CHADEMA yaijibu JWTZ

CHADEMA yaijibu JWTZ

Mwanaukweli

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2007
Posts
4,789
Reaction score
1,732
mnyika+ubungo.jpg

MBUNGE wa Ubungo na Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa Chadema, John Mnyika

SIKU moja baada ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), kutangaza kumsaka mtu aliyepiga picha na Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema akiwa amevalia sare za jeshi hilo, chama hicho kimeibuka na kulijia juu jeshi hilo.

Hata hivyo, mbali na kauli hiyo, jeshi hilo limekijibu Chadema likisema kwamba halifanyi siasa na kwamba litaendelea kumsaka mtu huyo, kwa kuwa kanuni zake haziruhusu askari kushabikia siasa.

Jana, Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa Chadema, John Mnyika alisema chama hicho kimeshangazwa na kasi ya jeshi hilo kuchunguza tukio hilo, huku akidai kwamba kuna masuala mazito ambayo hayajatolewa ufafanuzi kama lile la Meremeta.

"Serikali ilikataa kulifuatilia kwa madai ya kutokuingilia usiri wa jeshi hilo na halikutolewa ufafanuzi wala kufanyiwa uchunguzi mpaka sasa," alisema Mnyika na kuendelea.

"Isitoshe Septemba, mwaka huu katika Mkutano Mkuu wa UVCCM Iramba, aliyekuwa Mweka Hazina wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), ambaye kwa sasa ni Naibu Katibu Mkuu Bara wa chama hicho Mwigulu Nchemba (aliwahi kutoa matamko kuhusu JWTZ), lakini jeshi halikufikiria kuyatolea tamko."

Mnyika alidai pia kuwa wakati wa Kampeni za Uchaguzi Mkuu mwaka 2010, aliyekuwa Mnadhimu wa Jeshi hilo Luteni Jenerali Abdulahman Shimbo aliitisha mkutano na waandishi wa habari na kuvitaka vyama vya siasa kutokugomea matokeo ya uchaguzi kwa madai ya kulinda amani ya nchi.

"Kauli ile ya Shimbo ni ya kisiasa na ya kibaguzi ambayo ililenga kuvididimiza vyama vingine na kuibeba CCM. Mbona jeshi halichunguzi kauli hiyo hata baada ya Shimbo kustaafu?" alihoji Mnyika.

Mnyika alisema kwamba Chadema hakitaki kutumia tukio hilo la askari kuhalalisha makosa mengine, bali inataka sasa JWTZ iwajibike kwa kila jambo linalolihusu badala ya kukimbilia masuala yaliyofanywa na askari wadogo. Hata hivyo, Mnyika alisema chama hicho hakipo tayari kuingia katika mvutano na jeshi kuhusiana na tukio la askari huyo kujihusisha na siasa mpaka jeshi hilo litakapokamilisha uchunguzi na kutoa taarifa yake kwa umma.

Kwa upande wake, Msemaji wa JWTZ, Kanali Kapambala Mgawe alisema kuwa jeshi litaendelea kujiweka kando na shughuli za siasa na kusisitiza kuwa mtumishi wake yeyote anayetaka kujiingiza kwenye majukwaa ya kisasa anapaswa kujitoa jeshini. Akijibu hoja za Chadema kuhusiana na tamko lilitolewa na aliyekuwa Mnadhimu wa jeshi hilo Shimbo aliyewataka wanasiasa kutogomea matokeo wakati wa Uchaguzi Mkuu uliopita, Mgawe alisema: "Ebwa ehh! Na wewe sasa unataka kuniingiza kwenye siasa, mimi sitaki kuingia huko, lakini nikueleze kuwa sisi kama wanajeshi tuko royal (utii) kwa Serikali iliyoko madarakani," alisema Mgawe.

Alisema kwa mujibu wa sheria, Jeshi halipaswi kufungamana na itikadi zozote za kisiasa kwani kwa kufanya hivyo kunaweza kulitumbukiza taifa kwenye hatari. "Leo huyu anaingia kwenye mkutano wa chama na sare za jeshi, kesho atakuja mwingine na silaha, huoni kwamba sasa tutakuwa tunakaribisha hatari ?" alihoji Mgawe.

