CHADEMA yaitesa CCM Mbeya | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CHADEMA yaitesa CCM Mbeya

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Jul 28, 2012.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Jul 28, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) mkoani Mbeya kimeendelea kukitesa Chama cha Mapinduzi (CCM) kwa kujinyakulia makada wake wanane maarufu katika mtaa wa Soko Mwanjelwa Kata ya Ruanda, akiwemo Katibu mwenezi wa CCM wa kata hiyo, Baraka Mwakyabula.


  Makada hao walikabidhi kadi zao za CCM jana kwa Mwenyekiti wa CHADEMA Wilaya ya Mbeya Mjini, John Mwambigija, maarufu kama Mzee wa Upako, ambaye pia aliwakabidhi kadi mpya za CHADEMA.

  Mbali na Mwakyabula kuwa Katibu Mwenezi CCM Kata ya Ruanda pia alikuwa Katibu wa Hamasa wa Kata, Mjumbe wa Kamati ya siasa tawi la Ruanda, Mjumbe wa Mkutano Mkuu wilaya ya Mbeya na Mjumbe wa Mbaraza la Wazazi wilaya pamoja na Mwenyekiti wa Mtaa wa Soko Mwanjelwa.

  Makada wengine waliorejesha kadi za CCM na kukabidhiwa kadi za CHADEMA ni mabalozi saba waliotoka katika mtaa huo wa soko Mwanjelwa aliokuwa akiuongoza Mwakyabula ambao baadhi yao ni Chifu Adam Makatobe, Maneno Mwakabinga na Chifu Edward Mwakalukwa.

  Akikabidhi kadi yake kwa Mzee wa Upako, Mwakyabula alisema kabla ya kuchukua uamuzi huo aliamua kujiuzulu nyadhifa zake zote za ndani ya CCM na serikalini kwa kuandika barua alizozipeleka kwa viongozi wa CCM na Halmashauri ya Jiji la Mbeya.

  "Nimemwandikia barua Ofisa Mtendaji wa Kata ya kujiudhuru, lakini pia viongozi wa CCM wilaya nao nimekwishawapelekea barua ya kujiudhuru nyadhifa nilizokuwa nazo ndani ya chama," alisema.

  Akiwapokea wanachama hao wapya, Mzee wa Upako alisema kupokelewa kwa Mwakyabula ni kusajili timu nzuri katika mapambano ya kisiasa jijini Mbeya na kuwa sasa ndoto za CCM za kutaka kulirejesha jimbo la Mbeya Mjini kwenye uchaguzi wa mwaka 2015 ambalo kwa sasa linaongozwa na CHADEMA zimeyeyuka.
   
 2. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #2
  Jul 28, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145

  Yaani Pamoja na Speech Nzuri ya RAIS WETU MBEYA yaani ni Siku 5 zilizopita kwa Maringo kusifia Uwanja wa ndege

  Na Bwawa La Maji; Na Vijembe vyote na bado WANAHAMA????
   
 3. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #3
  Jul 28, 2012
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  kwani uwanja ni zawadi? au ni kodi ya watanzania au kikwete anadhani akiwajengea barabara na viwanja vya ndege atapunguza wimbi la wanaccm kuhamia chadema kuna kitu ccm haija tambua serikali yake itende haki, usawa hivi vinamana kubwa sana kuliko rami na viwanja vya ndege.
   
 4. O

  Ogah JF-Expert Member

  #4
  Jul 28, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 6,229
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  hawa mashemeji zangu wanajulikana kwa misimamo........tofauti yao na watu wa Iringa...ni kuwa wao hawajinyongi.....lol
   
 5. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #5
  Jul 28, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Nipo kwenye matanga ya CCM !
   
 6. Havizya

  Havizya JF-Expert Member

  #6
  Jul 28, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 1,573
  Likes Received: 169
  Trophy Points: 160
  Kwa hili mwambigija mzee wa upako nakupongeza, songa mbele songa mbele, kamwe usirudi wala kugeuka nyuma.
   
 7. zaleo

  zaleo JF-Expert Member

  #7
  Jul 28, 2012
  Joined: Dec 6, 2011
  Messages: 1,733
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 145
  CCM wanajifanya wajanja. Kitendo cha Kumlimboka mwana wa Mby kwa namna ile hata kusababisha wajukuu ambao wangekuja kuwa mashaka makubwa, mbali na kuwakyembe na kuwandosya kwa makusudi ati tu kwa sababu wanasema kile wanachoamini kuwa ni kweli kwa manufaa ya nchi, ni ushahidi tosha kwamba CCM na serikali yake wameichoka Mbeya. Ni wakati mwafaka sasa wanambeya kuitikia kwa umoja kwamba MBY na CCM ni "kya njinga na kya igali". Mkilala shauri yenu. mnaumwa na kupuliziwa kwa kupewa viti visivyo maalum na kupewa vuvuzela la kupuliza kuwazima fahamu zenu. Be smart, Liwalo na liwe.
   
