CHADEMA yaanza rasmi kampeni za Anga Arumeru | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CHADEMA yaanza rasmi kampeni za Anga Arumeru

Discussion in 'Chaguzi Ndogo' started by Molemo, Mar 22, 2012.

 1. M

  Molemo JF-Expert Member

  #1
  Mar 22, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Chama cha Demokrasia na Maendeleo-CDM kimeanza rasmi kutumia helikopta kumnadi mgombea ubunge wa jimbo la Arumeru Joshua Nasari.Katibu Mkuu wa CDM Dr Wilbrod Slaa ametumia helikopta leo kuzunguka vijiji mbalimbali kumnadi Nasari.Kila alikopita na helikopta alilakiwa na umati mkubwa wa watu.Source:ITV Habari

  [​IMG]
   
 2. F

  FJM JF-Expert Member

  #2
  Mar 22, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Kuweni makini na matumizi CHADEMA, maana kuna majimbo yatakuwa wazi muda si mrefu. Segerea ni moja, Muheza wanapelekana mahakamani na sasa tunasikia Kibaha kuna mtu anataka kuachana na siasa uchwara. bana matumizi.
   
 3. Mzee wa Rula

  Mzee wa Rula JF-Expert Member

  #3
  Mar 22, 2012
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 8,177
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Mkuu usihofu hicho no chama makini nadhani kila kitu kitakuwa ndani ya bajeti.
   
 4. idawa

  idawa JF-Expert Member

  #4
  Mar 22, 2012
  Joined: Jan 20, 2012
  Messages: 18,519
  Likes Received: 10,436
  Trophy Points: 280
  sisi wengine tunasubiri jimbo tu.
   
 5. M

  Molemo JF-Expert Member

  #5
  Mar 22, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Mkuu wangu usijali na ndio maana kesho kuna harambee iliyoombwa na wananchi kumchangia mgombea.
   
 6. chitambikwa

  chitambikwa JF-Expert Member

  #6
  Mar 22, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 3,940
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Ardhini tumemaliza
   
 7. M

  Molemo JF-Expert Member

  #7
  Mar 22, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Usishangae Magamba nao wakaiga wakaanza nao kurusha helikopta
   
 8. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #8
  Mar 22, 2012
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  Igunga hazikuwasaidia sana wananchi waliishia kushangaa Helkopta za chadema na CCM ingawa waanzilishi wa siasa za anga ni chadema wakamwagwa pwaaaaaaaaaaaaaaaaaaa
   
 9. O

  Otorong'ong'o JF-Expert Member

  #9
  Mar 22, 2012
  Joined: Aug 17, 2011
  Messages: 31,067
  Likes Received: 10,426
  Trophy Points: 280
  Sasa ni anga..
   
 10. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #10
  Mar 22, 2012
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  siasa za ardhini CCM watashinda na siasa za anga chadema watashinda..............wapiga kura wengi wako ardhini.
   
 11. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #11
  Mar 22, 2012
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  Jimbo la Arusha nalo litakuwa wazi Godbless Lema atakaposhindwa kesi na Kawe lingekuwa wazi kama chadema wasingeomba sulusu kwa Mbatia.
   
 12. Babuu blessed

  Babuu blessed JF-Expert Member

  #12
  Mar 22, 2012
  Joined: Oct 14, 2010
  Messages: 1,340
  Likes Received: 98
  Trophy Points: 145
  uzinduzi walishdwa kurusha LIVE kwenye kideo wakat TBC niyakwao.mkuu molemo nasikia ccm wananunua vitambulisho kuna mdogo wangu yupo univrsty of arusha ameniambia kuna watu wanapgia wanafunz simu wakitaka wawakabith vitambulsho kwa sh 10000,kama upo arumeru washaurini watu watunze vitambulisho wasimpe mtu.INANIUMA SANA CCM WANAPOTUMIA UJINGA WA WANANCH KUJINUFAISHA
   
 13. UmkhontoweSizwe

  UmkhontoweSizwe JF-Expert Member

  #13
  Mar 22, 2012
  Joined: Dec 19, 2008
  Messages: 2,956
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  CCm si waliutangazia umma kwamba cdm wanafanya harambee kwa kuwa wamefilisika baada ya ufadhiri kukatwa; sasa hizi za kukodi helkopta zimetoka wapi? Au ndo mwendelezo wa taarifa za UONGO toka chama tawala?! Mhhh, ccm kwa uongo hamjambo.
   
 14. C

  Chintu JF-Expert Member

  #14
  Mar 22, 2012
  Joined: Feb 4, 2011
  Messages: 3,399
  Likes Received: 856
  Trophy Points: 280
  Kwa tunaopenda kuchangia nguvu ya ukombozi - vipi ule mpango wa kuchangia kwa kutuma sms CHADEMA kwenda number 15710 bado upo? kwa mwenye habari tafadhari atujulishe. nipo nje ya mtandao wa voda lakini nikipata network nitajaribu nione kama bado ile account inaoperate.
   
