CHADEMA yalalamika viongozi wake wa nyumba 10 kutotambuliwa na Serikali na Jeshi la Polisi nchini | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CHADEMA yalalamika viongozi wake wa nyumba 10 kutotambuliwa na Serikali na Jeshi la Polisi nchini

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Jun 26, 2012.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Jun 26, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  JUMATATU, JUNI 25, 2012 05:16

  NA BENJAMIN MASESE, DAR ES SALAAM

  Na Gazeti la MTANZANIA

  CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimewataka viongozi wa Serikali na Jeshi la Polisi nchini, kuwatambua wajumbe wa nyumba 10 wa chama hicho cha upinzani, kwa kuwa nao ni viongozi halali.

  Pia kimesema kuwa, kitendo cha wajumbe hao kubaguliwa, hakiwezi kukubaliwa kwa kuwa wamechaguliwa kwa mujibu wa sheria.

  Akizungumza na wandishi wa habari Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa Uchaguzi CHADEMA, Msafiri Mtemelwa, alisema hivi sasa kuna mvurugano mkubwa wa kiutawala ndani ya jamii kuhusu wajumbe wa nyumba 10.

  "Sisi zamani hatukuwa na wajumbe wa nyumba 10, lakini baada ya kuona hatuwezi kuchukua nchi bila kuwa na mizizi hadi chini, tumeweka viongozi hao na wanatambuliwa kisheria.

  "Pamoja na kwamba wanatambulika, jambo la ajabu ni kwamba, mtu akipata shida na kuwenda kwa mjumbe wa nyumba 10 wa Chadema kisha akapeleka barua hiyo kituo chochote cha polisi, hatapokelewa.

  "Lakini mtu huyo huyo akienda kituo cha polisi na barua ya mjumbe wa nyumba 10 wa CCM, anasikilizwa vizuri na kupewa kila aina ya msaada anaotaka.

  "Sasa tunahoji kwa nini mjumbe wa Chadema asitambuliwe na mjumbe wa CCM atambuliwe wakati wote hao ni wawakilishi wa vyama vya siasa?

  "Huu ni ubaguzi wa hali ya juu na hatuwezi kuukubali, bila shaka hii ni mbinu ya CCM kutaka kuendelea kuwalazimisha wananchi kwamba mabalozi wa CCM, ndio wenye uhalali wanaotambulika katika maeneo husika.

  "Kwa kifupi hatuwezi kukubali hali hii, wajumbe wetu wa nyumba 10 wapo kisheria na wanatambuliwa kama ilivyo kwa wajumbe wa CCM," alisema Mtemelwa.

  Mtemelwa alisema kuwa, tangu Juni mosi mwaka huu, Chadema ilipoanza kuwaweka mabalozi katika maeneo mbalimbali nchini na kufanya kazi kama mabalozi wa CCM, baadhi ya wananchi wamekuwa wakikosa huduma pale wanapofika katika vituo vya polisi, ofisi za mtendaji wa kata na sehemu nyingine za Serikali, wakiwa na barua zilizotolewa na viongozi hao.

  Kutokana na hali hiyo, alitoa wito kwa viongozi wasiowatambua wajumbe wa nyumba 10 wa Chadema, kutoendelea na tabia hiyo vinginevyo watachukuliwa hatua za kisheria.

   
 2. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #2
  Jun 26, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Polisi tuache ubaguzi, hatujifunzi ya Zambia?
   
 3. Filipo

  Filipo JF-Expert Member

  #3
  Jun 26, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 9,330
  Likes Received: 210
  Trophy Points: 160
  Ingekuwa uamsho, makanisa yangechomwa moto!
   
 4. Fredrick Sanga

  Fredrick Sanga JF-Expert Member

  #4
  Jun 26, 2012
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 3,148
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Hata wajumbe wa nyumba kumi wa CCM ni wa CCM hawatakiwi kuandika chochote kwenda serikalini. Mjumbe wa nyumba kumi anayejishughulisha na maswala ya watu wasio wanachama wake anafanya utapeli tu. CDM angalieni hii vita kwa umakini. police anayepokea barua ya mjumbe wa nyumba kumi anatakiwa kushitakiwa, maana anakua ameingiza siasa sehemu ya kazi. Washitakini wjumbe wa CCM kwa kuingilia shughuli za serikali za mitaa.