Source: Mwananchi
 
Chonde chonde Mnyika siasa na Jeshi sio sahihi, CHADEMA kiangalie namna ya kuwa na mahusiano bora na jeshi, huyo mwanajeshi mmoja sio issue
 
CHADEMA wako sahihi, JWTZ ni chombo cha wananchi na wala si chombo cha CCM hivyo kama vipi wale wakuu wa mikoa na wilaya na wengine wanaotumikia vyeo vya u-kada katika CCM wachukuliwe hatua haraka kabla hatujamtazama mwanajeshi wa Mh Lema Jijini Arusha hivi majuzi.

Ni wakati mwafaka jeshi letu pendwa likajikwamua na U-CCM wa enzi za chama kimoja katika kipindi hiki cha vyama vingi ili chombo hiki muhimu kiweze kuendana na wakati wa hivi sasa.

Roho ikipenda kitu wala hakuna haja kuewndelea kujificha; ukweli wa mambo ni kwamba zaidi ya asilimia 80 ya jeshi letu linapenda chama kile ambacho wananchi tulio wengi tunakipenda - CHADEMA!!!!!
 
Hujui unachoakiongea!!!
Jifunze tofauti kati ya mwanajeshi na mwanajeshi mstaafu. Pia jifunze kuongea mambo kwa evidence...
 
Chonde chonde CCM,

siasa za kuwahonga baadhi tu ya wanajeshi wateule vyeo vya kichama na siasa si sahihi hivyo ni wakati mwafaka mkaiacha JWTZ kweli kikawa ni Jeshi la Wananchi na wala si Jeshi la chama kimoja tu nchini Tanzania.

JWTZ ni chetu sote na tunakihudumia kwa kodi zetu bila itikadi hivyo na wao kudhihirisha upenzi wao wa siasa bila mipaka ya ki-CCM ni jambo lililochelewa sana wakati wake.

Chonde chonde Mnyika siasa na Jeshi sio sahihi, CHADEMA kiangalie namna ya kuwa na mahusiano bora na jeshi, huyo mwanajeshi mmoja sio issue
 
CHADEMA wako sahihi, JWTZ ni chombo cha wananchi na wala si chombo cha CCM hivyo kama vipi wale wakuu wa mikoa na wilaya na wengine wanaotumikia vyeo vya u-kada katika CCM wachukuliwe hatua haraka kabla hatujamtazama mwanajeshi wa Mh Lema Jijini Arusha hivi majuzi.

Ni wakati mwafaka jeshi letu pendwa likajikwamua na U-CCM wa enzi za chama kimoja katika kipindi hiki cha vyama vingi ili chombo hiki muhimu kiweze kuendana na wakati wa hivi sasa.

Roho ikipenda kitu wala hakuna haja kuewndelea kujificha; ukweli wa mambo ni kwamba zaidi ya asilimia 80 ya jeshi letu linapenda chama kile ambacho wananchi tulio wengi tunakipenda - CHADEMA!!!!!

Nakuona mkuu unahoja tena nzito wakitoka jeshini wanahamia ukada wa ccm mikowa na wilaya, je huko ndo kutenganisha Jeshi

na siasa? watawala watuweke sawa hapa.
 
lakini alichokisema Mnyika ni kweli bana jeshi letu linatumika vibaya, tena limekuwa kichaka cha wanasiasa kufichia maovu yao... hivi yule police aliyegombea EC ya CCM alikuwa amestafu kazi au bado anapiga gwaride kama kawa na hakuna wa kufatilia kwa kuwa ni chama dola
 
Hujui unachoakiongea!!!
Jifunze tofauti kati ya mwanajeshi na mwanajeshi mstaafu. Pia jifunze kuongea mambo kwa evidence...

Mkuu zeMaracopolo

Ukiona mwenzio kapewa ukuu wa mkowa nawewe ndo umekalia kiti chake baada ya yeye kustaaafu na kuwa kada, je

hutashawishika kutetea maslahi ya chama ili nawewe ujepewa ukuu wa mkoa hapo baadaye? imekaaje hii!!
 
Hahahaaaaa! wakati wa uchaguzi ni chama gani kinakuwa kimeshikilia serikali?
na jeshi linapaswa kulinda maslahi ya chama au nchi?
kwani kama vyama vimetofautiana juu ya matokea ya uchaguzi nini jukumu la Jeshi?

nafikiri Jeshi linapaswa kulinda usalama wa nchi mpaka suluhu ya nani mshindi wa halali ipatikane!

