Waziri wa Kilimo Mhandisi Chiza ameichambua HOTUBA ya waziri kilimo wa Chadema kuwa haina viwango ilijikita kutoa lawama badala ya majibu muafaka.
Kwa kweli ukifuatilia hotuba ya Waziri Chiza utagundua CCM ipo makini kutatua matatizo ya kilimo wakati CHADEMA wamebaki kupiga kelele kwa kutumia mawaziri vivuli wasio na viwango
IPO makini kwa lipi?kama ni maneno matamu yameanza leo? acha unafiki na upambe kwa kusifia hata visivyopaswa kusifiwa.Leo hii takwimu zinakuambia nusu ya wilaya zote zinakabiliwa na tatizo la njaa,unakabiliwaje na njaa kama una sera nzuri na zinazomsaidia mkulima?
Angalia udhaifu wa sera ulivyozaa mlolongo wa kauli mbiu zisizo na mashiko...............kilimo cha kufa na kupona,,,,,,,,,kilimo kwa wote.........kilimo uti wa mgongo,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,kilimo kwanza.
Huku ni kushindwa na huhitaji kusifiwa na hotuba ya waziri kivuli bila kufanya lolote.sitashangaa kama utakuwa huoni kuwa ccm imeshindwa kwenye kilimo na hii inaweza kuwa wewe si mkulima na hivyo kufeli au kufaulu kwa mkulima hakukusaidii.
Mambo muhimu kama kilimo yanayogusa asilimia zaidi ya 75 ya watanzania sio ya kuyafanyia usanii, haijalishi madhara wanayopata wakulima cha msingi ni kumpongeza waziri ili ccm ionekane imefanikiwa!!! so what? kwa nini ucheze na future ya watanzania kwa sababu ya ccm? kwani ccm ni nani? NA ANA UMUHIMU GANI KTK MAISHA YANGU?