  Hii ni matatazo ya chama dhaifu. Hakioni haya kufanya mambo ya ajabu. Wamefanya makusudi kutoingiza uchaguzi wa wajumbe wa nyumba kumi katika uchaguzi wa serikali ya mitaa ili waendelee kuburuza wananchi, shame, shame, shame on you. Lakini sasa wameshajitengenezea jinai. Police wanachanganywa maana wanaenda kwa mzoea, hawatakiwi kupokea CCM wala CUF wala CDM katika level ya wajumbe, mpaka sheria zitakaporekebishwa.
   
 5. Kurunzi

  Kurunzi JF-Expert Member

  #5
  Jun 26, 2012
  Joined: Jul 31, 2009
  Messages: 4,003
  Likes Received: 325
  Trophy Points: 180
  CCM walifuikiri watatawala milele nakumbuka wakati tunaingia kwenye mfumo wa vyama vingi upinzani hasa CDM waliitaka serekali kuwatambua rasmi hawa mabalozi kwenye mfumo wa utawala ngazi ya chini kiserekali lakini ccm wakagoma.
   
 6. MANGUNGO

  MANGUNGO JF-Expert Member

  #6
  Jun 26, 2012
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 1,538
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 133
  Watawatambua tu siku moja!!
   
 7. ALEX PETER

  ALEX PETER Senior Member

  #7
  Jun 26, 2012
  Joined: Jan 17, 2012
  Messages: 117
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  8-chadema.jpg
  CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kupitia Kurugenzi ya Kampeni na Uchaguzi inapenda kutoa taarifa kwa umma na kukemea ubaguzi unaofanywa na baadhi ya watendaji wa serikali dhidi ya viongozi wa vyama vya siasa, hususan wale wa chama kikuu cha upinzani na chama mbadala, CHADEMA.

  Chama kupitia Kurugenzi ya Kampeni na Uchaguzi kimepata taarifa kutoka ngazi ya chini ya uongozi, yaani misingi na matawi kwamba mabalozi wa nyumba kumi wa CHADEMA wamekuwa wakibaguliwa katika utendaji kazi wao wa kila siku na watendaji wa serikali, huku watumishi hao wakiendelea kutoa ushirikiano kwa mabalozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).

  Ndugu wanahabari kupitia kwenu, tunaomba umma wa Watanzania ufahamu mambo mawili muhimu hapa;

  Kwanza; balozi wa nyumba kumi wa chama cha siasa si sehemu ya uongozi wa kiserikali. Suala hili limewahi kusisitizwa na serikali yenyewe kwa kutoa kauli bungeni. Ngazi rasmi ya uongozi wa kiserikali inaanzia serikali za mitaa/kitongoji.

  Lakini pia suala hili la ngazi za uongozi wa kiserikali na kuwa mabalozi si sehemu ya uongozi huo linaoneshwa pia katika katiba yetu ya sasa (pamoja na ubovu wake uliotusukuma tudai iandikwe upya).

  Pili; Sheria ya Vyama vya Siasa ya Mwaka 1992, inavitambua vyama vya siasa vyenye usajili wa kudumu kuwa vyote viko sawa mbele ya sheria. Halikadhalika kutokana na sheria hiyo, katiba za vyama vyote vya siasa ni sawa, hasa baada ya kuwasilishwa na kupitishwa kwa Msajili wa Vyama vya Siasa na kupitishwa.

  Kwa mantiki ya masuala hayo mwili hapo juu, Kurugenzi ya Kampeni na Uchaguzi, inatumia fursa hii kutoa tamko kwa umma kuwa mabalozi wa CHADEMA na CCM, wana haki sawa mbele ya sheria, kwa sababu wanatokana na vyama vilivyo sawa mbele ya sheria, halikadhalika katiba za vyama hivyo ziko sawa mbele ya sheria.

