CHADEMA yaanzisha operesheni ondoa msaliti

Msaliti namba moja ni Mbowe, alitusaliti wana mabadiliko na kuuza chama kwa fisadi Lowasa

Sent from my TECNO-W5 using JamiiForums mobile app
Si kweli Tanzania tuna Fisadi Magufull tu ambaye amehamishia paton la taifa Chato
 
Huo ukawa mwanzo wa maisha ya kubangaiza ya Kubenea. Kwa kipindi cha takribani miaka mitatu, Kubenea akawa anaishi kwa kuwapiga mizinga wanasiasa kama Salum Londa na Mwita Gachuma. Hawa ndiyo wafadhili waliomweka mjini Kubenea.

Ndipo Profesa Ibrahim Lipumba wa CUF akajitokeza na kumwokoa Kubenea.Akamchukua mwandishi huyo na kuwa msaidizi wake wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2005. Baadhi ya wana CUFhawakufurahishwa na uamuzi wa Lipumba kumchukua Kubenea lakini Profesa alishikilia msimamo wake.

Hadi leo, wapo wana CUF wanaoamini kuwa Kubenea alihusika na tukio la Lipumba kuibiwa kompyuta mpakato yake (laptop) kwenye siku za mwisho za kampeni hiyo. Lipumba ndiye aliyekuwa mgombea tishio wa upinzani kwenye uchaguzi huo na laptop hiyo ilikuwa na kila taarifa.

Kwa sababu ya mahusiano ya nyuma baina ya Kubenea na CCM, iliaminika kuwa pengine Kubenea aliichukua na kuipeleka kwa chama tawala ili kijue taarifa za CUF. Hadi leokompyuta ile haijawahi kupatikana.

Aliyewaunganisha Lipumba na Kubenea alikuwa ni aliyekuwa Mbunge wa Wawi (CUF), Hamad Rashid Mohamed. Baada ya kampeni zile, Lipumba alimpa Kubenea mtaji wa kuanzisha gazeti ambalo baadaye lilikuja kufahamika kwa jina la HaliHalisi na kutumika kama gazeti rasmi la kambi ya upinzani bungeni upinzani.

Baadaye, Kubenea na Hamad Rashid wakagombana na gazeti la HaliHalisi likafa. Hadi wakati huo, Kubenea alikuwaakijitambulisha kama mwana CUF wa kufa au kupona na aliandika makala nyingi za kukisifu pamoja na Lipumba.

Kufa kwa HaliHalisi na Kubenea kuhamia Chadema.

Saed Kubenea: Ndumilakuwili mbobezi
Toba yarabi maulana!
Kubenea ni zaidi ya Shilole kwa mujibu wa shutuma hizo.
 
CUF_.jpg

Dar es Salaam.
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimetangaza operesheni maalumu ijulikanayo kama Ondoa Msaliti Buguruni (OMB) kwa lengo la kutatua mgogoro unaokikabili Chama cha Wananchi (CUF).

Operesheni hiyo ya kidemokrasia imeanza rasmi leo Julai 10, ambapo vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) vimelenga kumuunga mkono Katibu wa CUF, Maalim Seif.

Akizungumza leo wakati wa kutangaza operesheni hiyo, Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA kanda ya Pwani, Saed Kubenea amesema kuwa mgogoro huo una athari kubwa kwa vyama vya upinzani hivyo wameamua kuungana pamoja ili kuimarisha vyama vya upinzani chini ya mwavuli wa Ukawa.

Kubenea ambaye pia ni Mbunge wa Ubungo, ameeleza kuwa baada ya kukaa na viongozi wa CUF ili kujua kiini cha mgogoro huo wamebaini kuwa siyo mgogoro ndani ya chama, bali unachochewa na CCM wanaomtumia Profesa Lipumba ambaye wamemuita kama ni msaliti.

"Sisi kama CHADEMA tumeamua kuwasaidia viongozi na wanachama wa CUF kumuondoa msaliti Lipumba Buguruni na kutupa nguo zake na viongozi halali wa CUF watarudi Buguruni, "amesema Kubenea.

