CHADEMA Wilaya ya Mwanga

CHADEMA Wilaya ya Mwanga

Jumanne Mkota

JF-Expert Member
Joined
Jan 25, 2012
Posts
3,011
Reaction score
1,793
Wadau JF

CHADEMA vipi! ni swali ambalo najiuliza kila siku hasa hapa Wilayani Mwanga.Hakuna Ubishi kuwa katika Wilaya ya Mwanga Chama cha Demokrasia na Maendeleo kilianzia harakati zake Kata ya Kileo.

Mimi ni miongoni mwa mashuhuda jinsi gani walivyojitoa kwa wananchi hawa kwa vipindi mbali mbali vigumu wanavyopitia hasa mafuriko ya maji kutoka mto Ghona ambayo kila msimu wa mvua lazima wakutane na dhahama hii ya kuharibiwa mazao yao na makazi yao kutokana na maji.

Itakumbukwa eneo la Kituri miaka michache iliyopita ambapo CHADEMA mlikuwa nao bega kwa bega(kipindi hicho nilikuwa bado nasoma sikuwa mwanachama )

Lakini juzi hapa wananchi hawa wamepigwa na kimbunga ambacho kimesababisha watu sitin kukosa makazi. CHADEMA Mwanga na Mkoa wa Kilimanjaro hamjaja hata kuwapa pole wanachama wenu waliokumbwa na kadhia hii.

Hawahitaji fedha faraja tu inatosha. Mkumbuke kuwa mnakitongoji mnakishikilia hapa katika Kata hii kati ya vitongoji 94 vilivyopo Mwanga.Na kwa bahati mbaya sana vitongoji vyote viwili mlivyokuwa navyo vinakumbwa na majanga ya asili ya vimbunga na Mafuriko.

Kwa ujumla ni vitongoji vya majaribu sana kwenu kwani magamba wanaangalia kuwa mtafanya nini wakati matatizo hayo yanapowatokea wananchi wa vitongoji hivyo.

Kwa mtizamo wangu njooni muwape pole hawa waathirika. Tunataka sana kuiamsha mwanga lakini uongozi wa CHADEMA wilaya ni kama upo likizo. nimewatafuta kwenye simu zao hawapatikani na Ofisi pia wamefunga sijui wako wapi. Mkoa saidieni hili. na Pia kwa sababu mgombea Ubunge wa CHADEMA mwanga ni Member humu nadhani ataona na ku take action kwenye hili

Naomba kuwasilisha
 
Bado wanagawana ruzuku kulipia madeni waliokopa kwa Mbowe wkt wa uchague I wa mwaka 1995/2000. Watakuja tu msiwe na wasiwasi
acha kuingiza UJINGA wenu wa kimagamba kwenye mambo ya msingi. Kukukumbashana ni ada na ndicho nilichofanya. ya kina mbowe na ruzuku yamekujaje? grow mkuu
 
Haya ndo Madhara mengine ya Shule za Kata, watu wanakuwa na Ubongon wa Konokono, Maafa inatakiwa yashughulikiwe na Serikali, Wewe ulisha wahi ona mfano kule USA, kimetokea then unawaona Democratic na Republican wakienda kutoa pole, sio kazi yao,

CCM wamekuwa wakitumia majanga kama hayo kisiasa, kitu ambacho sio kizuri kabisa,
 
acha kuingiza usenge wenu wa kimagamba kwenye mambo ya msingi. Kukukumbashana ni ada na ndicho nilichofanya. ya kina mbowe na ruzuku yamekujaje? grow mkuu

Mi Nadhani usenge unao wewe, mwaname mzima unalalamika wanaume wenzio waje kukushughulikia!
 
Haya ndo Madhara mengine ya Shule za Kata, watu wanakuwa na Ubongon wa Konokono, Maafa inatakiwa yashughulikiwe na Serikali, Wewe ulisha wahi ona mfano kule USA, kimetokea then unawaona Democratic na Republican wakienda kutoa pole, sio kazi yao,

CCM wamekuwa wakitumia majanga kama hayo kisiasa, kitu ambacho sio kizuri kabisa,
Mkuu Chasa elimu ni zaidi ya kuta nne za darasa. kuhusu faraja ni suala la kibinadamu. Na si kweli kuwa serikali ndio inatakiwa ishughulikie maafa tu. Kwa mfano nyumba yako ikaungua moto hutataka msaada wa jirani mpaka Ofisi ya waziri mkuu kitengo cha maafa kije?
 
Chini ya Pinda kuna kitengo cha maafa kwa nchi nzima.. vipi hilo lilifikiriwa kwanza ama blabla nyingi?
 
Chini ya Pinda kuna kitengo cha maafa kwa nchi nzima.. vipi hilo lilifikiriwa kwanza ama blabla nyingi?
Kutoa faraja kwa wahanga waliopata madhara sio lazima kitengo cha waziri mkuu. Chadema kama chama cha siasa ni vizuri kuonyesha upendo kwa wananchi ambao wanasubiri kwa hamu 2015 ifike wawape nchi waiongoze. Ni vizuri Chadema mkajenga ukaribu na wananchi sasa, wananchi hawa wameteseka chini ya utawala wa maccm kwa miaka 51 kuweni nao karibu na muwafariji wakati wa shida. Faraja sio lazima iwe misaada au fedha, hata neno POLE linatosha
 
Hivi hawa watu wanaowaombea watu wao msaada na kisha kumwaga matusi ya nguoni wana Elimu kiasi gani? It is pathetic.

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
 
hivi hawa watu wanaowaombea watu wao msaada na kisha kumwaga matusi ya nguoni wana elimu kiasi gani? It is pathetic.

Sent from my blackberry 9860 using jamiiforums
tusi lipo wapi mkuu nimeshaliondoa . Samahani mkuu
 
Mi Nadhani usenge unao wewe, mwaname mzima unalalamika wanaume wenzio waje kukushughulikia!
Malafyale ni neno linalobeba heshima kubwa kwa kabila la wanyakyusa, we unajiita Mwanafyale..sina hakika labda hutokei mbeya.,ila niseme kweli kule tu kukaribiana kwa majina haya kunanifanya nijisikie
nakereka,kama utataka kulitumia basi lazima utumie akili badala ya tumbo.
 
... hebu tema kwanza hayo machicha mdomoni ndio tuzungumze!!!
 
Mwana ukimdekeza lazima iko siku akuharibie. Watu walizoe kutukana "mafisadi" wakawa wanashangiliwa leo yamegeuka kila mtu anatukanwa! INASIKITISHA SANA!!
 
Back
Top Bottom