  Mabalozi wa CHADEMA wanapatikana kwa mujibu wa Katiba Mpya ya Chama ya Mwaka 2006, Sura ya Saba, ambayo inazungumzia ngazi, uongozi na majukumu ya vikao.

  Tofauti pekee ya mabalozi wa CHADEMA na CCM ni kwamba mabalozi wa CHADEMA wanavaa magwanda wale wa CCM wanavaa magamba. Lakini pia wanatofauti ya tabia;
  Mabalozi wetu wanasimamia ukweli, wakati wale wa CCM wanasimamia uongo, mabalozi wa CHADEMA wanasimamia uadilifu, wale wa CCM wanasimamia ufisadi, wakati mabalozi wetu wanasimamia na kutumikia wananchi, wale wa CCM wanatumikia maslahi ya chama chao na yao binafsi.

  Pamoja na kazi zingine, baadhi ya majukumu ya balozi wa CHADEMA ni pamoja na kuwa mwakilishi wa chama na wanachama. Ana wajibu wa kuwatambua wanachama wenzake, wananchi wote na pia anaufahamu wa kutosha wa masuala mbalimbali katika eneo lake la nyumba kumi.

  Tunasema hivyo kwa sababu wakati mwingine kutokana na kukosa mtandao mpana mpaka chini katika kaya za watu na wakati mwingine ukubwa wa maeneo ya kitongoji/mtaa unakuwa kikwazo, mamlaka za serikali katika kutekeleza majukumu mbalimbali zinashindwa kumtambua kila mwananchi, hivyo zinalazimika kuhitaji mtu/watu wa kusaidia kazi hiyo katika nafasi za uongozi walizoaminiwa katika maeneo madogo ambayo ni rahisi watu kutambuana. Hapo ndiyo dhana ya kuwa na kiongozi wa kaya kadhaa kwa jina la balozi unatokea.

  Mabalozi wetu CHADEMA kwa sababu wanatokana na taasisi inayotambulika kisheria, makini na imara wanafanya kazi kwa barua na mhuri wa chama.

  Kupitia tamko hili, Kurugenzi ya Kampeni na Uchaguzi ya CHADEMA, inawataka watendaji wa ngazi zote wa serikali kuacha mara moja tabia ya kuwabagua mabalozi wa CHADEMA kwani wanatokana na watu, wanatambua na wanaweza kutimiza wajibu wanaopaswa kufanya.

  Chama pia kinatumia fursa hii kutoa mwito kwa mabalozi wote wa CHADEMA nchi nzima ambao wanakutana na vikwazo vya watendaji wa serikali katika kutimiza majukumu yao mbalimbali ya kila siku, watoe taarifa rasmi kwa ngazi za juu zao, ili ngazi hizo husika nazo ziwasilishe kunakohusika, kwa ajili ya chama kuchukua hatua zaidi.
  [FONT=&quot]
  [/FONT]
  Imetolewa Juni 24, 2012 Dar es Salaam na
  Msafiri Abdulrahaman Mtemelwa
  Mkurugenzi wa Kampeni na Uchaguzi CHADEMA
  [FONT=&quot][/FONT]
   
 8. Sangarara

  Sangarara JF-Expert Member

  #8
  Jun 26, 2012
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 13,048
  Likes Received: 549
  Trophy Points: 280
  Hivi huyu msafiri naye ni muislamu. au hiki chama ni cha kiislamu jamani?
   
 9. Communist

  Communist JF-Expert Member

  #9
  Jun 26, 2012
  Joined: Jun 1, 2012
  Messages: 5,391
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Ritz anajua, atakwambia jina la bandia.
   