CCM pengine ni nafasi nyingine ya kumvua Kamanda Lema ubunge kwa kulitumia jeshi vibaya, hahahaa, wanasubiri nini??

NB. Mioyo ya watanzania imevunjwa vya kutosha na magamba sasa tunasema basi..tunataka mioyo yetu ipone 2015!

[
Mgawe alisema: "Ebwa ehh! Na wewe sasa unataka kuniingiza kwenye siasa, mimi sitaki kuingia huko, lakini nikueleze kuwa sisi kama wanajeshi tuko royal (utii) kwa Serikali iliyoko madarakani," alisema Mgawe.]
 
Binafsi napenda maeshimiano ya pande mbilzi zote yawepo kati ya JWTZ ambalo ni Jeshi la Watanzania na ki ukweli kila Mtanzania hata asiye na elimu ya Dalasa la saba anajua heshima lililojijengea Jeshi letu hilo kwa Watanzania.Lakini kwa tukio la Askari wao huyo wengine tumesema Jeshi lienda kistaarabu na CDM nao waende kistaarabu.Jeshi letu linanguvu ya Umma ambayo ni lasmi, bila kuzingatia Itikadi ya chama chochote,lakni CDM nao ni chama ambacho kinatafuta kuungwa mkono na jamii ili kiweze kupewa Serikali ambayo italisimamia Jeshi ilo ilo katika kazi zake za kila siku uende kikipewa dhamana hiyo kupitia sanduku la kura.

Heshima pande zote mbili,na kudeal na issue nzima in a fair way na sio ushabiki,italeta mwafaka mzuri na kuondoa kuwekeana kinyongo kwa baadhi yawatendaji wa Jeshi na Uongozi wa Kitaifa na wanachama na wapenzi wa CDM.
 
Hivi mnyika ameishia darasa la ngapi hasa kielimu?shimbo alivitaka vyama vya siasa visigomee matokeo yatalapotangazwa akimaanisha vyama vyote ikiwemo ccm,sasa mnyika alijuaje kwamba ccm ndio watashinda hivyo ushauri wa jeshi unakilenga chadema na cuf tu?halafu mkiambiwa mna miliki kadi mbili mbili mnatoa povu,unaingia kwenye uchaguzi ukijua unaenda kushindwa si bora usishiriki basi
 
Hujui unachoakiongea!!!
Jifunze tofauti kati ya mwanajeshi na mwanajeshi mstaafu. Pia jifunze kuongea mambo kwa evidence...

Hujui ya kuwa mwanajeshi akistaafu bado ni mwanajeshi,pakitokea tatizo lolote huitwa kikosi.Kwa nini usitwe wewe!
 
Hivi mnyika ameishia darasa la ngapi hasa kielimu?shimbo alivitaka vyama vya siasa visigomee matokeo yatalapotangazwa akimaanisha vyama vyote ikiwemo ccm,sasa mnyika alijuaje kwamba ccm ndio watashinda hivyo ushauri wa jeshi unakilenga chadema na cuf tu?halafu mkiambiwa mna miliki kadi mbili mbili mnatoa povu,unaingia kwenye uchaguzi ukijua unaenda kushindwa si bora usishiriki basi
Elimu ya Mnyika haina mashaka. Form 4 alipata point 7 akiwa na A 9 (Nafasi ya kwanza Tanzania), Form VI pia alipata point Tatu, kisha amesoma Shahada ya sheria UDSM.

No doubt about his ability and his capacity to reason.
 
Una uhakika na ulichokiandika hapo? Point tatu form six? Hamuogopi hata kudanganya?

Mnyika ana uwezo na ayafanyayo hata kama elimu yake sio kubwa. Ila hakuna haja ya kudanganya kuweka elimu au matokeo ambayo hana.
 
hayo ni matokeo yake halisi wala hakuna nyongeza ya uongo.
 
Kimsingi Mnyika kakubali kosa, ila katumia siasa za lawyerly obfuscation and diverting attention.

