Chadema yaliza watumishi halmashauri ya jiji mwanza!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Chadema yaliza watumishi halmashauri ya jiji mwanza!!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by samirnasri, Mar 13, 2011.

 1. samirnasri

  samirnasri JF-Expert Member

  #1
  Mar 13, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 1,377
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Kuna taarifa kuwa watumishi walioajiri katika ofisi za halmashauri ya jiji la mwanza wamekuwa katika wakati mgumu tangu chadema waanze kuiongoza halmashauri hiyo ambayo ni miongoni mwa halmashauri zinazokusanya mapato mengi zaidi hapa nchini. Watumishi hao wamekuwa katika wakati mgumu baada ya baraza la madiwani linaloongozwa na chadema kudaiwa kufuta malupulupu mbalimbali waliyokuwa wakijigawia watumishi hao wakiongozwa na mkurugenzi wa jiji. Taarifa zinazohitaji uchunguzi zaidi zinasema kuwa hapo nyuma watumishi wa halmashauri walikuwa wakipigana vikumbo hadi siku za jumamosi na jumapili kwenda ofisini kufanya kazi huku wakiambulia malupulupu yanayokadiriwa kufikia sh. Laki mbili na nusu za kitanzania kila mwisho wa wiki pamoja na malipo ya overtime. Baada ya chadema kuongoza halmashauri inasemekana malipo ya overtime yamefutwa pamoja na yale malupulupu ya kila mwisho wa wiki. Tangu uamuzi huo uchukuliwe watumishi wengi wamekua wakitoka ofisini sa tisa na wamekuwa wakionekana mara chache sana siku za jumamosi na jumapili. Taarifa zinazidi kusema kuwa kuna watumishi sasa wanatamani kuuza magari yao kwa kuwa pesa za kuyagharamikia zimekuwa ngumu. Chanzo: kutoka halmashauri ya jiji-mwanza.
   
 2. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #2
  Mar 13, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,174
  Likes Received: 892
  Trophy Points: 280
  hii safi.

  wasiwasi wangu ni source ya taarifa yenyewe. inaonekana uliambiwa tu na jamaa yako mkiwa kwenye baraza la supu ya sato
   
 3. samirnasri

  samirnasri JF-Expert Member

  #3
  Mar 13, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 1,377
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Kuna muajiriwa mmoja wa halmashauri ya jiji alikiri kwamba hali ni ngumu sana kwa sasa.
   
 4. Filipo

  Filipo JF-Expert Member

  #4
  Mar 13, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 9,330
  Likes Received: 210
  Trophy Points: 160
  Ufisadi wa kujipa marupurupu yasiyokuwa na maelezo ndio unasababisha mkurugenzi akishirikiana na CCM kulazimisha meya wao hapa Arusha maana wanajua wa CDM ajawaumbua na kuwakomesha kama huko Mwz. Big up Mwz. Mfanye na uchunguzi kama kuna ufisadi wapelekwe mahakamani. Sisi huku Arusha mpaka sasa hatuna serikali ya h/wilaya maana "hatuna" meya! Na hakuna kulala mpaka kieleweke!
   
 5. nsimba

  nsimba JF-Expert Member

  #5
  Mar 13, 2011
  Joined: Oct 7, 2010
  Messages: 785
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  kama ni kwa ajili ya kudhibiti rushwa, matumizi mabovu, na kuimarisha huduma ya waliowengi ni safi; bali si kwa minajri ya kukandamiza watumishi.
   
 6. Kiherehere

  Kiherehere JF-Expert Member

  #6
  Mar 13, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 1,804
  Likes Received: 245
  Trophy Points: 160
  nilitegemea hayo na bado mengine...
   
 7. commonmwananchi

  commonmwananchi JF-Expert Member

  #7
  Mar 13, 2011
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 2,144
  Likes Received: 475
  Trophy Points: 180
  Na kwa hili tunastahili kuwapongeza cdm kwa kudhibiti
  matumizi yasiyo na tija.kama kazi inaweza fanyika ktk muda wa kazi ulio kisheria iweje ulazimishe O/T.
  huo ni moja ya ufisadi pevu pia.
   
 8. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #8
  Mar 13, 2011
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,468
  Likes Received: 4,128
  Trophy Points: 280
  Safi sana....
   
 9. Mlangaja

  Mlangaja JF-Expert Member

  #9
  Mar 13, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 541
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  Ahsante Bwana Mungu. Nawaombea Mungu viongozi wa CDM waendelee kuongaza nchi katika misingi ya Mungu aliye hai.
   
 10. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #10
  Mar 13, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Mwambie na bado, wasubiri mabadiliko zaidi
   
 11. M

  MsandoAlberto JF-Expert Member

  #11
  Mar 13, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 1,019
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Watumishi wengi wa Halmashauri wamekuwa hawafanyi kazi zao au hawatimizi wajibu kwa mategemeo kwamba watafanya overtime na kulipwa. Suala hili limekuwa ni mzigo kwa Halmashauri nyingi.

