Chadema yalipua mawaziri wawili | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Chadema yalipua mawaziri wawili

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BAK, Mar 27, 2009.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Mar 27, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,921
  Likes Received: 83,429
  Trophy Points: 280
  Chadema yalipua mawaziri wawili

  2009-03-27 11:13:27
  Na Richard Makore

  Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimewalipua mawaziri wawili na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Nchini (Tanesco) na kuwataka wajiuzulu kutokana na kushindwa kusimamia kazi zao ipasavyo.

  Kauli hiyo ilitolewa jana jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Willibrod Slaa alipozungumza na waandishi wa habari.

  Alimtaka Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Lawrence Masha ajiuzulu kutokana na kushindwa kuzuia mapigano ya koo yanayoendelea wilayani Tarime, mkoa wa Mara na Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja, kwa kushindwa kuzuia nchi kuingia gizani kutokana na mgawo wa umeme ulioanza juzi jijini Dar es Salaam.

  Aidha, Dk. Slaa alisema mapigano hayo yanafadhiliwa na wanasiasa wilayani Tarime ili ionekane kwamba Chadema ambacho kinaongoza Halmashauri ya Wilaya imeshindwa kufanya kazi.

  Aliongeza kuwa Waziri Masha anatakiwa kujiuzulu katika nafasi hiyo kwa kuwa wananchi wengi wanapoteza maisha huku akiangalia bila kuchukua hatua yoyote kuzuia.

  ``Huyu Masha anatakiwa kujiuzulu kwani ameshindwa kuzuia mapigano, ila nchi hii viongozi wake hawana utamaduni wa kuachia ngazi, anapokosea na hili huenda lisifanyike,`` alisema.


  Kuhusu suala la mitambo ya kufua umeme ya kampuni ya Dowans Tanzania Ltd, Dk. Slaa ameitaka serikali kutaifisha mitambo hiyo na sio kuanza kujadili namna ya kuinunua.

  Dk. Slaa alisema Kamati Teule ya Bunge iliyokuwa chini ya uenyekiti wa Mbunge wa Kyela, Dk. Harrison Mwakyembe, ambayo ilichunguza suala la Richmond ilisema mitambo hiyo iliingizwa nchini kwa njia za rushwa hivyo haiwezekani serikali ifikirie kuinunua mitambo isiyopatikana kwa njia za halali.

  Alisema suala la kununua ama kutonunua mitambo hiyo halitakiwi kuzungumzwa kwa kuwa haikuingizwa nchini kwa njia halali, hivyo kujadili suala hilo ni kupoteza muda.

  Aidha, alimtaka Mkurugenzi Mtendaji wa Tanesco, Dk. Idris Rashid, pamoja na Waziri Ngeleja kujiuzulu kutokana na nchi kukumbwa na giza.

  Kuanzia jana Tanesco ilitangaza kuanza kwa mgawo wa umeme sehemu mbalimbali hapa nchini.

  Kuhusu mgawo wa umeme, Dk. Slaa alisema Kamati ya Dk. Mwakyembe iliyochunguza Richmond mwaka 2007 ilitoa mapendekezo kwa shirika hilo kuchukua tahadhari ili nchi isiingie katika mgawo wa umeme.

  Alidai kuwa Dk. Rashid hawezi kuisaidia Tanesco kwa kuwa ni mmoja kati ya watu waliochota fedha akiwa Gavana wa Benki Kuu Tanzania (BoT) kupitia ununuzi wa rada.

  Alisema ununuzi wa rada haukuwa na maslahi kwa taifa na kwamba Dk. Rashid ndiye aliyekazania suala hilo, lakini lengo lake lilikuwa kutaka apate fedha.

  Alimtaka Waziri Ngeleja kueleza matumizi ya mitambo ya Songas iliyopo Ubungo kwa kushindwa kutatua tatizo la umeme mpaka nchi kuingia katika giza.

  Katika hatua nyingine, Dk. Slaa aliungana na Dk. Mwakyembe na kuwaita mafisadi watu wanaompinga kuhusu ununuzi wa Dowans.


  Alisema msimamo wa Dk. Mwakyembe kwamba mitambo ya Dowans haifai kununuliwa ni sahihi na yeye anaunga mkono suala hilo.

  Kuhusu Naibu Katibu Mkuu wake, Zitto Kabwe, kutofautiana naye katika suala la ununuzi wa mitambo hiyo, Dk. Slaa alisema hawezi kutoa maoni.

