CHADEMA yailiza tena CCM Arusha | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CHADEMA yailiza tena CCM Arusha

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by palalisote, Jun 4, 2012.

 1. palalisote

  palalisote JF-Expert Member

  #1
  Jun 4, 2012
  Joined: Aug 4, 2010
  Messages: 8,352
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 0
  CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimekiliza tena Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa kuibomoa tena ngome yake baada ya kuwachomoa wanachama takriban 400, akiwamo Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana (UVCCM) Kata ya Enduleni, Cosmas Lakani.  Lakani ambaye ni mmoja wa viongozi machachari na aliyekuwa tegemeo kubwa la umoja huo katika Wilaya ya Ngorongoro, alihama na wanachama 394 kutoka kata za Ngorongoro na Enduleni juzi na kufanya idadi ya Wana CCM waliojiunga na CHADEMA ndani ya miezi miwili kufikia 3,481.

  "CCM imetunyonya mpaka mwisho, walisema tuache kilimo cha kujikimu watatupa chakula, lakini wanatupa chakula kidogo, wanaona mnyama anathamani kubwa kuliko sisi tunaoishi Ngorongoro. Ndiyo maana tunawaacha na CCM yao tumekuja CHADEMA itusaidie tukadai haki yetu," alisema Ndaito Sabore.  Kada mwingine apasua vichwa viongozi wake huko Moshi, viongozi wa CCM wa Wilaya ya Moshi Vijijini, wanaumiza vichwa kujaribu kumzuia kwa kila mbinu kada wake maarufu, Ansi Mmasi, anayetajwa kuwa katika harakati za kukihama chama hicho na kujiunga na CHADEMA.

  Mmasi ambaye amekuwa mpinzani mkubwa wa mbunge wa sasa wa Jimbo la Moshi Vijijini, Dk. Cyril Chami, anatajwa kuwa miongoni mwa vigogo wa CCM ambao wanatazamiwa kukihama chama hicho, ili kuwania nafasi hiyo katika uchaguzi mkuu ujao mwaka 2015.

  Hata hivyo, Mwenyekiti wa CCM wa Wilaya ya Moshi Vijijini, Gabriel Masenga, alidai kuwa hajapata taarifa rasmi kutoka kwa Mmasi kama anataka kuhama, lakini akakiri kusikia fununu hizo kupitia vyombo vya habari.


  Habari zaidi soma "CHADEMA yailiza tena CCM Arusha"
   
 2. M

  Molemo JF-Expert Member

  #2
  Jun 5, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimekiliza tena Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa kuibomoa tena ngome yake baada ya kuwachomoa wanachama takriban 400, akiwamo Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana (UVCCM) Kata ya Enduleni, Cosmas Lakani.

  Lakani ambaye ni mmoja wa viongozi machachari na aliyekuwa tegemeo kubwa la umoja huo katika Wilaya ya Ngorongoro, alihama na wanachama 394 kutoka kata za Ngorongoro na Enduleni juzi na kufanya idadi ya Wana CCM waliojiunga na CHADEMA ndani ya miezi miwili kufikia 3,481.

  Wanachama hao walihamia CHADEMA wakati wa mikutano ya hadhara iliyoongozwa na viongozi wa CHADEMA Mkoa wa Arusha, akiwamo Mwenyekiti, Samson Mwigamba, kwenye kata hizo.

  Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa kadi ya CHADEMA, Lakani alisema kuwa amechukua hatua hiyo kwa vile serikali ya CCM imeshindwa kutatua kero za wananchi, na kibaya zaidi kuonekana kuwa wanathamini wanyama walioko katika mbuga kuliko watu.

  Alizidi kuishambulia serikali akidai imeshindwa kuwapatia hospitali, ambapo kwa kipindi chote wamekuwa wakitegemea ile inayomilikiwa na Kanisa Katoliki, na kuhoji kama kanisa hilo lisingejitolea wao wangepata wapi huduma za afya.
  Alidai kuwa amekuwa akizuiwa na uongozi wa juu kusema lolote kuhusiana na kero za wananchi, huku akitakiwa kufumba mdomo wake.

