CHADEMA yalaani dhamira ya Serikali kukataza Mikutano ya hadhara ya vyama vya Siasa

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,658
55,487
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI KUHUSU KAULI YA WAZIRI MKUU MIKUTANO YA HADHARA

Tumeona kupitia vyombo vya habari na njia mbalimbali za upashanaji taarifa kwamba Waziri Mkuu Majaliwa Kassim amenukuliwa akitoa kauli inayoonesha Serikali ya CCM inataka kuzuia shughuli za kisiasa hususan mikutano ya hadhara.

Kupitia kauli hiyo, Waziri Mkuu amenukuliwa zaidi akisema kuwa Uchaguzi umekwisha hivyo sasa si wakati wa siasa bali maendeleo.

Hii ni kauli ya ajabu kutolewa na mtu anayesimamia utendaji wa shughuli za kila siku za serikali inayotaka kuwaaminisha kuwa itakuwa tofauti na serikali zingine zilizopita za CCM.

Kupitia taarifa hii, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) tunailaani na kuipinga kwa nguvu zote kauli hiyo yenye chembe za udikteta iliyotolewa na Waziri Mkuu Majaliwa.

Inaonekana imetolewa na mtu ambae ameanza kulewa madaraka mapema sana huku akisukumwa na utashi wa kisiasa wa kuiokoa CCM kwenye kasi ya kufa kisiasa na kulinda udhaifu wa serikali yao ambao umeshaanza kuonekana wazi kupitia kila hatua wanayochukua na matamko wanayotoa.

Kama wao (CCM) ndiyo walioshinda kama ambavyo Waziri Mkuu Majaliwa amesema na kwamba wanaendelea kutekeleza wajibu waliokabidhiwa na wananchi, tunahoji hofu yao nini hasa wakiona au wakisikia CHADEMA wanapanga kwenda kuongea na wananchi? Wanaogopa nini?

Kauli hiyo ya Waziri Mkuu Majaliwa imekuja siku chache tu baada ya kiongozi huyo mwandamizi wa serikali ambaye anatazamiwa kuwa mtumishi wa Watanzania wote bila kuwabagua kwa itikadi za kisiasa, kabila wala dini, kuwa ametoa upendeleo kwa chama kimoja cha siasa ambacho ni CCM kuhutubia na kufanya siasa kwenye mkutano wake mjini Lindi, ambapo Nape Nnauye alitumia jukwaa hilo la kiserikali kuzungumza kama kiongozi wa CCM akiwajibu viongozi wa vyama vinavyounda UKAWA.

Matukio haya yanaanza kumdhihirisha Waziri Mkuu Majaliwa ni kiongozi mwenye uelekeo wa namna gani hivyo kuanza kuifunua Serikali ya Rais John Magufuli chini ya CCM kwa miaka mitano ijayo itawapeleka wapi Watanzania.

Ni dalili za wazi za watu waliolewa madaraka na
kuchoka kuwa viongozi na sasa wanataka kuwa watawala wenye kudhani kuwa fikra zao ndizo zinazongoza nchi badala ya misingi ya inayokubalika miongoni mwa jamii nzima kupitia Katiba, Sheria, Kanuni na taratibu mbalimbali.

Tunatumia fursa hii kusisitiza kauli yetu kwamba walioko madarakani wanapaswa kutambua kuwa siasa haina msimu wala haianzi na kuishia wakati wa uchaguzi kwa sababu siasa ni mfumo wa maisha ya binadamu kila siku. Si suala la kupenda au kutokupenda.

Uchaguzi pia ni mchakato. Mwisho wa uchaguzi mmoja ndiyo mwanzo wa maandalizi ya uchaguzi mwingine kwa haraka kwa wadau wote, vikiwemo vyama vya siasa na vyombo vingine au taasisi zingine zote zinazohusika. Kuendelezwa kwa fikra za namna hiyo za Waziri Mkuu ndiyo kunasababisha Serikali na taasisi kama Tume ya Taifa ya Uchaguzi kuvunja sheria za nchi kwa kushindwa kuandikisha wapiga kura kama inavyotakiwa baada ya uchaguzi kumalizika.

Aidha kuheshimu misingi ya demokrasia, ikiwemo ushindani wa (hoja, sera, mikakati, mipango) wa vyama vingi, si suala la utashi wa walioko madarakani bali ni haki ya msingi ya kibinadamu na kikatiba na matakwa ya wanananchi wanaotoa dhamana ya watu kukaa madarakani kuongoza kwa niaba ya wengine.

Je Waziri Mkuu anataka kuwaambia Watanzania kuwa anatofautisha siasa na maendeleo? Je anataka kusema kuwa haki ya vyama vya siasa kukutana na kuzungumza na wananchi itabakia kwa CCM tu kwa miaka mitano ijayo? Anajua hilo halitakubalika.

Ni vyema Waziri Mkuu akatambua kuwa nchi hii haiko kwenye fikra wala mfumo wa chama kimoja tena.

Imetolewa leo Alhamis, Desemba 24, 2015 na;

Idara ya Habari na Mawasiliano

CHADEMA
 
CHADEMA hamna akili!
Mnaongelea kuhusu Demokrasia nitajieni nchi moja tu ya Kidemokrasia Dunia hii ambayo baada ya uchaguzi kuisha na Raisi kuapishwa wanasiasa wake wanaanza kampeni za uchaguzi ujao!
Kama ni hivyo kuna haja gani sasa ya Tume ya uchaguzi kuweka kipindi cha kampeni za kisiasa? au hata hilo pia hamulielewi? Bunge lina maana gani? Ni kwa nini mna Wabunge wameenda kufanya nini Bungeni?
 