  Alisema Zitto anaongoza Kamati ya Bunge ya Mashirika ya Umma na kwamba ripoti yake ataijua itakapofikishwa bungeni na hapo ataweza kujua kwa nini msaidizi wake anakazania serikali inunue mitambo hiyo.

  Aliongeza kuwa msimamo wa Zitto kutaka serikali inunue mitambo hiyo na yeye kupinga hakujazua migogoro kama ilivyoripotiwa na vyombo vya habari.

  Lakini kwa upande mwingine, Dk. Slaa alisema anakerwa na tabia ya Mbunge wa Igunga CCM, Rostam Aziz, kwa kumchezea rafu, Dk. Mwakyembe katika mradi wa umeme wa upepo anaotarajia kuanzisha mkoani Singida.

  Alisema kampuni ya kizalendo ya Dk. Mwakyembe ilikuwa inatarajia kuzalisha umeme katika kijiji cha Kisesida mkoani Singida, lakini Rostam akaingilia kati na kuvuruga mpango huo ili kazi hiyo aifanye yeye.

  Katika hatua nyingine, chama hicho kimewavua uanachama wanachama wake 15 kwa kosa la kueneza propaganda zilizolenga kuibua migogoro na kukigawa chama hicho.

  Uamuzi wa kuwavua uanachama ulitangazwa jana jijini Dar es Salaam na Dk. Slaa na kueleza kuwa uamuzi huo ulifikiwa baada ya kuunda kamati ya kuchunguza tuhuma hizo dhidi ya Mbowe na kubainika kuwa zote zilikuwa za uongo.

  Wanachama hao walimtuhumu Mbowe kwa kutafuna fedha za chama, kushiriki kumuua marehemu Chacha Wangwe kutumia chama kwa itikadi za ukabila, kudhoofisha vita dhidi ya ufisadi na kushindwa kufanya ziara mikoani.

  Aliongeza kuwa kamati ya kuchunguza madai hayo ya wanachama iliongozwa na Mwenyekiti mstaafu wa Chadema, Bob Makani.

  Dk. Slaa alisema wanachama wote walipoitwa na kamati hiyo ili kutoa ushahidi walikataa na kwamba matokeo ya uchunguzi yanaonyesha kwamba wanachama hao walikuwa wanatumiwa na watu kukivuruga chama.

  Katika uchunguzi huo kamati ilibaini watu saba kuwa wanatoka chama fulani cha siasa akiwemo mmoja ambaye ni mfanyakazi wa Mbunge mmoja jijini Dar es Salaam.

  Alimtaja mfanyakazi huyo kuwa jina tunalisitiri, jambo ambalo linaonyesha kuwa migogoro iliyokuwa ikisemwa ilipandikizwa na watu wasiokitakia mema chama hicho.

  Alisema wanachama hao kwa kutumiwa na wapinzani wao kisiasa walizusha tuhuma ambazo hazikuwa na ukweli wowote dhidi ya mwenyekiti wake, Freeman Mbowe.

  Dk. Slaa alisema mmoja wa wanachama waliofukuzwa ni Kaimu Mwenyekiti wa chama hicho wa Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam, Martin Mng`ong`o.

  Alisema wanachama hao walikuwa wanatumiwa na watu wasiokitakia mema chama hicho na kwamba hivi sasa wamewasafisha ili kukiwezesha chama kusonga mbele.

  Aliongeza kuwa walipata taarifa za kuwepo mipango ya kukivuruga chama hicho na hapo ndipo walipoanza kuweka mitego ya kuwafuatilia wanachama hao.

  ``Sisi tunapata taarifa nyingi kutoka sehemu mbalimbali hivyo ilikuwa rahisi kuwakamata mamluki hao wa kisiasa,`` alisema.

  Dk. Slaa alisema mwanachama yeyote anayetumiwa na watu kukivuruga chama chake watamshughulikia kwa kuwa wana mtandao mkubwa wa kuwabaini.

  SOURCE: Nipashe
   
 2. Scientist

  Scientist JF-Expert Member

  #2
  Mar 27, 2009
  Joined: Feb 7, 2009
  Messages: 392
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hivi mbona huyu slaa hajawa wazi kuhusu suala la Zitto a.k.a DOWANS?
   