Kadhalika amesema pamoja na mambo mengine, chama kimeazimia kuwa mameya wa Manispaa zote za Jiji la Dar es Salaam wasitoe ushirikiano kwa viongozi wenye ushirikiano na Profesa Lipumba.

Chanzo:
Mwananchi
Hivi mnapigania Katiba ya wananchi na akina LOWASA na KINGUNGE?
Ile ya UKUTA profesa aliita ukuta wenyewe ulikuwa wa BISCUTI - UKAWASHINDA
Huu wa MPINGO wa UNYAMWEZI mtauweza?
 
Wanacheza mziki wa sisiemu taratiiibu, sisiemu wanatisha sana, hivi tactician wao mkuu ni nani?? Jamaa akiamua wacheze sindimba chadema bila kuumiza kichwa wanaingia mazima, akibadili biti la mchiriku masela wa chadema hao, dah!!
....siasa na muzikiii acha kelele cheza muzikiii uuuwiiiiiiiiiii...........
Mpaka 2021 akili zikiwarudi treni itakuwa mbali sana!
 
msijaribu ngosha jamani fanyani kazi acheni hizi habari za maandamano yalisha pitwa na wakati hizi zama nyingine jamaani haya mtakumbuka maneno yangu.
 
Ikiwa mtu unahisi una akili timamu alafu hizo akili zinakusukuma kushangilia upuuzi huu unaoitwa OMB, nenda hospitali haraka yawezekana ujitambui.
CUF_.jpg

Dar es Salaam.
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimetangaza operesheni maalumu ijulikanayo kama Ondoa Msaliti Buguruni (OMB) kwa lengo la kutatua mgogoro unaokikabili Chama cha Wananchi (CUF).

Operesheni hiyo ya kidemokrasia imeanza rasmi leo Julai 10, ambapo vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) vimelenga kumuunga mkono Katibu wa CUF, Maalim Seif.

Akizungumza leo wakati wa kutangaza operesheni hiyo, Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA kanda ya Pwani, Saed Kubenea amesema kuwa mgogoro huo una athari kubwa kwa vyama vya upinzani hivyo wameamua kuungana pamoja ili kuimarisha vyama vya upinzani chini ya mwavuli wa Ukawa.

Kubenea ambaye pia ni Mbunge wa Ubungo, ameeleza kuwa baada ya kukaa na viongozi wa CUF ili kujua kiini cha mgogoro huo wamebaini kuwa siyo mgogoro ndani ya chama, bali unachochewa na CCM wanaomtumia Profesa Lipumba ambaye wamemuita kama ni msaliti.

"Sisi kama CHADEMA tumeamua kuwasaidia viongozi na wanachama wa CUF kumuondoa msaliti Lipumba Buguruni na kutupa nguo zake na viongozi halali wa CUF watarudi Buguruni, "amesema Kubenea.

Kadhalika amesema pamoja na mambo mengine, chama kimeazimia kuwa mameya wa Manispaa zote za Jiji la Dar es Salaam wasitoe ushirikiano kwa viongozi wenye ushirikiano na Profesa Lipumba.

Chanzo:
Mwananchi
 
Wanaochochea mgogoro wa CUF ni ccm na CDM kwa maslai yao.

Endeleeni kuibomoa CUF tu ili mvune wanachama wao.
 
Eti vyama vinavyounda UKAWA ...vipi hivyo? CUF ndio hiyo mnaipigania isife then vinabaki vyama gani hai nje ya Chadema? Hili koti la UKAWA ni ujanja ujanja mwingine wa kupotezeana muda ....
 
Natafakari tu. Chama cha siasa chenye ofisi zake ufipa kinondoni, kinafungaje safari kwenda kujishughulisha na mwenyekiti wa chama kingine kilichoko buguruni? Hivi hii operation ikitafsiriwa ni uvamizi na wizi kupelekea kosa la jinai, kukamatwa na polisi na kufunguliwa mashitaka itakuwa ni makosa? ushauri
Chadema waendesheshe siasa zao kama chama na waachane na CUF, na njia bora ya kumsaidia maalim ni kuanzisha chama kingine na kukisajili ili kama yeye ndiye anaekubalika basi cuf-lipmba na cu-seif viunde chama kipya chenye nguvu.
 
Back
Top Bottom