CHADEMA yaicharaza CCM Bumbuli, Tanga

CHADEMA yaicharaza CCM Bumbuli, Tanga

Tumaini Makene

JF-Expert Member
Joined
Jan 6, 2012
Posts
2,650
Reaction score
6,085
BAADA ya hila na mbinu haramu kadhaa kuzuia uchaguzi huru na haki, kuminya demokrasia ya sanduku la kura kuchukua mkondo wake, ikiwemo Mtendaji wa Kijiji cha Kwekitui kuharibu uchaguzi kwa kukimbia na sanduku la kura wiki iliyopita, CHADEMA imeibuka mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti wa kijiji hicho, kilichoko Jimbo la Bumbuli, wilayani Lushoto, Mkoa wa Tanga, kwa kura 196 dhidi ya CCM waliopata kura kura 189.

Uchaguzi huo wa marudio ulifanyika leo, Jumapili, Aprili 7, 2013.

Hongera za kipekee ziwafikie makamanda wa kijijini hapo, Jimbo la Bumbuli, Wilaya ya Lushoto, Mkoa wa Tanga, chini ya usimamizi wa Kanda ya Kaskazini. Ndiyo waliopigana na kupiganisha 'vita' hiyo.

Kanda ya Kaskazini kwa kweli inaendelea ku-take off vizuri ambapo uchaguzi wa marudio wa vijini na vitongoji huko Lushoto umekuwa na moja ya majaribio na wameonesha uwezo na mfano wa namna decentralization inavyoweza kufanya kazi nzuri kabisa, bila kusubiri Makao Makuu hata kwa vitu ambavyo vingeweza kufanywa na vipaji vingi vilivyoko ngazi za chini ambavyo CHADEMA ilikuwa haijawahi kuvitumia kwa kiwango kikubwa.

We hopefully look forward kwa kanda zingine kuja kwa kasi zaidi. Ushindani huleta ufanisi. Hili ni moja ya jambo la msingi sana katika dhana hii.

Ufanisi huu, hautakuwa kwenye kushinda uchaguzi pekee. Tutarajie kuona mengi to keep the fire burning.
 
Mkuu ni mbumbuli au bumbuli kwa januari makamba???
 
Sikutegemea CDM kushinda sehemu hizo .... Nilijua tu kuwa Makamba ni blah blaher!
 
Safi sana. Wembe ni huo huo katika chaguzi zote zilizo bakia!
 
Ya kinafki lakini imefika

Ndio tatizo lenu. Mkipongezwa kosa, msipopongezwa kosa. Lami ikijengwa kosa, isipojengwa kosa. Mshahara ukiongezwa kosa, usipoongezwa kosa. Washutumiwa wakikamatwa kosa wasipokamatwa kosa. Rais akiongea kosa, asipoongea kosa.

Ili mradi tu mlalamike...

Lakini watu kama nyinyi kwenye jamii hamkosekani, TUMESHAWAZOEA...
 
ccm unaumwa kuhara halafu wanalazimisha kucheka, mafuriko huwezi kuyazuia kwa kiganja.
 
Huko si ndo kwa mh. J.makamba naibu waziri wa sayansi na tekinolojia?
 
Nawapongeza CHADEMA ushindi huu unawasaulisha masaibu ya Lakatare na inaonyesha hizo promo za CCM haziawaingia wananchi .Kazi wanayo ccm .
 
You have made ma worderful sunday MORE HEALTHIER.Nawahurumia sana CCM.Wakigeuka kila upande wanachapwa.kushoto wanatandikwa,kulia wanatandikwa, mbele wanatandikwa,nyuma vilevile,juu wanatandikwa,chini kama kawa.They are overwhelmed.Maskini CCM.bado CD ya Lwakatare,bado kufeli wanafunzi,bado jitegemee kampuni ya CCM iliyojipa tenda bandarini,bado Budget ya mwaka huu,bado majengo yanaanguka,nauli zimepanda,Mfumuko wa bei,Richmond wanalipwa etc,etc.Am realy Happy.
 
Sipati picha mtu mzima anatimua mbio na sanduku la kura.....hatareee, hongereni sana makamanda haikuwa kazi rahisi.:rockon:
 
Back
Top Bottom