 3. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #3
  Mar 27, 2009
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,639
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  Siku akiwa wazi kuhusu hilo, naye atatakiwa kujiuzulu..!
   
 4. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #4
  Mar 27, 2009
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Mie sioni chochote cha maana alichoshauri bali kujitafutia umaarufu tu. Wakijiuzulu ndio nini?

  Wanunue mitambo ya umeme imekaa bure pale Ubungo, watu wanahangaika kwa kukosa umeme, hospitali zisizo kuwa na umeme time ya mgao inabidi zisitishe shughuli zao zinazohitaji umeme, viwanda inabidi shift kamili ya masaa 8 visizalishe. Ni hasra ngapi hiyo? hasara zaidi ya kununuwa mitambo iliyo tayari, uwani mwa Tanesco, ni kubofya tu kifungo na watu wanapata umeme kama kawaida.

  Watu wamekazana Dowans, Dowans! Dowans wanakosa gani? mbona hawajashitakiwa kama wanakosa? hao wabunge wanao tutungia sheria si wengi wao wana sheria? mbona wasione kama Dowans kafanya kosa na wamshitaki na tunaona kuwa Dowans ndio kashitaki! looh, hatuna hata kufikiri! umaarufu wa kupitia siasa unatufanya tupate hasara na mitambo ipo uwani kwetu. ''Afana aleki, kufa hakuna breki''
   
 5. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #5
  Mar 27, 2009
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 0
  - Very interesting,

  FMES!
   
 6. Kasheshe

  Kasheshe JF-Expert Member

  #6
  Mar 27, 2009
  Joined: Jun 29, 2007
  Messages: 4,690
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Ni tanzania mkuu unashangaa nini?

  Kasheshe
   
 7. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #7
  Mar 27, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Slaa anamkingia kifua fisadi Mwakiembe ,hivi ule mradi wa Mwakiembe ni wa kiasi gani ,fedha yote hiyo aliipata wapi ,hawa akina Slaa ni watu hatari sana ,hawana msimamo kabisa ,wanawayumbisha wananchi, yaani Slaa anasema wananchi na walale gizani ,ndio maana yake ,eti mitambo itaifishwe kwa sababu iliingia nchini kwa njia ya rushwa, sasa nani alitoa rushwa na nani alipokea rushwa ? Hapa kuna tatizo la rushwa ,sidhani kama Dowans watakuwemo na badala yake ni Richmond,hivyo kuihusisha mitambo na rushwa itakuwa ni kulazimisha tu lakini hakuna ukweli wowote.
  Zitto anaonekana ni mzalendo zaidi kuliko Slaa ,msimamo wa Zitto ni kupita njia zozote zile lakini mwananchi asiekwe gizani ,Zitto amekwisha ona kuwa kwa kufukuzana na mafisadi ni kupoteza wakati kwani ndani ya CCM hakuna asiekuwa fisadi hivyo ameona kuwa kumjali mwananchi ni kitu nambari one.
   
 8. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #8
  Mar 27, 2009
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,320
  Likes Received: 5,611
  Trophy Points: 280
  Chadema mnatuchanganya.....sasa tutakiamini chama gani kama mnagombana kweli mtaweza kuongoza nchikama nyie tu mko 20 hivi mnagombania vijiruzuku ivyo??shame on u chadema....make kimya muuwaache isadis wapete tu kama bado hamjajipanga .....mnatia aibu.
   
 9. Makaayamawe

  Makaayamawe JF-Expert Member

  #9
  Mar 27, 2009
  Joined: Feb 21, 2009
  Messages: 341
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0

  Huu ndio upuuzi wetu wapinzani kutegemea kuwa CCM wanaweza kuwachukulia hatua wapendwa wao kwenye mambo wanayoweza kukwepa kiurahisi.
  1. Hivi vijana wa UDSM wanafanikiwa mambo yao kwa kuuandikia uongozi vibarua vya mapenzi???
  2. Huu ni wakati wa kuingia mitaani kulazimishia haki yetu. Watanzania wameshasikia maovu ya CCM na wanasubiri tu uongozi imara ili kuwang'oa.
  Kama akina Dr. Slaa, Mbowe, Zitto n.k. hamyawezi haya ya NGANGARI, basi tufahamisheni tujue moja, maana CCM hawatang'atuka hata siku moja kwa kelele za mlango tu.
   
 10. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #10
  Mar 27, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Na ndio hapo nilipowashukia na kuwambia kwa kuwafichua mafisadi watawamalizawafuasi wa Sultani CCM wote na hakuna litakalo wasaidia ,sasa inaonekana wazi rangi yao ya kutumiliwa na makundi ya Sultani CCM ,Slaa na Mbowe kundi la Mwakiyembe na Zitto akiwa upande mwengine japo anaonekana kuwa zaidi upande unaoonyesha kuwasaidia wananchi ,ule upande ambao mwananchi wa kawaida hatolala gizani.
   
 11. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #11
  Mar 27, 2009
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  ..Ninapata shaka na uwezo wako wa kufikiria mkuu wangu.
   
 12. Madela Wa- Madilu

  Madela Wa- Madilu JF-Expert Member

  #12
  Mar 27, 2009
  Joined: Mar 24, 2007
  Messages: 3,074
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 135
  Kumradhi.

  Hii nisawa na lile tusi la rejareja ambalo wanasiasa wengi wa Tanzania wamekua wakitutukana wananchi kwamba "Wananchi tumekalia uchumi".

  Duniani kuna wanaume kibao wanaishi maisha ya Kichoko. katika maana kwamba huuza miili yao kwa wanaume wengine na kujiingizia kipato.

  Ni kweli pia kwamba wako wanaume wengi ambao huishi katika maisha ya ufukara huku wakiwa na 90% ya sifa zote ambazo wanaume choko wanazo isipokuwa nia ya kuuza miili yao kwa wanaume wenzao.
  Kwa vile tu mwanaume rijari unashidwa kujikimu na kuna njemba hapo karibu anakukonyeza na kukuzengea na yuko tayari kutatua matatizo yako ya kiuchumi kama tu uko radhi kukata nae mtaa na kupoozaa kiu yake chafu, basi unaacha heshima yako yote na enzi yako na kujirahisi kwake??

  Kumradhi tena.
  Dowans ni sawa na Basha.
  Dowans ni Fisi aliyeweka chambo chake pale Ubungo ili tuiingie kwenye 18 zake atubararue.

  Kwa nini kila siku tunataka kutatua matatatizo yetu kwa njia zionekanazo rahisi lakini zilizo jaa mashaka?

  Utajiri ni kujaza fedha mifukoni mwetu au ni kuwa na nchi ilojaa huduma bora na yenye mazingira yanyoruhusu ukuaji wa uchumi na maendeleo?

  Ni lini kwetu kutakuwa kuzuri kama kwao?

  Ni nani atakaye fanya kwetu kuwe kuzuri kama kwao?
   
 13. Makaayamawe

  Makaayamawe JF-Expert Member

  #13
  Mar 27, 2009
  Joined: Feb 21, 2009
  Messages: 341
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Dar Es Salaam,
  Kwa vile tatizo hili la umeme lilikuwepo tokea 2005 na tokea mwaka jana chini ya hao hao viongozi wa sasa, Ngeleja na Dr.Iddris, lakini;
  1. Kwa furaha kabisa waliwaachisha kazi AGGREKO, kampuni mashuhuri duniani kwa umeme wa dharura/kukodisha, na badala yake
  2. Wakawabakisha DOWANS wasiojulikana wamiliki wala uwezo wao kiutendaji,
  Kwa nini tusiwabadilishe hao viongozi na kuweka wenye maamuzi mazuri, k.m. ya;
  1. Kubakisha reputable company kama ya AGGREKO kwa ajili ya emergency mpaka TANESCo watakapopata mitambo yao na
  2. Kuwafilisi DOWANS kwa udanganyifu na kutotimiza masharti ya mkataba?
  Je hapa si tutakuwa tumetatua tatizo la kiuongozi na hapo hapo kupata umeme?
   
 14. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #14
  Mar 27, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Chadema wamepata tenda ya kupambana na mafisadi hawana jipya.
   
 15. rmashauri

  rmashauri JF-Expert Member

  #15
  Mar 27, 2009
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 3,008
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Weee ndugu yetu, vipi na rafiki yakp Dar es Salaam? Hujui kuwa mafisadi wamejulikana kwa sasabu ya CHADEMA ambao walianzisha mpambano dhidi ya EPA then Richmond? Mbona unakuwa hivyo au nawe ni mnufaika wa akina Rostam wasiopenda kuona maendeleo ya nchi hii wao wanalala na kuamka wakibuni ni namna gani wanaweza kuikamua nchi yetu? Jirekebishe ndugu yetu na tuungane kwa pamoja kuikomboa hii nchi ambayo imefanywa kuwa shamba la bibi.
   
