MAFILILI
JF-Expert Member
- Apr 28, 2011
- 2,377
- 1,194
Ilikuwa ni patashika mara baada ya matokeo ya uchaguzi kuwekwa hadharani katika kata ya Mianzini mara ilipogundulika CHADEMA imeanguka vibaya sana huku CCM ikiibuka kidedea. Wananchi hawakushangaa matokeo kwa vile kampeni za CHADEMA ziliendeshwa pasipo mikakati ya ushindi pamoja na kutumia raslimali nyingi. Kati ya vyama vine vilivyoshiriki, CHADEMA kilishika nafasi ya pili kutoka mwisho, huku CCM ikiongozwa ikifuatiwa na CUF kwa tofauti kubwa sana. Kwa ujumla CHADEMA ilishindwa kufurukuta kutokana na sababu ifuatazo:-
1/ Kampeni kuratibiwa na uongozi wa CHADEMA wilaya ya Kinondoni.
2/ Kutokuwepo kwa ofisi za CHADEMA zilizo hai wilayani Temeke.
3/Shughuli za kampeni wakati wa uchaguzi kuratibiwa kutokea Kakonko BAR.
4/ Mgombea wa CHADEMA kutokuwa karibu na wakazi wa kata ya Mianzini.
5/ Ruzuku ya chama kupelekwa Arusha wakati ambapo mgombea wa Mianzini kutopata chochote toka makao makuu ya chama.
Kwa ujumla viongozi na wanachama wa CHADEMA mchukulie kushiriki uchaguzi mdogo wa udiwani mkoani DSM,hasa wilayani Temeke kama changamoto huku tukisubiri uchaguzi wa serikali za mitaa mwakani, vinginevyo mtapata AIBU kubwa mwakani kwa kutoambulia hata kiti kimoja wilayani Temeke