CHADEMA yaanzisha operesheni ondoa msaliti

Donatila

JF-Expert Member
Oct 23, 2014
7,557
21,515
CUF_.jpg


Dar es Salaam.
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimetangaza operesheni maalumu ijulikanayo kama Ondoa Msaliti Buguruni (OMB) kwa lengo la kutatua mgogoro unaokikabili Chama cha Wananchi (CUF).

Operesheni hiyo ya kidemokrasia imeanza rasmi leo Julai 10, ambapo vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) vimelenga kumuunga mkono Katibu wa CUF, Maalim Seif.

Akizungumza leo wakati wa kutangaza operesheni hiyo, Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA kanda ya Pwani, Saed Kubenea amesema kuwa mgogoro huo una athari kubwa kwa vyama vya upinzani hivyo wameamua kuungana pamoja ili kuimarisha vyama vya upinzani chini ya mwavuli wa Ukawa.

Kubenea ambaye pia ni Mbunge wa Ubungo, ameeleza kuwa baada ya kukaa na viongozi wa CUF ili kujua kiini cha mgogoro huo wamebaini kuwa siyo mgogoro ndani ya chama, bali unachochewa na CCM wanaomtumia Profesa Lipumba ambaye wamemuita kama ni msaliti.

"Sisi kama CHADEMA tumeamua kuwasaidia viongozi na wanachama wa CUF kumuondoa msaliti Lipumba Buguruni na kutupa nguo zake na viongozi halali wa CUF watarudi Buguruni, "amesema Kubenea.

Kadhalika amesema pamoja na mambo mengine, chama kimeazimia kuwa mameya wa Manispaa zote za Jiji la Dar es Salaam wasitoe ushirikiano kwa viongozi wenye ushirikiano na Profesa Lipumba.

Chanzo:
Mwananchi
 
Chadema yaanzisha Operesheni Ondoa Msaliti

Haya ni baadhi ya mambo ya kujiuliza mapema!!!
Watafanikisha hili?
Mbona matamko mengi hatutekelezi??


CUF_.jpg

Dar es Salaam.
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimetangaza operesheni maalumu ijulikanayo kama Ondoa Msaliti Buguruni (OMB) kwa lengo la kutatua mgogoro unaokikabili Chama cha Wananchi (CUF).

Operesheni hiyo ya kidemokrasia imeanza rasmi leo Julai 10, ambapo vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) vimelenga kumuunga mkono Katibu wa CUF, Maalim Seif.

Akizungumza leo wakati wa kutangaza operesheni hiyo, Makamu Mwenyekiti wa Chadema kanda ya Pwani, Saed Kubenea amesema kuwa mgogoro huo una athari kubwa kwa vyama vya upinzani hivyo wameamua kuungana pamoja ili kuimarisha vyama vya upinzani chini ya mwavuli wa Ukawa.

Kubenea ambaye pia ni Mbunge wa Ubungo, ameeleza kuwa baada ya kukaa na viongozi wa CUF ili kujua kiini cha mgogoro huo wamebaini kuwa siyo mgogoro ndani ya chama, bali unachochewa na CCM wanaomtumia Profesa Lipumba ambaye wamemuita kama ni msaliti.

"Sisi kama Chadema tumeamua kuwasaidia viongozi na wanachama wa CUF kumuondoa msaliti Lipumba Buguruni na kutupa nguo zake na viongozi halali wa CUF watarudi Buguruni, "amesema Kubenea.

Kadhalika amesema pamoja na mambo mengine, chama kimeazimia kuwa mameya wa Manispaa zote za Jiji la Dar es Salaam wasitoe ushirikiano kwa viongozi wenye ushirikiano na Profesa Lipumba.
 
Huo ukawa mwanzo wa maisha ya kubangaiza ya Kubenea. Kwa kipindi cha takribani miaka mitatu, Kubenea akawa anaishi kwa kuwapiga mizinga wanasiasa kama Salum Londa na Mwita Gachuma. Hawa ndiyo wafadhili waliomweka mjini Kubenea.