 10. zaleo

  zaleo JF-Expert Member

  #10
  Jun 26, 2012
  Joined: Dec 6, 2011
  Messages: 1,733
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 145
  Mmm, chichemi mie. chijachikia njomba
   
 11. WA-UKENYENGE

  WA-UKENYENGE JF-Expert Member

  #11
  Jun 26, 2012
  Joined: Oct 1, 2011
  Messages: 2,904
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 160
  Huwezi kujua madhara ya hiyo sentensi yako hadi yatakapotokea.
   
 12. Nduka

  Nduka JF-Expert Member

  #12
  Jun 26, 2012
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 8,479
  Likes Received: 761
  Trophy Points: 280
  Wanawatumia kama kondomu ma yuda iskarioti.
   
 13. DOUGLAS SALLU

  DOUGLAS SALLU JF-Expert Member

  #13
  Jun 26, 2012
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 11,595
  Likes Received: 4,707
  Trophy Points: 280
  Kama wewe unavyotumiwa na mafisadi wenye mabilioni huko Uswiss hali wewe unaambulia posho ya ya kuganga njaa toka kwa nepi.
   
 14. webondo

  webondo JF-Expert Member

  #14
  Jun 26, 2012
  Joined: Apr 29, 2012
  Messages: 1,724
  Likes Received: 110
  Trophy Points: 160
  Nimepita
   
 15. Bilionea Asigwa

  Bilionea Asigwa JF-Expert Member

  #15
  Jun 26, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 12,627
  Likes Received: 9,838
  Trophy Points: 280
  du...sisiem ina mbinu chafu sana...hata huku kwenye vyombo vya usalama??
   
 16. Sangarara

  Sangarara JF-Expert Member

  #16
  Jun 26, 2012
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 13,048
  Likes Received: 549
  Trophy Points: 280
  Hiyo sentensi ni matokeo ya madhara yaliyopo mpaka sasa mkuu
   
 17. Ndallo

  Ndallo JF-Expert Member

  #17
  Jun 26, 2012
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 7,131
  Likes Received: 1,088
  Trophy Points: 280
  Wajumbe wa nyumba 10 CCM wanachojua nikusuluhisha ndoa za watu tu! That is all I know.
   
 18. Tuko

  Tuko JF Bronze Member

  #18
  Jun 26, 2012
  Joined: Jul 29, 2010
  Messages: 11,186
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  Malalamiko mengine sio hadhi ya chama makini kama CDM. Tujiheshimu
   
 19. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #19
  Jun 26, 2012
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  MGOGORO WA KI-KATIBA UNANUKIA NCHINI KITENDO CHA CCM KUDAIWA KUKWAMISHA UTENDAJI KAZI WA SERIKALI MASHINANI ETI KWA SABABU TU YA WAJUMBE KUTOKEA UPINZANI

  Haya madai ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (JMT) kudaiwa kuwa ni KIKWAZO KIKUBWA KWA UTENDAJI KAZI MURUA hadi mashinani eti kwa madai tu kwamba mjumbe fulani ni wa kutoka chama cha upinzani.

  Hakika hili ni jambo ambalo si adui tu wa dhana zima ya demokrasia ya vyama vingi nchini bali hadi hapo ni kwamba taaifa letu litakua limejielekeza moja kwa moja kuingia kwenye MGOGORO MZITO WA KIKATIBA nchini.

  Hili si jambo la kuchezea kwani ni jambo ambalo ni NYETI kuliko kawaida hili! Demokrasia tayari imeingia mtihani hapa!!! Maana ya kitendo kama hiki ni kwamba Serikali ya CCM haikubali Mfumo wa vyama vingi nchini.

  Hiyo si kazi ya CHADEMA tena bali ni kazi za John Tendwa kuhakikisha kwamba Demokrasia inapewa nafasi kufanya kazi yake kwa vyama vyote kote nchini.

  Ndio nasema ni jukumu la Waziri wa Mambo ya Ndani kuhakikisha kwamba serikali kamwe HAIKIUKI KATIBA YA NCHI inavyosema hivyo ni jukumu lake kuamuru vyombo vyake vyote vya usalama kufuata maelekezo ya katiba katika utendaji wao kazi wa kila siku.

