CHADEMA yamteua Mh Lema kuongoza kampeni Kalenga, huku CCM ikimteua Lusinde

Mkuu, nitawashangaa sana kama CHADEMA watampora nafasi hiyo Makene na kumpa Yeriko. Yeriko anajipendekeza tu kama alivyokuwa anafanya Ben Saanane. Leo hii anajuuuta!

mkuu. yericko anahakikisha anakuwa wa kwanza kupost matamko ya chadema huku jf ili kumuharibia makene aonekane hafai kazi imemshinda, alafu yericko anajipendekeza sana kwa mbowe apewe nafasi ya makene, yericko na mnafiki sana
 
Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA kimemteua mwanasiasa wake machachari Mbunge wa Arusha Mjini Mh G. Lema kuwa kampeni meneja katika uchaguzi wa jimbo la Kalenga,

Wakati huo chama cha Mapinduzi CCM kimemteua Mh Lusinde kuwa kampemi meneja wake,

Hii ni tafsiri ya mapambano ya siasa na matusi, ikikumbukwa matusi ya nguoni aliyowahi kuyaporomosha Mh Lusinde katika uchaguzi wa jimbo la Arumeru bado yapo katika kumbukumbu za watanzania, na wanakalenga watakumbushwa katika hilo

Kwakuongezea tu ni kuwa Pingamizi lililowekwa na Chadema dhidi mgombea wa CCM, limetupiliwa mbali katika mazingira ya kutatanisha kwakuwa halikusikilizwa na kikao chochote,

Taarifa za kuamini kutoka kwa Mkurugenzi wa Kalenga zinasema kuwa kapigiwa simu kutoka kwa "Mlanchi" wa Dar na kuambiwa atupilie mbali kabisa habari za kinachoitwa pingamizi la Chadema.

Sasa wagombea ni

CHADEMA
CCM
CHAUSTA
Juzi ulikuja na porojo kuwa Lema kakamatwa kumbe uongo leo tena umekuja na drama mpya.
 
Mkuu, CHADEMA wamechemsha sana kumtuma Lema kuongoza kampeni. Kalenga si Arusha

Ni heri kufuga panya wengi kuliko kuwa na mtu mwenye akili kama wee,changia yako inaonesha kuwas hujui sias hata kidogo una bwabwaja tuu!! Pole wewe
 
Lema tunakuaminia.Usifanye makosa kama kawaida mwishoni mwa kampeni usisahau kumwita Sauti ya Simba(Silinde ).
 
mkuu. yericko anahakikisha anakuwa wa kwanza kupost matamko ya chadema huku jf ili kumuharibia makene aonekane hafai kazi imemshinda, alafu yericko anajipendekeza sana kwa mbowe apewe nafasi ya makene, yericko na mnafiki sana
Mkuu, akipost tu huku anaenda na kule kwingine. We fuatilia tu
 
Juzi ulikuja na porojo kuwa Lema kakamatwa kumbe uongo leo tena umekuja na drama mpya.

Mkuu Ritz inawezekana ni kweli, maana nina vielelezo vyote vya kusapoti kuwa CHADEMA sio chama cha watanzania bali watu flani flani. ndio maana tarehe 16.02.2014 nilisema LEMA ndio ataongoza Kampeni huko Kalenga na Leo naona huyu mhehe anayetumia jina la baba wa taifa kaja na habari inayorandana na hiyo. Sema haaminiki huyu!
 
Last edited by a moderator:
Dah! Huo ni uonevu wa hali ya juu sana ! Utampambanisha vipi JOHN CENA ( MH LEMA ) na japhet kaseba ( lusinde ) ! KAMA NI SOKA , HIYO INAITWA ONE WAY TRAFFIC !
 
Mkuu Ritz inawezekana ni kweli, maana nina vielelezo vyote vya kusapoti kuwa CHADEMA sio chama cha watanzania bali watu flani flani. ndio maana tarehe 16.02.2014 nilisema LEMA ndio ataongoza Kampeni huko Kalenga na Leo naona huyu mhehe anayetumia jina la baba wa taifa kaja na habari inayorandana na hiyo. Sema haaminiki huyu!

natamani MAGESA MULONGO AHAMISHIWE IRINGA .
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom