CHADEMA yalalamika viongozi wake wa nyumba 10 kutotambuliwa na Serikali na Jeshi la Polisi nchini

Ubaguzi wa kichama ndani ya serikali yetu huenda ukazaa msukule hivi karibuni endapo mwenendo huo hautobadilika kwa udhati na haraka kote nchini.
 
mimi sidhani kama upo uelewa wa kutosha kwa muundo wa serikali ulivyo kwa waliwengi, haswa baada ya mfumo wa vyama vingi. kiufupi mjumbe wa nyumba kumi ni wa chama husika na hivyo awe wa updp/cck/cdm/ccm/tlp/cuf, hawamo ktk structure ya serikali. na kuendelea kulijadili hili ni moja ya kigezo tosha cha aina ya wanasiasa tulionao leo. kimsingi kila chama kinanayo fursa ya kuwa na mjumbe wake kwa kutegemea na muundo wake na ambaye kimsingi hujachaguliwa na wanachama wenzake na hatimaye anajihusiha na mambo yanayohusu chama chake na si vinginevyo. naomba nieleweke kuwa upo wakati wanasiasa kuwatumia mabalozi wao na wakati mwingine kwa kuwapatia majukumu ya kukusanya michango hususani ktk serikali zetu za mitaa, kitu ambacho ni makosa, na kwa sasa maeneo mengi wameliona hili na hata polisi kwa sasa huwatumia wajumbe wa serikali hizo za mitaa na vitongoji ama vijiji.
 
utakuwa hauelewi siasa za field wewe, we bakia kwenye internet tu.

Sangarara kweli kama ulivyosema, ni bahati mbaya sana kwamba tuna wataalamu wengi wa siasa za mitandao ya kijamii wasiojua battle ya huko field ikoje.
Watakapotangaziwa kwamba mabalozi wa nyumba kumi, wa vyama vyote wameondolewa kwenye mfumo wa utendaji wa kiserikali ndipo watajua kwamba Chadema wanajua sana wanachokifanya katika siasa za nchi hii.
Chadema imeshaanza rasmi kuwatumia wajumbe wa nyumba kumi. Hata kama ikitokea vyama vingine kama cuf imeshindwa kuweka wajumbe wa nyumba kumi lakini huu mkorogano wa wajumbe wa Chadema vs wa ccm utasaidia sana kuwaondoa wajumbe wa ccm katika mfumo wa kiserikali ama kuwatambua wa Chadema katika mfumo huo.
 
Last edited by a moderator:
huko siyo kuinga ya ccm ? maana jamaa walipoenda jangwani iliandikwa sana kuwa wanaiga,sasa mvumo wa mabalozi wa nyumba kumi hapa nchini kwetu ni wa ccm je siyo kwamba sasa mmeanza kuiga ?
 
Sangarara kweli kama ulivyosema, ni bahati mbaya sana kwamba tuna wataalamu wengi wa siasa za mitandao ya kijamii wasiojua battle ya huko field ikoje.
Watakapotangaziwa kwamba mabalozi wa nyumba kumi, wa vyama vyote wameondolewa kwenye mfumo wa utendaji wa kiserikali ndipo watajua kwamba Chadema wanajua sana wanachokifanya katika siasa za nchi hii.
Chadema imeshaanza rasmi kuwatumia wajumbe wa nyumba kumi. Hata kama ikitokea vyama vingine kama cuf imeshindwa kuweka wajumbe wa nyumba kumi lakini huu mkorogano wa wajumbe wa Chadema vs wa ccm utasaidia sana kuwaondoa wajumbe wa ccm katika mfumo wa kiserikali ama kuwatambua wa Chadema katika mfumo huo.

Huu ni ushahidi kwamba CHADEMA imedhamiria kuiondoa CCM Madarakani comes 2015, sababu wanaadvance in every battle field.
 
Back
Top Bottom