  Baadhi ya wanachama hao walidai mbele ya viongozi wa CHADEMA Mkoa wa Arusha kuwa serikali imeshindwa kuwasaidia hata kupata chakula cha kutosha familia zao kama walivyowaahidi wakati wakiwazuia kuendesha kilimo cha kujikimu ndani ya eneo la Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA.

  "CCM imetunyonya mpaka mwisho, walisema tuache kilimo cha kujikimu watatupa chakula, lakini wanatupa chakula kidogo, wanaona mnyama anathamani kubwa kuliko sisi tunaoishi Ngorongoro. Ndiyo maana tunawaacha na CCM yao tumekuja CHADEMA itusaidie tukadai haki yetu," alisema Ndaito Sabore.

  Mwana CCM mwingine mpya wa CHADEMA, Shuraa Sungai, alisema kuwa CCM iliwadanganya kuwa itatoa ajira kwa vijana lakini inasikitisha mpaka sasa vijana wao wanahitimu kidato cha nne na wengine vyuo vikuu lakini wanarudi kijijini hapo baada ya kukosa kazi.

  Mwenyeki wa CHADEMA wa mkoa, Mwigamba, aliwaeleza wananchi hao kuwa CCM haijawahi kuwa na sera ya kuwasaidia wafugaji, jambo alilosema limechangia kuibuka kwa mapigano kati ya wafugaji na wakulima mara kwa mara.

  Naye mratibu wa Baraza la Wanawake Mkoa wa Arusha, Cecilian Ndossi na Ephata Nanyaro, walisema maisha ya wananchi hao yanasikitisha kwa vile wanaishi katika umaskini wa kupindukia wakati wilaya yao ikiliingizia taifa mamilioni ya fedha za kigeni kupitia utalii unaofanyika ndani ya Hifadhi ya Ngorongoro.

  "Serikali ya CCM inaonesha ni kiasi gani inathamini wanyama kuliko wananchi wake, hata ukiangalia barabara zinazotumika kwa ajili ya utalii zimetengenezwa vizuri lakini hizi zinazokuja huku kwa wananchi ni mbovu na zinapitika kwa shida sana," alisema Nanyaro.

  "Mimi niko kwenye sekta ya utalii, Ngorongoro inaliingizia taifa mamilioni ya dola, Serikali ya CCM inaacha kuwaletea huduma muhimu kama hospitali, maji safi na barabara kwa sababu inajua nyie ni wateja wao, wakataeni mje CHADEMA tushirikiane kudai haki hiyo mpaka kieleweke," alisema Ndossi.


  Source:Tanzania Daima
   
 3. Technician

  Technician JF-Expert Member

  #3
  Jun 5, 2012
  Joined: Mar 30, 2010
  Messages: 843
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Hizi ndo habari zinazonifanya napata afya njema.
  Bravo CDM
  Bravo Dr Slaa
  Bravo Mbowe
   
 4. POMPO

  POMPO JF-Expert Member

  #4
  Jun 5, 2012
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 6,694
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Maumivu ya kichwa huanza pole polee...
   
 5. mmbangifingi

  mmbangifingi JF-Expert Member

  #5
  Jun 5, 2012
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 2,855
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Ni "oil chafu" huyo! teh!teh!
   
 6. BASHADA

  BASHADA JF-Expert Member

  #6
  Jun 5, 2012
  Joined: Jul 13, 2011
  Messages: 487
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Duh, hii nimeipenda. Kumbe arusha mkutano unaoongozwa na viongozi wa chama wa mkoa unavuna watu mia nne. Akija Dr Slaa si anamaliza mkoa wote
   
 7. t

  thatha JF-Expert Member

  #7
  Jun 5, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  amejivua gamba huyo.
   
