CHADEMA yagawanyika mapokezi ya Lissu kwa sababu ya mbio za urais 2020 CHADEMA, ubadhilifu na ukanda

Ekethocho

Member
Jul 19, 2018
99
189
anakula,bata.jpg

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kinafanya Maandalizi ya Kumpokea aliyekuwa Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Antipas Lissu anayetarajiwa kuwasili nchini tarehe 07/09/2019 akitokea Ubelgiji alikokuwa akipata Matibabu.
Hata hivyo Chama hicho kimegawanyika namna ya kumpokea Mbunge huyo huku sababu za kugawanyika zikithibitika kuwa ni Makundi ya Urais 2020 ndani ya Chama hicho, Matumizi mabaya ya Madaraka na sababu nyingine ni ile ya siku zote ambayo imekuwa ikikitafuna Chama hicho ya Ukabila na Ukanda.

Mwenyekiti wa Chama hicho Taifa Freeman Mbowe (Mzee wa kubadili gia angani) anataka Lissu atoke moja kwa moja Ubelgiji na kushuka Uwanja wa Ndege wa Kimataifa na kuelekea Nyumbani kwake moja kwa moja na siyo mapokezi ya Maandamano ili kuepuka kupata kuungwa mkono na wanachama wengi wa Chama hicho kupitia Maandamano hayo.

Mbowe anaamini Mgombea urais kupitia Chama hicho katika Uchaguzi Mkuu wa 2020 atatoka tena CCM. Mbowe anaungwa mkono na Waziri Mkuu wa awamu ya tatu, Fredrick Tluwaye Sumaye na Wabunge wote wa Chama hicho ambao ni Wazaliwa wa Kanda ya Kaskazini akiwemo John Mnyika, Godbless Lema na Halima Mdee. Wengine wenye ushawishi ndani ya Chama walioko nyuma ya kundi hili ni Mbunge wa Tarime mjini, Ester Matiko na Mwenyekiti wa BAVICHA Taifa, Patrick Ole Sosopi

Katibu Mkuu wa Chama hicho, Vincent Mashinji haridhiki na namna Mbowe anavyotumia Fedha za Chama hicho na hivyo kuendesha Kampeni za kutaka aliyekuwa Mbunge wa Singida Kaskazini , Lazaro Nyalandu kuwa Mwenyekiti wa Chama hicho Taifa na Tundu Antipas Lissu kuwa Mgombea Urais wa Chama hicho Mwaka 2020. Kundi hili la Mashinji na Nyalandu linataka Lissu apate Mapokezi Makubwa yatakayotamalaki nchi nzima ili Mwanasheria huyo wa Chadema apate umaarufu zaidi kuelekea 2020.

Wengine walio nyuma ya kundi hili ni Mbunge wa Mlimba, Suzan Kiwanga, Mbunge wa Tarime Vijijini John Heche, Katibu Mwenezi CHADEMA Taifa Hemedi Ali(Kijana wa Kizanzibar) Taarifa zilizothibika zinasema Mashinji na Wenzake wanataka Lissu asije Dar es Salaam moja kwa moja na badala yake afikie kilimanjaro na kupokelewa na wafuasi wa chama hicho wa Mikoa ya Manyara , Arusha na Kilimanjaro na baadaye kuanza safari ya kwenda Dar es Salaam kwa Msafara utakaopitia Mikoa ya Tanga, na Pwani.

Inasemekana LISSU ataondoka Ubelgiji kati ya tarehe 04/09/2019 na tarehe 05/09/2019 na atatumia shirika la ndege la Uswisi au KLM.

Wito wangu kwa CHADEMA: Ni wakati wa kuwa kitu kimoja wakati huu tunapojianda kumpokea ndugu yetu na siyo kutumia ujio wake kukigawa chama.
 
Unajipendekeza uteuliwe kuwa msemaji wa Chadema? Kaombe kazi hii uko kwenu maana uku haufai hata kuwa msemaji wa kata
 
Tunawatakia kila la kheri.. ila msirumbane sana basi aishiiiii.. inajulikana juu yenu kwenye hilo la uraisi.

Fanyeni yote ila msiumizane kuichafua nchi hii.
 
Dhambi ya kuua, kutesa, kupoteza, kumchonganisha, kutenganisha na kupiga watu risasi itawatesa sana.
 
