CHADEMA wazidi kuitesa CCM | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CHADEMA wazidi kuitesa CCM

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Sokomoko, Oct 20, 2008.

 1. Sokomoko

  Sokomoko JF-Expert Member

  #1
  Oct 20, 2008
  Joined: Mar 29, 2008
  Messages: 1,918
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  CHADEMA wazidi kuitesa CCM
  Mwenyekiti Mbowe akihutubia Musoma mjini
  na Kulwa Karedia  MAMIA ya wakazi wa mji wa Musoma na vitongoji vyake jana walijitokeza kwa wingi katika uzinduzi wa kampeni ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ‘Operesheni Sangara’, ambapo wito ulitolewa kwa Rais Jakaya Kikwete kuwafikisha mahakamani mafisadi wote walioiba fedha katika Akaunti ya Malipo ya Nje (EPA).

  Wito huo ulitolewa mjini hapa na Katibu wa chama hicho, Dk. Willibrod Slaa, wakati akihutubia mamia ya wananchi kwenye uwanja wa Shule ya Msingi ya Mkendo.

  Alisema endapo Rais Kikwete atashindwa kuwashughulikia mafisadi hao, ni bora kuwaachia wafungwa wote waliomo katika magereza mbalimbali nchini.

  Mkakati wa ‘Operesheni Sangara’ umelenga zaidi kupeleka madaraka kwa wananchi kuanzia ngazi za chini hadi taifa, ili kujenga uwezo wa chama.

  “Napenda kumwambia Rais Kikwete kwamba sasa muda wa Rais Kikwete kuona kipimo cha uongozi wake ni Oktoba 31 pale atakapowafikisha mahakamani mafisadi wote… lakini kama hatafanya hivyo, tunasema wafungwa wote walioko gerezani waachiwe, ili haki itendeke kwa wote,” alisema Dk. Slaa.

  Alisema iwapo Rais Kikwete atashindwa kufanya hivyo atasababisha wananchi kuendelea kupoteza imani kwake, kama sasa ambapo wamefikia hatua ya kupiga mawe msafara wake.

  “Ni jambo la ajabu mkuu wa nchi kutupiwa mawe akiwa katika shughuli za serikali. Hii inaonyesha wazi jinsi wananchi walivyoanza kuchoshwa na serikali yake… tunasema kama ataendelea na mwenendo huu anastahili kuondolewa hata kesho,” alisema Dk. Slaaa.

  Alisema kushindwa kwa serikali ya Kikwete kutoa maisha bora kwa kila Mtanzania kumetokana na wasaidizi wake wengi kujali masilahi binafsi, badala ya kutumikia umma.

  Alisema tangu Rais Kikwete alipoingia madarakani wananchi walikuwa na matumaini makubwa, lakini hivi sasa wamekata tama, baada ya kunyanyaswa na watu waliopewa dhamana ya kuwasaidia.

  Dk. Slaa alisema pamoja na hatua atakazochukua Rais Kikwete juu ya mafisadi, bado CHADEMA italipua bomu la ufisadi wa sh milioni 155 zilizoibiwa katika mgodi wa dhahabu wa Buhemba kupitia Kampuni ya Meremeta inayomilikiwa na Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).

  “Rais tulimwambia mambo mengi kuhusu wizi wa fedha za umma, lakini tunashangaa kuona ameamua kushughulikia EPA peke yake, nawaambia jamani tulimwambia atupatie maelezo, lakini amekuwa akitukwepa kila siku.

  “Ufisadi mkubwa uliofanywa kwenye Kampuni ya Meremeta chini ya JWTZ sasa tunasema tutawasha moto hadi kuona waliochukua fedha hizi wanajulikana,” alisema Dk. Slaa.

  Kwa upande wake, Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho, Zitto Kabwe, alisema serikali ya CCM imechoka na sasa umefika wakati wa kukaa kando na kuachia kizazi kipya ambacho anaamini kuwa kitaleta mageuzi ya kweli.

  “Chama kimejaa mafisadi, wanalindana, wamechoka hata kwa mawazo, tunasema wakazi wa Musoma mna wakati wa kufanya maamuzi kama yaliyofanywa na ndugu zenu kule Tarime, ambako CCM tuliibwaga bila ubishi na leo hii tukifanya tathmini ya gharama za maisha, mtaona serikali ya Kikwete ilivyosababisha umaskini kuongezeka,” alisema Zitto.

  Huku akishangiliwa na maelfu ya wananchi, Zitto alisema taifa limeuzwa, kwani rasilimali zote muhimu zikiwemo madini, samaki, mbuga zimeuzwa kwa wakezaji kutoka nje ya nchi.

