Candid Scope
JF-Expert Member
- Nov 8, 2010
- 11,890
- 6,898
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu,
Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), George Mkuchika
Chadema wamfikisha Mkuchika kwa AG
Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimemwandikia barua Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) kumtaka atoe ufafanuzi wa kisheria kuhusu uamuzi wa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), George Mkuchika, wa kuruhusu madiwani watano, kuendelea na nyadhifa zao, kuhudhuria vikao vya halmashauri na kulipwa posho, licha ya kuvuliwa uanachama na chama hicho.
Mkuchika alitoa maamuzi hayo kupitia barua yenye kumbukumbu namba HA.23/235/01/06 aliyomwandikia Mkurugenzi wa Jiji la Arusha, Estomih Changah ya Agosti 23, mwaka huu, akiwaruhusu kuendelea na vikao vya halmashauri hiyo hadi hapo mahakama itakapotoa uamuzi juu ya kufukuzwa kwao uanachama.
Akizungumza na NIPASHE jana, Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, alisema wanataka ufafanuzi huo kutoka kwa AG kwa vile wanaamini maamuzi yaliyofikiwa na Mkuchika ni kinyume cha sheria. Tumemwandikia Mwanasheria Mkuu wa Serikali atoe ufafanuzi wa kina wa kinachofanyika ndani ya serikali yake, kama hiyo ni misingi ya sheria, au atoe ushauri wa kisheria kurekebisha udhaifu uliojitokeza, alisema Mbowe. Alisema madiwani waliofukuzwa katika chama, kamwe hawawezi kuhudhuria vikao vya halmashauri, kwani hawana sifa hiyo.
Mbowe alisema wananchi wa Jiji la Arusha hawatakuwa tayari kuwaruhusu madiwani hao kuhudhuria vikao hivyo, badala yake watawazuia. Alisema watu waliowachochea na kuwadanganya madiwani hao kukisusia chama chao kwa sababu ya kufukuzwa, walishawaahidi kuwa wangewalinda. Hata hivyo, alisema hawawezi kuwalinda bila kufuata sheria.
IPPMedia