Chama cha Demokrasia na Maendeleo kinatishia kukitokomeza CCM katika jimbo la Iramba Magharibi.
CHADEMA kimeanza operesheni kubwa katika jimbo hilo ambapo imefanyika mikutano mfululizo katika Kata za Ndulungu,Kaselya na Kidaru.
Chama hicho leo kitashambulia kata ya Mtoa na kuanzia kesho kitawasha moto katika kata za Kiomboi,Ntwike,Shelui,Ndago,Kinampanda,Mgongo na Tulya.
Operesheni hiyo kubwa inaongozwa na Makamanda wa CHADEMA ambao ni Dr Kitila Mkumbo,Jesca Kishoa maarufu kama Iron Lady,David Djumbe na Makamanda wengine wa Singida.
Kwa hali inavyoonekana Chadema imeiva zaidi jimbo la Iramba Magharibi kuliko jimbo lingine lolote katika mkoa huo.Mamia ya wananchi wanachukua kadi za chama katika kila Kata na matawi yanafunguliwa mfululizo.
Pia kuna taarifa baadaye mwaka huu CHADEMA itakuwa na mikutano mfululizo zaidi ya 100 katika Jimbo hilo.[/QUOTE
Hali ya CDM IRAMBA MAGHARIBI ni nzuri mno. Mara kwa mara naenda huko na kukutana na wananchi wako na mwamko wa juu sana.
Nimekutana changamoto ya kutakiwa niwapelekee kadi na bendera watundike majumbani mwao. Nilizidiwa na mahitaji pamoja na upatikanaji wa hivi bendera kuwa mgumu hapa niko mwanza natafuta bendera.
Kitaeleweka tu.