 8. A

  Asa79 JF-Expert Member

  #8
  Jul 28, 2012
  Joined: Jul 19, 2012
  Messages: 591
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nasikia huko kenya "mombasa inataka kujitenga"............hongereni sn wana mbeya
   
 9. g

  great 2012 Member

  #9
  Jul 28, 2012
  Joined: Jun 27, 2012
  Messages: 23
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kama vip chama cha mafisadi (ccm) si mpeleke pingamizi mahakamani maanake ndio zenu
   
 10. S

  Sessy Senior Member

  #10
  Jul 28, 2012
  Joined: Jun 16, 2012
  Messages: 118
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mabadiliko hayaangalii hotuba nzuri watu wakiamua wameamua
   
 11. GreenCity

  GreenCity JF-Expert Member

  #11
  Jul 28, 2012
  Joined: May 28, 2012
  Messages: 4,652
  Likes Received: 2,100
  Trophy Points: 280
  Thats my City! Ila naomba hao waliopokewa wasipewe uongozi mapema...!
   
 12. maria pia

  maria pia JF-Expert Member

  #12
  Jul 28, 2012
  Joined: Jul 24, 2012
  Messages: 516
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  yap,nyanda za juu kusini ss wamefunguka....viva m4c
   
 13. U

  Ulimakafu JF-Expert Member

  #13
  Jul 28, 2012
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 17,991
  Likes Received: 733
  Trophy Points: 280
  Peoples....................
   
 14. Chademakwanza

  Chademakwanza JF-Expert Member

  #14
  Feb 28, 2015
  Joined: Jun 11, 2014
  Messages: 6,350
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Mbeya. Mwenyekiti wa Chadema mkoani hapa, Joseph Mwachembe maarufu kwa jina la China amesema chama chake hakina ndoto ya kuwapo kwa serikali ya mseto awamu ya tano ya uongozi wa nchi, kwa vile kimejiandaa kushinda kuanzia ngazi ya urais, ubunge hadi udiwani .
  China alisema Chadema inaamini kwa niaba ya Watanzania kwamba mwisho wa utawala wa CCM ni Oktoba mwaka huu, hoja za baadhi ya watu kwamba CCM ikikosa wabunge wengi ikubali kuunda serikali ya mseto ni propaganda za wafuasi wa CCM.
  Alitoa kauli hiyo alipoulizwa maoni ya chama chake kuhusu taarifa kwamba upinzani watapata wabunge wengi, lakini rais atatoka CCM katika uchaguzi ujao na kuishauri CCM ijiandae kuunda serikali ya mseto.
  Hivi karibuni mwanasiasa mstaafu Kanali Edmund Mjengwa (68) aliishauri CCM iwe na mawazo ya kujiandaa kuunda serikali ya mseto ikiwa rais atatoka CCM na wabunge wengi ndani ya Bunge wakawa ni wa upinzani.
  Naye Mbunge wa zamani wa Musoma Vijijini, Paul Ndobho alitoa kauli kama hiyo alipozungumza na mwandishi wetu Kanda ya Ziwa.
  Akifafanua hoja zake jana, China aliwasihi Watanzania kushika moja la kuwachagua wagombea wa chama kuanzia rais hadi madiwani ili kuundwa kwa serikali itakayofanya kazi kwa uhakika zaidi .
  Alisisitiza kwamba Chadema itashinda kwa wingi viti vya udiwani, ubunge na urais na kwamba hawana ndoto za kuwapo kwa mseto.
  Naye Mwenyekiti wa CUF mkoani hapa Yassin Mrotwa akitoa maoni yake alisema CUF ina uhakika kwamba CCM imefika kikomo kwa sababu Watanzania wamechoshwa na ufisadi uliopo serikalini.
  Wafanyakazi wamechoshwa na kukopwa fedha zao kupitia mishahara hata mifuko ya hifadhi, wakulima wamechoshwa kukopwa mahindi na mpunga,” alisema na kuongeza: “Kibaya zaidi ni kwamba CCM haina mgombea safi na makini.”

  Chanzo: Mwananchi
   
Loading...