CHADEMA yairarua tena CCM | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CHADEMA yairarua tena CCM

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by abdulahsaf, May 8, 2012.

 1. a

  abdulahsaf JF-Expert Member

  #1
  May 8, 2012
  Joined: Aug 31, 2010
  Messages: 859
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  [TABLE]
  [TR]
  [TD="bgcolor: #ffffff"][TABLE]
  [TR]
  [TD]
  • Yazoa wanachama 1300

  na Happiness Matanji, Iringa


  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [/TD]
  [TD="width: 140, bgcolor: #ffffff"][​IMG] [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD][TABLE]
  [TR]
  [TD]ZAIDI ya wanachama 1300 wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kutoka mikoa ya Simiyu, Morogoro na Njombe wamekihama chama hicho na kujiunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).
  Katika mkoa wa Njombe pekee, wana CCM 600 walijiunga na CHADEMA na wengine 421 kutoka mkoa wa Simiyu wakati wa ziara iliyofanywa na timu ya baadhi ya wabunge wa chama hicho.
  Wabunge hao katika mkoa wa Njombe, licha ya kufungua matawi matatu na ofisi moja ya kata, naye kada wa siku nyingi wa CCM, Martin Mohamed Kaduma (72), aliwasihi wazee kujiunga na CHADEMA kama alivyofanya yeye.
  “Mimi nimefanya kazi na chama hiki toka mwaka 1954 na nimepitia kila cheo. Hapa Majembe nimetengeneza barabara lakini nikajikuta na mimi ni mwizi kutokana na mfumo uliokuwepo. Nimesema sasa basi nahamia CHADEMA chama cha wapenda haki,” alisema Kaduma katika mikutano iliyohutubiwa na wabunge Peter Msigwa wa Iringa Mjini, Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi, na wa Mbozi Magharibi, David Silinde.
  Huko Simiyu, wanachama waliojiunga wanatoka katika wilaya za Maswa na Meatu juzi katika mikutano tofauti ya hadhara iliyofanyika katika mji wa Nyalikungu wilayani Maswa na Mwanhuzi wilayani Meatu iliyohudhuriwa na maelfu ya wananchi.
  Mikutano hiyo iliyohutubiwa na wabunge, Meshack Opulukwa wa jimbo la Meatu na Slivester Kasulumbayi wa Maswa Mashariki walisema wameamua kuhama kwa vile serikali inayoongozwa na CCM imeshindwa kuwahudumia wananchi.
  Walisema kuwa kila kukicha maisha ya Watanzania yanazidi kuwa magumu kutokana na serikali kushindwa kudhibiti mfumko wa bei za bidhaa muhimu na hivyo kuwafanya waishi kwa umaskini mkubwa.
  Opulukwa katika mikutano hiyo, aliwaambia wananchi kuwa serikali hii inayoongozwa na CCM imesababisha hali ngumu ya maisha kwa wananchi hasa wa kipato cha chini ambao ndiyo wengi.
  Aliendelea kueleza kuwa licha ya wabunge wa vyama vya upinzani kupiga kelele bungeni juu ya suala hilo lakini hakuna hatua zozote zinazochukuliwa kutokana na serikali kutowajali.
  Naye Kasulumbayi aliwataka wananchi kufanya maamuzi magumu ya mabadiliko kwa kuiondosha serikali ya CCM madarakani katika sanduku la kura katika uchaguzi mkuu ujao wa mwaka 2015 kwa kujiunga na CHADEMA ambacho kimejipambanua wazi katika kuwaletea maendeleo kwa kupinga vitendo vya kifisadi vinavyofanywa na viongozi wa serikali.
  Iringa wabeza Baraza la Mawaziri
  Kwa mara nyingine tena, CHADEMA mkoani hapa kimekosoa mabadiliko ya baraza jipya la mawaziri kwa kudai kuwa sio suluhisho la matatizo ya Watanzania.
  Wakihutubia mkutano mkubwa wa hadhara uliofanyika Mkoa mpya wa Njombe, wabunge Peter Msigwa wa Iringa Mjini, Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi na wa Mbozi Magharibi David Silinde walisema kinachotakiwa ni kubadilisha mfumo mzima na wale wote ambao wametajwa kwamba ni wezi wa mali za umma waende jela na wafilisiwe na si kuachwa bure.
  Msigwa alisema kumbadilisha waziri kutoka nafasi moja kwenda nyingine hakusaidii kutatua ubadhirifu wa mali ya umma.
  Alisema ndiyo maana wanawataka wananchi wa Nyanda za Juu Kusini na Watanzania kujitokeza kwa wingi kutoa maoni ya Katiba mpya kwani ndiyo njia pekee ya kuubadilisha mfumo aliodai ni kandamizi wa serikali ya Chama cha Mapinduzi.
  Kwa upande wake Joseph Haule amesema watafanya kila jitihada kuhakikisha wale walioshutumiwa wote wanawajibishwa kwa kufikishwa katika mikono ya sheria ili iwe mfano kwa mawaziri wengine waliochaguliwa.
  “Kuwaweka pembeni mawaziri walioshutumiwa kwa kujenga majumba na uchafu wowote walioufanya haitoshi, hiyo ni sawa na kuwaambia haya sasa mko huru hamna mtu wa kuwahoji wala kuwaangalia nendeni mkatafune fedha mlizochukua.
  “Hilo halitakubalika, tutakomaa mpaka tuhakikisha wale walioshutumiwa wanafikishwa kwenye mikono ya sheria na wachukuliwe hatua kali za kisheria ili iwe mfano kwa mawaziri wengine walichaguliwa,” alisema Mbilinyi.
  Wakati huohuo CHADEMA imeahidi kufuatilia majengo mbalimbali yanayoaminika kumilikiwa na viongozi wa juu akiwemo Rais Jakaya Kikwete na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, ili kujua vyanzo gani vya fedha vilivyowawezesha kujenga na kununua majengo yenye gharama kubwa namna hiyo.


