CHADEMA wazidi kujipanga; Wenje Mambo ya Nje

EasyFit

JF-Expert Member
Jul 4, 2011
1,269
1,082
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimemteua Mbunge wa Nyamagana, Ezekiah Wenje kuwa Mkurugenzi wa Mambo ya Nje na Uhusiano wa Kimataifa wa chama hicho. Anajaza nafasi iliyoachwa wazi na John Mnyika aliyeteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Habari na Uenezi.

Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Wilbroad Slaa alisema jana kuwa pamoja na uteuzi huo, Wenje ataendelea pia kutumikia Baraza Kivuli la Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni kwa nafasi yake ya Waziri Kivuli wa Mambo ya Nje na Uhusiano wa Kimataifa.

Hongera Chadema.

 
Safi sana Wenje kwa uteuzi huo unafaa sana,kaza buti ukombozi upatikane Tanzania,tupo nyuma yako.
 
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimemteua Mbunge wa Nyamagana, Ezekiah Wenje kuwa Mkurugenzi wa Mambo ya Nje na Uhusiano wa Kimataifa wa chama hicho.

Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Wilbroad Slaa alisema jana kuwa pamoja na uteuzi huo, Wenje ataendelea pia kutumikia Baraza Kivuli la Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni kwa nafasi yake ya Waziri Kivuli wa Mambo ya Nje na Uhusiano wa Kimataifa.

Kwa uteuzi huo, Wenje anajaza nafasi iliyokuwa ikitumikiwa na Mbunge wa Ubungo, John Mnyika ambaye ameteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa Chadema.

Ofisa Habari wa Chadema, Tumaini Makene alisema jana kuwa chama hicho kimejipanga kuendelea kutimiza wajibu wa chama hicho kwa Watanzania.

Pia alisema chama hicho kitaendelea kutumia njia nyingine zote za kidemokrasia ili kuunganisha Watanzania katika uwajibikaji wa Serikali na viongozi wake na kuchochea maendeleo ya watu.

"Wananchi watarajie Chadema kuendelea na ziara katika mikoa mbalimbali mijini na vijijini tukiweka kipaumbele kwa maeneo ambayo chama hakikufika kwa ukamilifu katika mwaka 2011 kwa kufuata ratiba itakayotangazwa na Kamati Kuu.

"Kwa mwaka 2012, vipaumbele vikuu ni kuboresha mchakato wa mabadiliko ya Katiba ili Tanzania iwe na Katiba mpya na bora," alisema Makene.

Alisema kipaumbele cha chama katika nyanja ya uchumi ni kunusuru uchumi wa nchi na kupunguza ongezeko la kupanda kwa gharama za maisha na kuongeza uzalishaji bila kufafanua njia watakazotumia kuongeza uzalishaji huo.

Katika masuala ya jamii, Makene alisema kipaumbele ni kushughulikia vyanzo vya migogoro katika maeneo mbalimbali badala ya kukabiliana na matokeo au viashiria vya matatizo bila kuweka iwapo watatumia maandamano na kama yatasaidia kuongeza uzalishaji kama ilivyo katika kipaumbele cha uchumi.
 
Vizuri sana.Wenje anafaa sana.Chama makini na sikivu kwa manufaa ya watanzania
 

Hongera Wenje. Lakini mbona hakuna tofauti na CCM kwamba mtu ni Mbunge kisha analundikiwa vyeo vingine. CDM ingejitofautisha na CCM kwa kuwapa vyeo vijana wengine ambao si wabunge ili nao waonekanane mbele ya watanzania. Sasa kila siku ni hao hao tuuuuu! Wenje, Mnyika, Zitto Wenje, Mnyika, Zitto! Wapeni vijana wengine nao vyeo jamani. Hao wabunge waachwe na shughuli za kutekeleza ahadi zao majimboni pamoja na shughuli za uwazir vivuli.
 
Hongera Wenje, Hongera CHADEMA, uteuzi umezingatia uwezo wa mtu na mahitaji ya wananchi kwa wakati.
 

bora umeliona, utadhani wengine hakuna. Kuna watu wanafanya kazi, lakini hawana nafasi ya kiutendaji nadani ya chama. Hao wangetumika kuimarisha chama. Mifano ni wale wote waliogombea nafasi mbalimbali za ubunge, hao ni mhimu kwani licha ya kuwa viongozi, itawatia moyo wa kujipanga kwa uchaguzi unaofuata.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…