  Ni mkakati wa CDM kuhakikisha tabia hiyo inakoma. Watumishi wafanye kazi ndani ya muda uliowekwa na zikamilike.
  Overtime iwe ni kwa kazi za dharura tu. Pia wawe wazalendo na wenye moyo wa kujitolea sio kila kitu wanataka walipwe.
   
 12. S

  Songasonga Senior Member

  #12
  Mar 13, 2011
  Joined: Mar 13, 2011
  Messages: 152
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Politics vs civil service kazi ipo ngoja tuone mwanza
   
 13. Ndumbayeye

  Ndumbayeye JF-Expert Member

  #13
  Mar 13, 2011
  Joined: Jan 31, 2009
  Messages: 4,784
  Likes Received: 1,038
  Trophy Points: 280
  kwani walikuwa hawafuati taratibu za kiutumishi, viwango vya serikali si vinajulikana!
   
 14. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #14
  Mar 13, 2011
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 10,844
  Likes Received: 11,962
  Trophy Points: 280
  That is what we have been waiting for so long, i wish Musoma Arusha Kigoma Ukerewe Hai etc etc......could practice the same.
   
 15. I

  Ipole JF-Expert Member

  #15
  Mar 13, 2011
  Joined: Apr 15, 2008
  Messages: 296
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Mnasema msiyo yajua madiwani hawana uwezo wa kuzuia marupurupu ya watendaji. Kwa kuwa hakuna hata documenty moja inayo sainiwa iwe ni diwani au meyer msizungumze habari za mitaani
   
 16. K

  Kakalende JF-Expert Member

  #16
  Mar 13, 2011
  Joined: Dec 1, 2006
  Messages: 3,259
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 135
  Na bado!
   
 17. Halfcaste

  Halfcaste JF-Expert Member

  #17
  Mar 13, 2011
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 973
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 45
  Nijuavyo mimi serikalini hakuna hela maana Wageni(according to Membe) hawajatoa Mshiko wa kutosha.
   
 18. MTAZAMO

  MTAZAMO JF-Expert Member

  #18
  Mar 13, 2011
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 12,482
  Likes Received: 5,557
  Trophy Points: 280
  inaweza kuwa kweli lakini maeneo mengi serikalini hali ni mbaya sana na hasa zile zinazotegemea ruzuku kwa % kubwa.mshahara kwa graduate ni
  Kama laki 3 bila marupurupu hapatakalika na kuna tishio kubwa watu kurudi private sector na hapo ndio itapokuwa balaa.bila marupurupu serikalini hapakaliki cha msingi ni kuyasimamia yawe reasonable.swala la overtime kule ni sh 10,000 tu kwa siku hivyo hiyo si motivation watu waende w'end kazini.tuwe makini isijekuwa watu moral imeshuka sabab ya hali ngumu!Cdm wawe makini ili watumishi wajitume cha msingi ni kuweka utaratibu wa uwajibikaji,najua wapo wazalendo wenzetu kule kama mshahara laki 3 na alivuta ka mkopo ka 4mil anakatwa anabaki na laki na nusu! ni hatari waungwana.ni tahadhari tu wakuu!
   
 19. K

  KICHAPO Member

  #19
  Mar 13, 2011
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 51
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mwevitinyekiti wa Halmashauri akiwa fisadi anao uwezo mkubwa wa kumshawishi Mkurugenzi na wakaiba mamilioni ya shilingi,ndio maana huku mikoani tunawaona wenyeviti wakijenga mahekalu na kununua magari wakati hawana mishahara ya kueleweka.Hilo la Mwanza linawezekana kwani Meya anao uwezo wa kuidhinisha pesa zitumike vipi.
  TUKUMBUKE SALA HII KILA SIKU NDUGU ZANGU

  TUOMBE:
  Ee KIKWETE uliye tufilisi, jina lako USANII MTUPU,utakalo lifanyike BAGAMOYO tu, utupe leo mabilioni yetu ya EPA, uwapeleke MAFISADI wote mahakamani, uwalipe wastaafu pesa zao,CCM ianguke kwenye uchaguzi ujao kama wewe unavyoanguka majukwaani,usiwalipe DOWANS kama vile unavyofikiria AMIN Mungu ibariki Tanzania na Watanzania
   
 20. Pakawa

  Pakawa JF-Expert Member

  #20
  Mar 13, 2011
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,713
  Likes Received: 3,122
  Trophy Points: 280
  What do you mean ulitegemea hayo. Wanachokifanya ni sahihi kabisa ni njia mojawapo ya kudhibiti ujinga uliokithiri sehemu nyingi makazini. Kujilipa pesa ovyo ovyo wakati hamleti maendeleo yoyote kwa wananchi mnategemea nini.
   
Loading...