  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 2. stephot

  stephot JF-Expert Member

  #2
  May 8, 2012
  Joined: Mar 1, 2012
  Messages: 5,034
  Likes Received: 2,648
  Trophy Points: 280
  Kazi ipo!
   
 3. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #3
  May 8, 2012
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,219
  Likes Received: 84
  Trophy Points: 145
  Ngoja Nape asikie
   
 4. TUKUTUKU

  TUKUTUKU JF-Expert Member

  #4
  May 8, 2012
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 11,852
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Safi sana CDM!songa mbele!
   
 5. a

  abdulahsaf JF-Expert Member

  #5
  May 8, 2012
  Joined: Aug 31, 2010
  Messages: 859
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Baada ya wimbi wa la afus na bahi ya viongozi kukihama chama cha ccm , hivi sasa kumezuka mtindo wa makamishna wa polisi kuwahujumu viongozi wa Chadema kwa kuwabambikizia kesi na kukisizi kwa vitendo vya mauwaji huku polisi wakiwa kama hawapo nchini au hayawahusu hayo.

  hii yote ni mpinu chafu ya chama tawala kuingiwa na hofu kubwa ya kuona siku hadi siku chama chao kina meguka na kukimbiwa na makundi ya wafuasi wao na kuwa na mpasuko mkumbwa ndani ya chama.

  Wengi wa vigogo wa ccm wamesha shtushwa na kuona 2015 huenda ikawa ccm ndio end of the road, mazambi ya ccm yamesha kuwa mengi na duwa za Watanzania zimeshaonyesha kukubaliwa na Mungu , na ndio hivi sasa ccm inaanza kupata tabu na kusaka mchawi wake huku chama kikiwa na mpasuko wa vigae.

  Hakuna shaka kuwa mizimi yao wenyewe ccm ndio inayo watesa na sio Chadema. mazambi ya ccm yamekuwa mengi na viongozi wasio watakatifu mbele ya Watanzania.
   