 8. Lekanjobe Kubinika

  Lekanjobe Kubinika JF-Expert Member

  #8
  Jun 5, 2012
  Joined: Dec 6, 2006
  Messages: 3,067
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Unaona? Na kavaa gwanda. Kazi ndio inaanza sasa. Sikilizia muziki utamu weeee! Nauona utamu weeeee!
   
 9. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #9
  Jun 5, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,196
  Likes Received: 1,977
  Trophy Points: 280
  Wakati Chama kubwa (CDM) linavuna wanachama huko Ngorongoro Baba Mwanaasha anatembea kwenye vichochoro vya Arusha akijidai anafanya mazoezi kumbe anavizia videmu
   
 10. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #10
  Jun 5, 2012
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  umefanya siku yangu kuwa njema nimeipenda hii sana
   
 11. Maishamapya

  Maishamapya JF-Expert Member

  #11
  Jun 5, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 1,280
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Maumivu yalishaanza siku nyingi ... wametumia kila pain killer haijawafaa. Sasa hivi wanahitaji: "Maumivu yakizidi - Vua Gamba, Vaa Gwanda"
   
 12. mansakankanmusa

  mansakankanmusa JF-Expert Member

  #12
  Jun 5, 2012
  Joined: Sep 30, 2010
  Messages: 4,084
  Likes Received: 601
  Trophy Points: 280
  ni vizur kuhama kabla ya 2015
   
 13. samstevie

  samstevie JF-Expert Member

  #13
  Jun 5, 2012
  Joined: Nov 11, 2011
  Messages: 202
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nadhani kule hakuna haja na viongozi wa kitaifa watu wameshaelimika vya kutosha kilio changu mimi ni Dar hasa Temeke District tuwabambe hawa wazaramo kwa kweli wanahitaji ukombozi.
   
 14. hashycool

  hashycool JF-Expert Member

  #14
  Jun 5, 2012
  Joined: Oct 2, 2010
  Messages: 5,899
  Likes Received: 442
  Trophy Points: 180
  CCM mkinuna hatutawauliza sababu!
   
 15. IKHOIKHOI

  IKHOIKHOI JF-Expert Member

  #15
  Jun 5, 2012
  Joined: Jan 30, 2012
  Messages: 366
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Mimi jamani taarifa kama hizi zinanipa burudaaaaaaaaaaaaani kama vile nakamata tasker baridi
   
 16. M

  Mthuya JF-Expert Member

  #16
  Jun 5, 2012
  Joined: Jun 9, 2011
  Messages: 1,415
  Likes Received: 65
  Trophy Points: 145
  Msaragambo uendelee kijiji kwa kijiji ,nyumba kwa nyumba na mtu na mtu mpaka tukamate nchi
   
 17. IKHOIKHOI

  IKHOIKHOI JF-Expert Member

  #17
  Jun 5, 2012
  Joined: Jan 30, 2012
  Messages: 366
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Eebwanaaaeeeh!! Hizo kwa kweli ni news ninazopenda kuzisikia. Huwa zinaniongezea kilo.
   
 18. kuku dume

  kuku dume JF-Expert Member

  #18
  Jun 5, 2012
  Joined: Apr 22, 2012
  Messages: 415
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  CDM forever.
   
 19. O

  Otorong'ong'o JF-Expert Member

  #19
  Jun 5, 2012
  Joined: Aug 17, 2011
  Messages: 31,077
  Likes Received: 10,435
  Trophy Points: 280
  Kuna habari nyingine auhitaji hata chakula zenyewe ni chakula tosha.
   
 20. Omonto wa-hene

  Omonto wa-hene Senior Member

  #20
  Jun 5, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 179
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  M4C itakuja lini huku Serengeti nauliza tena? Jimbo hili litaachwaje kukaa wazi miaka yote mitano?
   
Loading...