 15. h

  hans79 JF-Expert Member

  #15
  Mar 23, 2012
  Joined: May 4, 2011
  Messages: 3,802
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 145
  umebaki na mipasho tu,mwenzio mbatia kajisalimisha la sivyo asingekuwa na mbunge hata mmoja wote walitaka kujiuzuru.na bado mwaka huu hamtoki kwa mashambulizi ya anga + ardhini raha tupu.ardhini LOWASA anawashika na anga ndio usipime CHADEMA(THE NGUVU YA UMMA) tumo.hatutaki kesi kamwagize hakimu atoe hukumu hata leo uone nguvu ya umma inavyofanya kazi kwa ushahidi nenda katafute au kama uliangalia itv saa mbili usiku ndo mtajijua jinsi mlivyo watupu.hawaowi na chemba leo wamehutubia majengo + miti na ilikuwa kali ya mwaka anayehutubiwa haonekani, kwa wahedi leo itv wametenda haki arumeru.mwaka huu hamtoki mmeshikwa kila pahala,chaguzi zote ndogo andikeni maumivu.

  jk kaambiwa ajiuzuru kutokana na kutumia vibaya nembo ys karamazoo ktk uchaguzi 2011 na asipofanya hivyo UN(MAREKANI + WASHIRIKA WAKE) watamgadafi na bado kila mlotenda gizani kuonekana mwangani,twasubiri na marudio ya uchaguzi wa rais kabla ya 2015.makinda kisha watabiria ya kuwa wabunge wengi wa ccm kujiuzuru kabla ya 2015,tulia acha joto mmekatwa kila kona na nguvu ya umma.

  Mwangalie mpiga chabo maarufu pichani
   
 16. h

  hans79 JF-Expert Member

  #16
  Mar 23, 2012
  Joined: May 4, 2011
  Messages: 3,802
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 145
  ushindane na mpumbavu usije fananae na pia mbunge wao mwingine katolewa nduki na wananchi sengerema,hao wameshindwa achana nao.tujenge chama letu CHADEMA.
   
 17. bibikuku

  bibikuku JF-Expert Member

  #17
  Mar 23, 2012
  Joined: Feb 16, 2011
  Messages: 828
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  CHADEMA yaanza kutumia Helikopta

  Neville Meena na Mussa Juma, Arumeru
  CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) jana kilianza kutumia helkopta katika kampeni zake za kumnadi mgombea wake wa ubunge katika uchaguzi mdogo wa Jimbo la Arumeru Mashariki, Joshua Nassari.

  Habari ambazo gazeti hili limezipata zinasema helkopta hiyo itaendelea kutumika hadi siku ya mwisho ya kampeni na kwamba itakiwezesha chama hicho kufanya mikutano kati ya mitano hadi minane kwa siku.

  Mkuu wa Operesheni wa uchaguzi wa Chadema katika jimbo hilo, John Mrema alisema kuanza kutumika kwa helkopta hiyo kutamwezesha mgombea wao kufanya mikutano mitano kwenye kata tano tofauti.

  Mikutano ya jana ilifanyika katika vijiji vya Ngurdoto Kata ya Maji ya Chai, Ngabobo Kata ya Ngarenanyuki, Kijiji cha Sakila Kata ya Kikatiti na vijiji na kata za King’ori na Nkoanrua.

  Helkopta hiyo ilianza kuonekana katika anga la Usa River, Arumeru jana asubuhi na hakukuwa na taarifa za awali kuhusu ujio wake kama ambavyo chama hicho kimekuwa kikifanya katika kampeni nyingine zilizotangulia.

  Helkopta hiyo yenye maneno makubwa CHADEMA, ilitumika wakati wa uzinduzi wa kampeni za chama hicho zilizofanyika katika Uwanja wa Shule ya msingi Leganga, Usa River Machi 10 mwaka huu na tangu wakati huo haikuwahi kuonekana tena hadi jana.

  Dk Slaa na ardhi

  Katikamikutano ya jana, Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa alimshambulia Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Gudluck Ole Medeye kwamba anahusika na kukodisha shamba la Valesca lililo Jimbo la Arumeru Mashariki kwa wawekezaji kwa bei ya kutupa.

  Akizungumza katika mkutano wa hadhara katika kijiji cha Ngabobo, Ngurdoto na Sakila, Dk Slaa alisema ni aibu mawaziri wa Serikali ya CCM kuomba kura katika Jimbo la Arumeru Mashariki huku wakiwa ni waasisi wa mpango wa kugawa ardhi ya umma kwa walowezi wa kizungu.

  Alisema Naibu Waziri huyo, ambaye ni mbunge wa Jimbo la Arumeru Magharibi, kabla ya kukubali kutolewa shamba hilo lenye zaidi ya ekari 400 ambalo Serikali itapata kiasi cha Sh2.4 milioni tu kwa mwaka walipaswa kuwakumbuka wananchi.

  “Hivi kweli nyie wananchi wa Meru hamuhitaji ardhi hii na mngeshindwa kulipa Sh6000 kwa ekari moja ili muweze kulima, kama alivyouziwa mzungu? ”alihoji Dk Slaa.

  Aliwataka wakazi wa jimbo hilo, kukubali mabadiliko sasa kwa kuchagua mbunge wa upinzani ili aweze kuhoji ardhi ya Meru ambayo kiasi kikubwa kimegawanywa kwa walowezi kutoka nje ya nchi.

  MY TAKE: Sasa hivi wazee wa kuiga (CCM) wataleta Choppa, kama hamuamini angalieni after 3 days!!
   
 18. MARCKO

  MARCKO JF-Expert Member

  #18
  Mar 23, 2012
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 2,265
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  CDM kimbilio letu!
   
 19. Mwana Mpotevu

  Mwana Mpotevu Platinum Member

  #19
  Mar 23, 2012
  Joined: Sep 7, 2011
  Messages: 3,294
  Likes Received: 333
  Trophy Points: 180
  kumbe hela ipo, sasa fundraising ya weekend hii kwa ajili ya nini? lakini nawaombea ushindi
   
 20. bibikuku

  bibikuku JF-Expert Member

  #20
  Mar 23, 2012
  Joined: Feb 16, 2011
  Messages: 828
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  tatizo vituo bandia 55 CCM wameshaviandaa na NEC haivitambui, wizi wa kura as ususl
   
Loading...