CHADEMA wazomewa Mwanza

CHADEMA wazomewa Mwanza

kaka h

Member
Joined
Sep 6, 2010
Posts
38
Reaction score
7
VIONGOZI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wa Wilaya za Misungwi, Nyamagana, Geita na wafuasi wao, jana walionja joto ya jiwe, baada ya wananchi wa eneo la Senta kuwazomea na kuambulia watu wachache kwenye mkutano wa hadhara.

Mkutano huo, ulinusurika kuvunjika kwa kupata watu hao kidogo, baada ya Diwani wa Kata ya Buselesele wilayani Geita, aliyetajwa kwa jina moja la Kagoma, kutumia muda mwingi wa hotuba yake kumfagilia Mbunge wa Misungwi, Charles Kitwanga kwa kuchapa kazi za maendeleo na kupambana na ubadhirifu kwenye halmashauri hiyo.

Hatua hiyo, ilionekana kuwakera wananchi waliotaka kujua mkutano huo ulikuwa na lengo la kuwaeleza nini, kutokana na madai kuwa wamekuwa wakifanya mikutano na kuishia kutoa lugha za matusi.

Dalili za kukosa watu katika mkutano huo, uliotakiwa uanze saa 9:00 alasiri, zilianza kuonekana wakati gari la matangazo na lile la M4C lilipowasili kwenye kituo cha daladala cha Misasi kwa mbwembwe na kujikuta wakizomewa na wapiga debe na baadhi ya wananchi waliokuwepo maeneo hayo.

Akihutubia mkutano huo kwa kusoma alama za nyakati, Diwani Kagoma aliishia kumfagilia Kitwanga "Mawe Matatu", akidai kuwa anapambana na ubadhirifu kwa sababu anataka wananchi wapate huduma bora za jamii, lakini baadhi ya viongozi wa chama chake (CCM) wanampiga vita kwa sababu ya maslahi yao binafsi.
 
Hata huko ulikotupeleka ni umbeya mtupu, not a credible source.
 
Hindee moniii -- hindeee monii eeee - pumba eee pumba; utakula pumbaa....
wabunge.jpg
 
Mleta uzi atakuwa amevurugwa tu,anaongelea eneo la senta ipi? mara buselesele,misugwi,misasi,geita! ndo nini maana yake? acha kukurupuka wewe gamba tuwekee picha tuone!
 
Wewe chaumbeya utachanbwa vibaya .au wewe msukule hujui mambo yanayo endelea hapa tz.nyoooo chadema yazomewa .kacheze huko mchiruku na ccm wezio
 
VIONGOZI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wa Wilaya za Misungwi, Nyamagana, Geita na wafuasi wao, jana walionja joto ya jiwe, baada ya wananchi wa eneo la Senta kuwazomea na kuambulia watu wachache kwenye mkutano wa hadhara.

Mkutano huo, ulinusurika kuvunjika kwa kupata watu hao kidogo, baada ya Diwani wa Kata ya Buselesele wilayani Geita, aliyetajwa kwa jina moja la Kagoma, kutumia muda mwingi wa hotuba yake kumfagilia Mbunge wa Misungwi, Charles Kitwanga kwa kuchapa kazi za maendeleo na kupambana na ubadhirifu kwenye halmashauri hiyo.

Hatua hiyo, ilionekana kuwakera wananchi waliotaka kujua mkutano huo ulikuwa na lengo la kuwaeleza nini, kutokana na madai kuwa wamekuwa wakifanya mikutano na kuishia kutoa lugha za matusi.

Dalili za kukosa watu katika mkutano huo, uliotakiwa uanze saa 9:00 alasiri, zilianza kuonekana wakati gari la matangazo na lile la M4C lilipowasili kwenye kituo cha daladala cha Misasi kwa mbwembwe na kujikuta wakizomewa na wapiga debe na baadhi ya wananchi waliokuwepo maeneo hayo.

Akihutubia mkutano huo kwa kusoma alama za nyakati, Diwani Kagoma aliishia kumfagilia Kitwanga “Mawe Matatu”, akidai kuwa anapambana na ubadhirifu kwa sababu anataka wananchi wapate huduma bora za jamii, lakini baadhi ya viongozi wa chama chake (CCM) wanampiga vita kwa sababu ya maslahi yao binafsi.

Hapa ndipo mnapokosea, hii ngoma ya kuzomewa ni yenu maccm hapa unabalance equation, yaani unawadhibitishia wananchi kuwa kuzomea ni poa.

MTAJUTA KUIFAHAMU CHADEMA
 
Masikini chama cha machina aka ukoo wa panya unaweweseka,haya kachukue double buku saba walau na wewe uende chooni...
 
mleta huu uzi ni mmbea,mini npo mwanza chadema huku ni noumaaaaaa
 
Kumbe alizomewa sababu aliwasifia maccm! Miccm bana hadi raha!
 
huko kuzomewa ni ishara kuwa wananchi wamewachoka
 
Back
Top Bottom