 16. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #16
  Mar 27, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Tatizo makelele yao hayana mafaida zaidi ya kusaidia makundi au mitandao ndani ya CCM,unaweza kusema yalianzishwa na Chadema na iwe hivyo ,hadi wameanzisha hadi hii leo nini WaTz wamefaidika,hatua gani zimetimizwa,nani wamechukuliwa hatua ,na hapa tulipofikia shida zipo kwa nani ?

  Sawa kama unavyotaka tuamini kuwa CHADEMA ndio waanzilishi wa mapambano hayo ya mafisadi sasa,hebu tuambieni enyi wapenzi wa CHADEMA ni wapi mlipofikia ,naona siku zinakwenda na kila siku mnazuka na kuibua mepya What the hell of these zoezi ,kila mkiambiwa kuwa haya hayatamwokoa Mtz kutoka kwenye ukali wa maisha bado mmeshikilia tu ,sasa mnafanya kuaminike kuwa mnatumika au mnatumiliwa kuibua siri za kundi fulani ndani ya CCM ili iwe rahisi kwa wao kuzomeana na kuangushana ,na sio kuanguka kwa CCM ,maana kama haya mazoeizi mnayofanya yangekuwa yanaihatarisha CCM kuanguka tungesema kweli yanasaidia katika kumuondoa Sultani CCM alietawala kwa zaidi ya miaka 50 ,lakini hakuna hata dalili zaidi ya kubomoana wao kwa wao asubuhi na jioni wanakutana kupanga jingine ,kwa ufupi CCM yao yanawaendea mbali ya kukabana shingo mwisho wa siku wanaelewana ,natumai nimeeleweka hapo.

  Sasa mbio za CHADEMA zinaonekana kuwasaidia CCM kuliko wao wapinzani na sasa kuna kutofahamiana ndani ya CHADEMA japo wenyewe wanapinga kwa nguvu zote lakini ukweli siku zote unakuja juu. Uchaguzi wenu lini ?
   
 17. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #17
  Mar 27, 2009
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Sharti lipi la mkataba ambalo Dowans hawakutimiza?
   
 18. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #18
  Mar 27, 2009
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Sawa, unahaki ya kuwa na shaka kwa ukipendacho, hilo ni tatizo lako si langu. Tatizo langu ni umeme kwa sasa na nauliza hivi: kama Dowans wanamakosa yoyote kisheria kwa sasa, kwa nini wasishitakiwe? simpo!
   
 19. kinepi_nepi

  kinepi_nepi JF-Expert Member

  #19
  Mar 27, 2009
  Joined: Aug 16, 2007
  Messages: 870
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Chadema wana njia mbili za kuchagua ama wambebe Zito kwenye swala la dowans nao waende nae chini na kuingia mgogoro mkubwa na wapiga kura, kwani ni vigumu sana kumwelewa Zito na uhusiano wake na akina Rostam, na kama songas wamesema ile mitambo haifai kibiashara hivyo hawawezi kuinunua kwanini zito ameipigia chepua fedha za wavujajasho zipotee.

  Pili Chadema wamtose Zito wajenge chama kwani Dr Slaa anaonekana wazi anapata kigugumizi kikubwa sana kuhusu Zito huwezi msapoti Mwakyembe halafu ukambeba Zito, Zito kawa kasa that was political sucide for mr Zito wamwache aende down Chama kiende mbele. Kwa kufanya hivyo Chadama wataonyesha tofauti kubwa na Sultan ila siasa za kulindana zimetufikisha pabaya sana. Zito anatakiwa ajioshe mwenyewe sio Slaa.
   
 20. N

  Ngekewa JF-Expert Member

  #20
  Mar 28, 2009
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 7,730
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Aisee nilianza kujiweka tayari baada ya kuona heading only to be dissapointed to find the same song be sung here again.
  Nini jipya kwa Waziri Ngeleja na Masha au Dr Rashid? tumeandika na kuandika hadi thread zimetrail off. Naanza kuhisi kuwa kuposti thread kunaweza kukawa deal hapo mbeleni. Mtangulia hugwa pema.
   
Loading...