 6. Manyanza

  Manyanza JF-Expert Member

  #6
  May 8, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,446
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Hapo kwenye red ni Prof J yule mwanamuziki au makosa yakiuandishi?
   
 7. Fredrick Sanga

  Fredrick Sanga JF-Expert Member

  #7
  May 8, 2012
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 3,148
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Morogoro kumetokea nini? Mbona umeitaja tu.
   
 8. Papizo

  Papizo JF-Expert Member

  #8
  May 8, 2012
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 4,611
  Likes Received: 392
  Trophy Points: 180
  Hawa CCM by 2015 najuwa watatafuta njia ya kutokea tu lazima lazima
   
 9. kibogo

  kibogo JF-Expert Member

  #9
  May 8, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 9,481
  Likes Received: 790
  Trophy Points: 280
  PeoooooooPleeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeezzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzz
   
 10. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #10
  May 8, 2012
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  WATANZANIA TUMESHAAMUA KWAMBA CCM PAMOJA NA MAFISADI WAKE SASA BAI BAI!!!

  ... WaTanzania walalahoi tunaodhalilika kila siku kwa matokeo ya UFISADI huko serikali ya CCM sasa TUMEASHAAMUA kwamba ukombozi wa nchi hii utaletwa na sisi wenyewe tunaonyanyasika; je sasa ni nani tena wa kutuzuia?

  Utaifa mbeeeeeele kama tai huku tukiwafurumshia mbali MAFISADI wa CCM kwa kujiunga CHADEMA kila kichwa katika kila kijiji hapa nchini!!!!

  Na kwa kuwa mabadiliko ya kweli siku zote huaanza na mtu mmoja mmoja na kuenea zaidi, hebu sasa chukua HATUA tangu muda huu na kuelimisha wengine 10 kila wiki kufunguka macho na akili kupanda MV safina kabla lango halijafungwa.
   
 11. MD25

  MD25 JF-Expert Member

  #11
  May 8, 2012
  Joined: Jan 28, 2012
  Messages: 3,078
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  M4C in action, sasa kina Rejao na Mama Porojo, Je, hao pia ni wa-Kaskazini?
   
 12. Mlitika

  Mlitika JF-Expert Member

  #12
  May 8, 2012
  Joined: Mar 23, 2012
  Messages: 458
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Reading this really warms my heart; Tehe tehe tehe teheee!
  Yes indeed, tehe tehe tehe teheee!
   
 13. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #13
  May 8, 2012
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  KASI YA MABADILIKO NCHINI NA DHARAU ZILIZOWAPONZA MAFISADI HUKO CCM:

  Tulipoanza walitubeza (vyama vya uchaguzi / msimu) na sasa wanapozama wanatukaba (mauaji ya kutishia umma)!!

  Ukombo mbeeeeeeeeeeeele kama tai; ewe mama ewe baba nawe kijana hapo,
  Vua gamba leo hii hii na uvae gwanda la ukombozi ili taifa letu lipate tena hueni kuondokana na MAFISADI WA huko ndani ya CCM.
   
 14. B

  Bweru JF-Expert Member

  #14
  May 8, 2012
  Joined: Nov 3, 2011
  Messages: 213
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Kweli muda wa ukombozi umefika. Kila Mtanzania anapaswa kujizatiti katika kuondokana na mafisadi walioizamisha nchi yetu tukufu katika lindi la umasikini wa kutupwa. Nchi ni tajiri lakini wananchi wake hawajiwezi kabisa. Kuanzia sasa msemo wetu ni Chagua Chadema, Chagua Mabadiliko. Nchi bila Ufisadi inawezekana. CCM (Chama cha Mafisadi) bye!!!
   
 15. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #15
  May 8, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,202
  Likes Received: 1,978
  Trophy Points: 280
  Rejao anasema CCM wapo period!!!
   
 16. b

  baraka moze Member

  #16
  May 8, 2012
  Joined: Apr 21, 2012
  Messages: 99
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  na bado
   
Loading...