  “Tumekuwa na rasilimali nyingi ambazo zimeuzwa kwa wawekezaji wa nje… hata bajeti yetu ya serikali imeendelea kubaki tegemezi, kwani mpaka sasa wafadhili wanatoa asilimia 34. Hii ni aibu kubwa, tukatae fedheha hii,” alisema Zitto.

  Aidha, Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe, ambaye alifungua rasmi operesheni hiyo, alisema huo ni mpango uliobuniwa na CHADEMA bila kujali jinsia, rangi wala itikadi, kwa lengo la kulikomboa taifa.

  “Leo hii (jana) tumeanzisha vuguvugu la kweli lenye kuleta mapinduzi mapya na tumeamua kuzindulia hapa Musoma, kwa sababu ya kumuenzi hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, ambaye ni mzaliwa wa mkoa huu,” alisema Mbowe.

  Katika mkutano huo, wanachama zaidi ya 400 wa CCM walirudisha kadi zao na kukabidhiwa za CHADEMA, wakiwamo mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Vijana (mkoa), Gewa Anthony, na aliyekuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana Wilaya ya Musoma (UVCCM), Hamis Tumbo.
  Source: Tanzania Daima

   
 2. K

  Karandinga Member

  #2
  Oct 20, 2008
  Joined: Jun 25, 2008
  Messages: 66
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Waandishi wetu wa habari inabidi wawe waangalifu kidogo..

  Wito huo ulitolewa mjini hapa na Katibu wa chama hicho, Dk. Willibrod Slaa, wakati akihutubia mamia ya wananchi kwenye uwanja wa Shule ya Msingi ya Mkendo.

  Halafu..

  Huku akishangiliwa na maelfu ya wananchi, Zitto alisema taifa limeuzwa, kwani rasilimali zote muhimu zikiwemo madini, samaki, mbuga zimeuzwa kwa wakezaji kutoka nje ya nchi.

  Anyway it is very encouraging to see Tanzanian's slowly wiping the cold out of their eyes as they begin to wake up from their deep slumber.... DK. Slaa and Comrade Zitto keep the fire burning.....Mpaka kieleweke!!
   
 3. M

  MkamaP JF-Expert Member

  #3
  Oct 20, 2008
  Joined: Jan 27, 2007
  Messages: 7,313
  Likes Received: 1,452
  Trophy Points: 280

  Mimi namuunga mkono mwanakijiji
  Kuwa hii nchi tuibinafisishe tu yani MAKATIBU WAKUU wote wawe WAZUNGU,najua mtasema najidharirisha lakini ukweli ndio huo.

  MIMI niwape siri moja tuseme wajerumani wote wahamie Tanzania leo harafu watanzania wote wahamie ujerumani na kila kitu watuachie .Nakupeni ni miaka mitano tu tunaanza kubigana kumbo ubalozi wa tanzania kutafuta namna yakwenda kubbeba mabox nakutafuta elimu bora huko tz.
   
 4. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #4
  Oct 21, 2008
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,543
  Likes Received: 1,892
  Trophy Points: 280
  Maneno mazito sana hayo kutoka kwenye hiyo CHADEMA TRIO.
  Watanzania ni muhimu kuunga mkono juhudi za wazalendo hawa.
   
 5. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #5
  Oct 21, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,405
  Likes Received: 81,432
  Trophy Points: 280
  Tatizo siyo Watanzania bali ni viongozi wabovu ambao wanajali zaidi maslahi yao badala ya yale ya Taifa. Kumbuka tulipopata uhuru tulikuwa hatuna chuo kikuu, tulikuwa na mashule machache sana ya sekondari, tulikuwa hatuna makampuni yetu wala viwanda. Kutokana na vision ya Mwalimu kuhakikisha uchumi wa Tanzania unakuwa mikononi mwa Watanzania akajenga chuo kikuu na vyuo vingine ili kuhakikisha Watanzania wanaelimishwa ndani ya nchi yetu na wao ndiyo wanaoshika madaraka ndani ya juu katika makampuni na viwanda hivyo. Akajenga viwanda mbali mbali pamoja na kuunda makampuni yaliyofanya biashara ndani na nje ya nchi. Akajenga mahospitali, kwa kweli alifanya juhudi kubwa sana kuhakikisha uchumi unakuwa mikonono mwa Watanzania.

  Hivyo ni kweli kabisa kama viongozi wataweka usanii na ufisadi pembeni na kuweka maslahi ya Taifa letu mbele basi tunaweza kupiga hatua kubwa sana kimaendeleo kwa faida ya Watanzania wote. Tanzania siyo nchi maskini tuna utajiri mwingi sana kupitia rasilmali zetu, kinatochotuangusha ni sera mbovu za walio madarakani katika kusaini mikataba ya rasilimali zetu na kutaka kuishi kwa gharama za hali ya juu kushinda hata viongozi wa nchi tajiri duniani.
   
Loading...