  Naam, ni vema ikaeleweka kwa vyombo vya usalma kwamba wao wamewekwa na katiba na wala hawajawekwa na chama cha siasa ofisini. Hivyo ni jukumu lao wenyewe kuhakikisha kwamba wajumbe wa nyumba 10 waliopatikana kwamujibu wa sheria na maelekezo ya katiba ndio wanaokua washirika wao na wadau katika masuala ya kiutawala.

  Ndio, wafanyakazi wote wa serikali ni wafanyakazi wetu sote na wala si mali ya chama fulani na ndio maana kila siku tunawalipa nje ya mipaka ya itikadi zetu za kisiasa kupitia kodi zetu. Sasa pale kunapotokea ripoti eti mtumishi kama huyu sasa anaanza kuwa mbaguzi wa chama gani kukitumikia - ni kosa kubwa hilo!!!!

  Mhe John Tendwa ofisi yako itakua inashindwa kazi jambo hili likionekana kuendelea hata kwa siku moja zaidi nchini.

  Polisi wafanye kazi kwa mujibu wa katiba na sheria za nchi kwa kushirikiana na wadau wote HALAI na wala si kufuata maelekezo ya chama kimojawapo cha ushindani (interested political party - CCM) kwa maelekezo yanayoweza kuibua mgogoro wa ki-katiba ndani ya nchi kwa sekunde chache tu.

  Nasema hili jambo linaloonekana dogo mbele yetu leo, likiachwaa likaendelea hivo bila kudhibitiwa huenda likasababisha sokomoko ambalo halikutarajiwa hata siku moja.

  Hatari iliopo ni kwamba wale wajumbe halali, ingawaaje ni wa kutoka vyama vya upinzani, waakiendelea kukataliwa sana na kubaguliwa na serikali ya CCM wao huenda wakajitengenezea 'MFUMO USIORASMI' wa kupitishia shughuli zote zao zaa kiutendaji. Na mfumo kama huo ukizaliwa nchini huenda ukawa vigumu kuiondoa baadaye.

  Kuna hatari kubwa y huu ubaguzi wa serikali ya CCM kwa watendaji mashinani ukazaa saratani itakayopanda juu hadi wizarani watu tukawa na mafisa waserikali lakini wa CUF, DC Handeni lakini wa NCCR-Mageuzi, Mlinzi wa Rais lakini akiwa ni mtendaji mwaminifu wa CHAADEMA.

  Nasema Wazee hebu tutafakari kidogo kama kweli hivi sasa baada ya kuwa na VYMA VINGI nchini hivi sasa ni kwamba kweli pia tunatamani uwepo wa SERIKALI NYINGI ndani ya taifa moja???? Ndio mfumo wa wapi huo??

  Kumbukeni kwamba kitendo cha Serikali ya CCM kukataa kuwapa ushirikiano uongozi wa serika za nyumba 10 zilizochaguliwa na wananchi wenyewe huenda ukageuka GHRIKA la serikaali yenyewe nalo KUKATALIWA na wananchi kote kwenye maeneo yao; hakuna hta mmoja wetu anayetamani kuona hali kama hiyo ikitokea nchini.

  Sasa ndio tusema tunafanya mambo gani kwa CCM kuleta mambo ya ukeweza kwenye mfumo rasmi wa kiserikali tunaougharimia sote wana-CUF, NCCR Mageuzi, CHDEMA pamoja na vyama vinginevyo na hali hiyo imepangwa kuendelea hadi lini kabla ya kuleta tafrani miongoni mwa wananchi??

  Ushindani wa kisiasa tukauendeleze kwa sana tu kote nchini lakini KAMWE Busara za kuzaliwa na utaifa mbele kma tai katika kila jambo tulitendalo lisije likatutoka hata siku moja - wadau wote zingatieni maneno haya machche.
   
 20. Ringo Edmund

  Ringo Edmund JF-Expert Member

  #20
  Jun 26, 2012
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 4,895
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  Chadema ianzishe na jeshi lake.
   
Loading...