Top Bottom