Ndipo Profesa Ibrahim Lipumba wa CUF akajitokeza na kumwokoa Kubenea.Akamchukua mwandishi huyo na kuwa msaidizi wake wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2005. Baadhi ya wana CUFhawakufurahishwa na uamuzi wa Lipumba kumchukua Kubenea lakini Profesa alishikilia msimamo wake.

Hadi leo, wapo wana CUF wanaoamini kuwa Kubenea alihusika na tukio la Lipumba kuibiwa kompyuta mpakato yake (laptop) kwenye siku za mwisho za kampeni hiyo. Lipumba ndiye aliyekuwa mgombea tishio wa upinzani kwenye uchaguzi huo na laptop hiyo ilikuwa na kila taarifa.

Kwa sababu ya mahusiano ya nyuma baina ya Kubenea na CCM, iliaminika kuwa pengine Kubenea aliichukua na kuipeleka kwa chama tawala ili kijue taarifa za CUF. Hadi leokompyuta ile haijawahi kupatikana.

Aliyewaunganisha Lipumba na Kubenea alikuwa ni aliyekuwa Mbunge wa Wawi (CUF), Hamad Rashid Mohamed. Baada ya kampeni zile, Lipumba alimpa Kubenea mtaji wa kuanzisha gazeti ambalo baadaye lilikuja kufahamika kwa jina la HaliHalisi na kutumika kama gazeti rasmi la kambi ya upinzani bungeni upinzani.

Baadaye, Kubenea na Hamad Rashid wakagombana na gazeti la HaliHalisi likafa. Hadi wakati huo, Kubenea alikuwaakijitambulisha kama mwana CUF wa kufa au kupona na aliandika makala nyingi za kukisifu pamoja na Lipumba.

Kufa kwa HaliHalisi na Kubenea kuhamia Chadema.

Saed Kubenea: Ndumilakuwili mbobezi
 
Kila nikitaka kuandika vidole vinajaa maji sijui kwanini, labda zamu yangu ya kulipa mil 7 imefika.

Ila kimsingi nataka kusema kuna wakati risasi ina nguvu kuliko maneno.
Namuomba sana Mungu na nnasubiria kwa hamu wakati watu wa aina ya Lema na mimi watakapopata nafasi zaidi kiutendaji, vinginevyo nawatakia kila laheri kwenye ugomvi wa maneno, mimi huwa siuwezagi.
 
JPM noma mwaka wa pili sasa hakuna maandamano, teh! teh! teh! teh.....
Isipokuwa kumshangilia yeye. Makaburu walifanya hivyohivyo, lakini pamoja na maguvu yote walishindwa kubadilisha yaliyo mioyoni mwa wananchi wenye uzalendo. Ila waliwapata wasaliti, wachumia matumbo.

Sent from my HUAWEI Y530-U00 using JamiiForums mobile app
 
Hizi operation zinanikumbusha vision za Africa kila kukicha utasikia vsionya 2000 sasa masikia tunayo inayosema mpaka 2020 waziri wa ustawi wa jamii leo kasema. CDM ni chama kikubwa sana, kikiendelea kujifanya chama cha migogoro ya watu yatakikuta yaliyowakuta NCCR-Mageuzi. Nina imani kubwa kabisa hiyo mizigo mikubwa miwili waliyopewa na rafiki zao CCM wakiitupia nje mwaka 2020, hasa yule wa mvi maana mke wake ana usongo wa kuitwa first lady, wajue atahama na watu wake na kwenda hata ACT. Huyu jamaa wanatakiwa kumshika kama glass bila kuangusha maana ana nguvu zaidi ya CDM, kule CCM nusura awabomoe alishindwa kwasababu CCM wamejikita na wana mizizi lakini huko CDM hakuna miziz.

Baada ya kujiimarisha kwa wananchi majimboni mwao wanamuacha Magu apige kampeni zake kirahisi namna hii, na wanavyompinga japo wakati mwingine wana agenda ya maana jamaa anasema wanatetea wezi. Balaa.
 
Sasa ni dhahiri chadema wamepoteza muelekeo
Kuingilia mgogoro wa CUF ni kupoteza bure nguvu za chadema,kwani Lipumba hang'oki na mwaka 2020,watalalamika wameibiwa kura
 
Back
Top Bottom