Safi sanaa maccm hayajui hata maana ya democracy na wameshaanza kupwelepweta maana direction washakosa.
 
Yani ccm wanaishi kihofu hofu tu, vp makontena yameshalipiwaaa au ndo maigizo kama kawa
 
Chama cha kulialia tu hiki. PM kisha sema hakuna huu upuuzi, waagizeni wabunge wenu wakafanye hiyo kazi bungeni.watanzania wanataka kuona faida ya kuwaweka bungeni sio kuzurura kila sehemu na kusambaza umbea.serikali ya sasa ni serikali dume, haitaki upuuzi,KAENI MKIJUA HATA KIPIGO CHAKE NI CHA UHAKIKA
 
Safi sanaa maccm hayajui hata maana ya democracy na wameshaanza kupwelepweta maana direction washakosa.



Hata uwe ni kiongozi mzuri lakini unapokuwa ccm basi tayari ni jipu lililojaa usaa. Pinda yeye alikuja na wapigwe tu. Majaliwa yeye anazuia mikutano ya vyama vya upinzani. Hawa viongozi wa nchi hii ni sawa na mbwa mwitu aliyejivisha ngozi ya kondoo...
 
CHADEMA hamna akili!
Mnaongelea kuhusu Demokrasia nitajieni nchi moja tu ya Kidemokrasia Dunia hii ambayo baada ya uchaguzi kuisha na Raisi kuapishwa wanasiasa wake wanaanza kampeni za uchaguzi ujao!
Kama ni hivyo kuna haja gani sasa ya Tume ya uchaguzi kuweka kipindi cha kampeni za kisiasa? au hata hilo pia hamulielewi? Bunge lina maana gani? Ni kwa nini mna Wabunge wameenda kufanya nini Bungeni?

Wewe ni kubwa jinga. Siasa na mikutano ya siasa inasimamiwa kikatiba siyo matamko ya kukinzana ya watawala
 
matamko sio kuwa na msingi mbona yeye alikuwa kwao ruangwa alikuwa anafanya nn? sio kushukuru ache mihemko kila chama inahaki ya kufanya siasa
 
kuna amri mbili now ambazo zote ziko against na katiba na haki za binadaamu
1.marufuku mikutano ya siasa
2. kila jumamosi kila mtu 'lazima' shiriki siku ya usafi

Magufuli na huyo Majaliwa wote ni viazi.

Na Watanzania walivyo wapumbavu hata kuhoji iweje walipe kodi na ushuru halafu na fagio washike.

Wanabaki kusema 'hapa kazi tu'.

Monkey see monkey do.
 
Wewe ni kubwa jinga. Siasa na mikutano ya siasa inasimamiwa kikatiba siyo matamko ya kukinzana ya watawala

Uchaguzi umeisha kulikuwa na muda wa kutosha kufanya hayo yote ambayo chadema wanataka kuyafanya sasa hivi, kama wana mapendekezo, malalamiko, au ujumbe wowote ambao wanataka kuwafikishia Watanzania Bunge liko wazi kwa ajili hiyo na watasikiwa, ila mikutano ya kisiasa haina nafasi tena!

Na hii ni Dunia nzima siyo TanZania tu, kwamba uchaguzi ukishaisha raisi kuapishwa ndiyo mwisho wa kampeni na mikutano mikubwa ya kisiasa mpaka hapo Tume itakaporuhusu tena!
 
Majaliwa anachoweza ni ziara za kustkiza tu..

Hakuna lingine analoweza.
 
Huyu majaliwa anataka kupeleka nchi kusivyo kabisa.huo ni mwanzo wa udicteta.
 
Nakumbuka wakati flani hivi kikwete alisema huwezi ua inzi kwa nyundo!! Na sisi upinzani hatutatumia nguvu anayotegemea tutatumia sheria cose tuna Wanasheri wazuri kuliko wao.
 
CHADEMA hamna akili!
Mnaongelea kuhusu Demokrasia nitajieni nchi moja tu ya Kidemokrasia Dunia hii ambayo baada ya uchaguzi kuisha na Raisi kuapishwa wanasiasa wake wanaanza kampeni za uchaguzi ujao!
Kama ni hivyo kuna haja gani sasa ya Tume ya uchaguzi kuweka kipindi cha kampeni za kisiasa? au hata hilo pia hamulielewi? Bunge lina maana gani? Ni kwa nini mna Wabunge wameenda kufanya nini Bungeni?

Yaani wew ndio hujui siasa kabisa..wao hawapigi kampeni wanafanya mikutano ya hadhara kuwashukuru wanaichi na kueleza mipango ya chama..kwani kinana alivozunguka nchi zima mwaka jana alikua ktk kampeni..wew ZUZU kaa kimya km huna hoja..au umepewa ela ya sikukuu utoe uharo wko umu
 
CHADEMA lazima mlifikishe swala hili Mahakamani ili Mahakama itoe uamzi kama ni halali vyama vya siasa kuzuiliwa kuendesha mikutano ya kisiasa iwe ni kutoa shukrani,kutangaza sera au kampeni.

Lazima kutumia utaratibu uleule wa Mwanza wakti wa kutafuta HAKI ya kumzika Kamanda Mawazo.Tanzania haiko kwenye hali ya hatari hivo hizi marufuku hazina tija kwa nchi zaidi ya kutaka kuchochea hasira miongoni mwa Wanachama wa Upinzani na hivo Kupelekea maandamano ya kuidai HAKI hiyo ya KIKATIBA.
 
Back
Top Bottom