Nakubali JWTZ linaweza kuwa na makosa mengi, lakini ukiamua kuacha mambo mengine yote na ku focus kwenye hili la mwanajeshi katuni kutumika kisiasa katika rally ya CHADEMA Mnyika kakubali kosa, in not so many words.
 
Hawa wajeda waache double standards,masuala mengi mazito yanatamkwa yakihusisha wao lakini wamekuwa kimya kuyatolea ufafanuzi.Mfano ni suala la meremeta n.k.Tunajua sana wanatumika kama kichaka cha mafisadi na wamekuwa mstari wa mbele kuwalinda mafisadi. Kwa kifupi ni kwamba wanatumiwa sana kuhujumu rasilimali za nchi hii.

Wanao faidika zaidi ni hao wa vyeo vya juu sababu wanajua fika kwamba kikiingia chama kingine madarakani nafasi zao za ulaji zitakuwa matatani. Sote tunakumbuka Shimbo 2010 alivyo kimbilia kwenye vyombo vya habari akitaka vyama vikubali matokeo na jeshi haliku sema chochote juu ya hili. Sasa kama anavyo sema Mnyika kuna mambo mengi wanayo husishwa nayo na hawaja yatolea ufafanuzi wana kimbilia Jambo dogo la askari kupiga picha tu!

Majuzi Mwigulu Nchemba amesema jeshi litalinda magamba mpaka kufa mbona hawaja mkanya wala kutoa matamko?

Kimsingi wanao faidika na ufisadi ni hao wa vyeo vya juu na siyo wadogo kama aliye piga picha na Lema. Hawa jamaa wakiona jambo litakalo hatarisha ulaji wao wanalishupalia. Matamko wanayotoa hayana hata chembe ya uzalendo bali ni hofu tu ya maswahiba wenzao katika ufujaji wa rasilimali za nchi kung'oka.

Waonapo mjeda wa cheo cha chini hawi upande wao wanakuwa na hofu make hawa ndiyo wapiganaji halisi mstari wa mbele. Kuhitimisha napenda kusema "GO MJEDA GO AND DON'T BE SCARED FOR 2ND LIBERATION"
 
Hivi mnyika ameishia darasa la ngapi hasa kielimu?shimbo alivitaka vyama vya siasa visigomee matokeo yatalapotangazwa akimaanisha vyama vyote ikiwemo ccm,sasa mnyika alijuaje kwamba ccm ndio watashinda hivyo ushauri wa jeshi unakilenga chadema na cuf tu?halafu mkiambiwa mna miliki kadi mbili mbili mnatoa povu,unaingia kwenye uchaguzi ukijua unaenda kushindwa si bora usishiriki basi

wewe umeishia darasa la ngapi? Kama huwezi kuona kuwa tamshi la Shimbo lililenga Chadema, nina wasiwasi pia na uelewa wako
 
Mkuu zeMaracopolo

Ukiona mwenzio kapewa ukuu wa mkowa nawewe ndo umekalia kiti chake baada ya yeye kustaaafu na kuwa kada, je

hutashawishika kutetea maslahi ya chama ili nawewe ujepewa ukuu wa mkoa hapo baadaye? imekaaje hii!!

Unachosema kinaweza kuwa na ukweli lakini hakihusu jeshi pekee. Hata hivyo wanjeshi hawakatazwi kupenda vyama, wanachokatazwa ni kuonyesha ushabiki wao hadharani hasahasa wakiwa wamevaa uniform.
Vile vile ikumbukwe kuwa jeshi lilikuwa na uhusiano wa karibu sana na CCM mpaka mwaka 1992. Ikumbukwe kuwa hata JKT ilianzishwa kwa mawazo ya TANU youth league katika mkutano wao kule Tabora. Kwahiyo ni kweli kuwa jeshi bado lina chembechembe za CCM lakini haimaanishi kuwa sasa wanajeshi wavae sare za CCM na kwenda kuishabikia. Ukitaka kufanya majaribio ingia na gari yenye picha za kushabikia CCM katika eneo rasmi la jeshi kama Lugalo utaona kitakachotokea. Hata watumishi raia jeshini hawaruhusiwi kuvaa fulana za vyama katika maeneo ya yao ya kazi jeshini. na hili linahusu watumishi wote wa umma...
 
Back
Top Bottom