Chadema yaduwaza uchaguzi udiwani mianzini

MAFILILI

JF-Expert Member
Apr 28, 2011
2,377
1,194
Ilikuwa ni patashika mara baada ya matokeo ya uchaguzi kuwekwa hadharani katika kata ya Mianzini mara ilipogundulika CHADEMA imeanguka vibaya sana huku CCM ikiibuka kidedea. Wananchi hawakushangaa matokeo kwa vile kampeni za CHADEMA ziliendeshwa pasipo mikakati ya ushindi pamoja na kutumia raslimali nyingi. Kati ya vyama vine vilivyoshiriki, CHADEMA kilishika nafasi ya pili kutoka mwisho, huku CCM ikiongozwa ikifuatiwa na CUF kwa tofauti kubwa sana. Kwa ujumla CHADEMA ilishindwa kufurukuta kutokana na sababu ifuatazo:-

1/ Kampeni kuratibiwa na uongozi wa CHADEMA wilaya ya Kinondoni.
2/ Kutokuwepo kwa ofisi za CHADEMA zilizo hai wilayani Temeke.
3/Shughuli za kampeni wakati wa uchaguzi kuratibiwa kutokea Kakonko BAR.
4/ Mgombea wa CHADEMA kutokuwa karibu na wakazi wa kata ya Mianzini.
5/ Ruzuku ya chama kupelekwa Arusha wakati ambapo mgombea wa Mianzini kutopata chochote toka makao makuu ya chama.

Kwa ujumla viongozi na wanachama wa CHADEMA mchukulie kushiriki uchaguzi mdogo wa udiwani mkoani DSM,hasa wilayani Temeke kama changamoto huku tukisubiri uchaguzi wa serikali za mitaa mwakani, vinginevyo mtapata AIBU kubwa mwakani kwa kutoambulia hata kiti kimoja wilayani Temeke
 
Hapo namba tatu kwa kweli umeniacha hoi,kampeni kuratibiwa kutokea bar??????????
 
temeke ni ya ccm wanaakili zao hawawezi kuchagua vurugu dar iache kama ilivyo.
 
Dar Es Salaam imewekwa kwenye chupa iliyofichwa Bagamoyo. Hatutegemei ukombozi wa nchi hii uanzie Dar labda Rais atoke upande wa pili.
 
sidhani kama dar unaweza kuwa mkoa wa kiukombozi wazaramo na ukombozi wapi nawapi??? angalia mikoa yenye wasomi ndio yenye changamoto lakini dar sidhani kwakweli huo ni mkoa wa mabwanyeye.
 
Kamanda Mwita Maranya alifanya kampeni kubwa sana humu jamvini lakini sie tunaokaa huku Mianzini kusema ukweli cdm hatukuwaona, inawezekana waliwekeza nguvu nyingi sana Arusha walikotegemea kushinda.
 
Last edited by a moderator:
sidhani kama dar unaweza kuwa mkoa wa kiukombozi wazaramo na ukombozi wapi nawapi??? angalia mikoa yenye wasomi ndio yenye changamoto lakini dar sidhani kwakweli huo no mkoa wa mabwanyeye.

Kwa bahati mbaya sana sasa hao unaowaita Wasomi wenye changamoto za ukombozi kanuni za Hisabati zinawatupa mkono, kwa maana wengi wetu sisi ndio kama hao Wazaramo, hapo sasa!
 
Bila shaka uelewa wa watu wa Temeke unaeleweka vema. Ni Wilaya pekee ambayo bado haipata mchanganyiko wa makabila mbalimbali. Wenyeji wa pwani bado wengi wako Temeke kuliko wilaya zilizobaki kwa upande wa Dar.
 
Kwa bahati mbaya sana sasa hao unaowaita Wasomi wenye changamoto za ukombozi kanuni za Hisabati zinawatupa mkono, kwa maana wengi wetu sisi ndio kama hao Wazaramo, hapo sasa!
kwa uelewa wako sidhani kama utaweza kuelewa nilicho maanisah,walio na uelewa wameelewa na hawana shida,kazi unayo
 
Sijawahi kuona analysis ya kijinga kama hii hapa JF.
This is JF, the home of Great thinkers.
Please try to write with FACTS and FIGURES.

Ulichoandika ni vitu vya kufirika zaidi kuliko uhalisia wenyewe. Inawezekana una hoja lakini umeshindwa kuiwasilisha vema na mwisho ukaharibu kwa kuweka ushabiki wa kimagamba.

Kwa mfano:
1/Haujaweka matokeo kamili yakoje.

2/Umeshindwa kutoa mchanganuo wowote kiwiano wa kura kati ya vyama.

3/Umeshindwa kuoanisha matokeo haya na uchaguzi uliopita 2010.
 
Kifupi analikuwa anatafuta buku saba ya leo iingie.
 
Hapo namba tatu kwa kweli umeniacha hoi,kampeni kuratibiwa kutokea bar??????????
Kakonko Bar ilipatiwa sekeseke la kufa mtu, ni moja ya Bar tulivu, safi lakini ikafugwa eti chafu. Sasa imefunguliwa CCM wamefungua tawi hapo. CCM ilaaniwe.
 
Back
Top Bottom