Propaganda aliziweza Nape japo naye zilikuja kumtafuna, ninyi vimburu wengine ni njaa kali ...msifikiri wananchi ni wajinga kama Chama chenu kinavyowatumia kina musiba na ninyi wenye akili ndogo kuwaaminisha watu!
 
Tunawatakia kila la kheri.. ila msirumbane sana basi aishiiiii.. inajulikana juu yenu kwenye hilo la uraisi.

Fanyeni yote ila msiumizane kuichafua nchi hii.
"Msirumbane" matamshi hayo tuu yamewajulisha wajuzi kuwa uko katika level ipi. Jitahidi kuongeza elimu maana hata ya ngumbaru ipo sio lazima shuleni
 
View attachment 1172795
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kinafanya Maandalizi ya Kumpokea aliyekuwa Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Antipas Lissu anayetarajiwa kuwasili nchini tarehe 07/09/2019 akitokea Ubelgiji alikokuwa akipata Matibabu.
Hata hivyo Chama hicho kimegawanyika namna ya kumpokea Mbunge huyo huku sababu za kugawanyika zikithibitika kuwa ni Makundi ya Urais 2020 ndani ya Chama hicho, Matumizi mabaya ya Madaraka na sababu nyingine ni ile ya siku zote ambayo imekuwa ikikitafuna Chama hicho ya Ukabila na Ukanda.

Mwenyekiti wa Chama hicho Taifa Freeman Mbowe (Mzee wa kubadili gia angani) anataka Lissu atoke moja kwa moja Ubelgiji na kushuka Uwanja wa Ndege wa Kimataifa na kuelekea Nyumbani kwake moja kwa moja na siyo mapokezi ya Maandamano ili kuepuka kupata kuungwa mkono na wanachama wengi wa Chama hicho kupitia Maandamano hayo.

Mbowe anaamini Mgombea urais kupitia Chama hicho katika Uchaguzi Mkuu wa 2020 atatoka tena CCM. Mbowe anaungwa mkono na Waziri Mkuu wa awamu ya tatu, Fredrick Tluwaye Sumaye na Wabunge wote wa Chama hicho ambao ni Wazaliwa wa Kanda ya Kaskazini akiwemo John Mnyika, Godbless Lema na Halima Mdee. Wengine wenye ushawishi ndani ya Chama walioko nyuma ya kundi hili ni Mbunge wa Tarime mjini, Ester Matiko na Mwenyekiti wa BAVICHA Taifa, Patrick Ole Sosopi

Katibu Mkuu wa Chama hicho, Vincent Mashinji haridhiki na namna Mbowe anavyotumia Fedha za Chama hicho na hivyo kuendesha Kampeni za kutaka aliyekuwa Mbunge wa Singida Kaskazini , Lazaro Nyalandu kuwa Mwenyekiti wa Chama hicho Taifa na Tundu Antipas Lissu kuwa Mgombea Urais wa Chama hicho Mwaka 2020. Kundi hili la Mashinji na Nyalandu linataka Lissu apate Mapokezi Makubwa yatakayotamalaki nchi nzima ili Mwanasheria huyo wa Chadema apate umaarufu zaidi kuelekea 2020.

Wengine walio nyuma ya kundi hili ni Mbunge wa Mlimba, Suzan Kiwanga, Mbunge wa Tarime Vijijini John Heche, Katibu Mwenezi CHADEMA Taifa Hemedi Ali(Kijana wa Kizanzibar) Taarifa zilizothibika zinasema Mashinji na Wenzake wanataka Lissu asije Dar es Salaam moja kwa moja na badala yake afikie kilimanjaro na kupokelewa na wafuasi wa chama hicho wa Mikoa ya Manyara , Arusha na Kilimanjaro na baadaye kuanza safari ya kwenda Dar es Salaam kwa Msafara utakaopitia Mikoa ya Tanga, na Pwani.

Inasemekana LISSU ataondoka Ubelgiji kati ya tarehe 04/09/2019 na tarehe 05/09/2019 na atatumia shirika la ndege la Uswisi au KLM.

Wito wangu kwa CHADEMA: Ni wakati wa kuwa kitu kimoja wakati huu tunapojianda kumpokea ndugu yetu na siyo kutumia ujio wake kukigawa chama.
Hawa jamaa wamekaa kikanda zaidi. Hili ndio tatizo lao kubwa litakaowamaliza kabisa.
 
Back
Top Bottom