Dume la Mende
JF-Expert Member
- Mar 23, 2011
- 423
- 66
Nimekusoma mkuuNarudia kusema wanaokimbilia bungeni hawana msaada wowote na wananchi zaidi ya kujineemesha wenyewe. Hivi si tunawajua wafanyabiashara wakubwa wa upinzani? mbona wao hawathubutu kusema mishahara yao iende kusaidia wapiga kura majimboni mwao kwa kuwa wao wapo kuwatumikia wananchi na wanatosheka na wanachokipata kwenye biashara zao? si tuna mawakili maarufu wanaosimamia makesi makubwa na wanalipwa vizuri? mbona hawapo tayari ku sacrifice mishahara yao ili ilipie watoto mayatima kwenye majimbo yao ada za shule? mil 7 zinaweza kulipia watoto wangapi wa shule za kata?
Ifike wakati tutambue wanasiasa wapo kwenye siasa kwa manufaa yao na kutafuta protections na sio kwa ajili ya kukutumikia wewe! wachache wana dhamira hizo lakini kipato ni masikini na hawana biashara yoyote ndio maana wanapigania hizo posho.
Hii habari iko kishabiki zaidi, source not disclosed.
Rating 0.4/10.
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeingia kwenye mgogoro baada ya baadhi ya wabunge kupandwa na hasira dhidi ya wenzao wanaoendesha kampeni ya kutaka posho za vikao kwa wabunge ziondolewe.Mkwaruzano huo iliibuka ndani ya kikao cha wabunge wa Kambi ya Upinzani Bungeni inayoongozwa na Mwenyekiti wa Taifa wa Chadema na Mbunge wa Hai, Freeman Mbowe.
Kikao hicho kiliitishwa na kambi hiyyo kwa lengo la kuweka msimamo wa kupinga posho za vikao kwa wabunge, lakini kikageuka uwanja wa vita uliozusha vurumai kubwa kiasi cha kushindwa kufikia muafaka.
Baada ya kikao hicho kufunguliwa, John Mnyika (Ubungo-Chadema) aliwasilisha hoja hiyo ya kutaka wabunge wa upinzani kuweka msimamo wa pamoja wa kupinga posho hizo ili mkakati huo ulioanzia kwenye Bunge hilo la Bajeti, uweze kufanikiwa.
Akifikiri ataungwa mkono, Mnyika aliwataka wabunge kuonyesha moyo huo wa kishujaa kwa kutosaini kitabu cha mahudhurio bungeni, lakini wawepo ndani ya vikao.
Kauli hiyo ya Mnyika ilikuwa sawa na kumwaga petroli kwenye moto unaowaka ambapo wabunge watatu wa Chadema (majina tunayahifadhi kwa sasa) walikuja juu na kupinga vikali hoja hiyo.
Upinzani huo mkali uliotolewa na wabunge hao ulidhihirisha kauli ya Waziri Mkuu Mizengo Pinda aliyesema kuwa ingawa baadhi ya wabunge wa chama hicho wanajionyesha kimbelembele kusisitiza mpango huo, wengine wa chama hicho pia wanaumia kimoyomoyo, lakini hawasemi.
Suala la kukataa posho bungeni lilianzishwa na Zitto Kabwe (Kigoma Kaskazini-Chadema) akisema zinaenda kinyume na mpango wa Taifa wa kupambana na umasikini kwa kuondoa posho zisizo na tija.
Zitto akionekana kuwa na ushupavu mkubwa ilifikia mahali akaamua kutosaini mahudhurio Bungeni ili jina lake lisiorodheshwe miongoni mwa watakaolipwa licha ya Spika, Anne Makinda kutishia kuwa kitendo hicho kinaweza kumfukuzisha bungeni.
Mkakati wa Mnyika ulikuwa ni wabunge wote wa upinzani kuwa na mshikamano katika hilo jambo ambalo sasa limeonekena kuwa ni nyongo kiasi cha wengine kutaka kuwararua wenzao wakisema ni msimamo usio na maana.
Source: Gazeti la habari za kiswahili la kila siku Tanzania, linaongoza
Jamaa wanaweza wakaandamana fasta kupingana wao kwa wao Teh teh
Naam, kwakweli hakuna marefu yasiyo na ncha na penye haki uongo hujiengua.Methali na msemo huu umekuja baada kuuona mkanganyiko mkubwa wa kauli za CHADEMA zinazotolewa na viongozi wao Mahasimu .Kauli zinazotolewa na viongozi hao zinapelekea kuyaengua mahubiri ya uongo yanaohubiriwa na viongozi hao wadhalimu.Mikutano na maandamo haramu yanayoendeshwa na chama hicho chenye viongozi na wafuasi wenye tabia za kizulu za kupenda vita;imejikita katika kuhubiri mapambano dhidi ya Rushwa,ufisadi maisha magumu na hivi karibuni kuna sakata la posho za wabunge huko Dodoma.kujikanganya kwa chama hicho hasimu, kumedhihirika baada ya chama hicho kwenda tofauti na yale yanohubiriwa.Bila shaka sote ni mashahidi kuwa chama kimekuwa kikihubiri mapambano dhidiya rushwa na ufisadi, wakati huohuo katibu mkuu wa chama hicho,Padri Slaa akikifanyia ufisadi chama chake kwa kukishiniza kumlipa ml.7.5 huku akipinga ml.7 zinzopokelewa na wabunge akinadi kuwa huko ni kuifilisi Nchi.Evi jamani tuache kwanzwa suala ushabiki hapa,kupi kuifilisi Nchi kati ya kupokea ml.7.5 na ml.7? ambapo zote hizo ni fedha za wananchi wetu tunaojinadi kuwa tunawaonea huruma.Hivyobasi, hapa ndipo CHADEMA inapojikanganya katika kauli zake na hatimaye kutarajia anguko kubwa la chama hicho pale waloghiribiwa akili watakapouona unga wa Rutuba.Aidha mkanganyiko mwingine unajipambanua pale chama hicho kilipopanga mkakati wa kupinga posho za wabunge kikidai kuwa kupokea posho hizo ni sawa na kuwadumbukiza wananchi shimoni,huku mwenyekiti wa chama hicho,Freeman Mbowe, akiwa msitari wa mbele kusaini fomu za mahudhurio ambapo kwa pamoja hujumuishwa na kupewa posho wakati wa kusaini kama alivyo kaririwa Spika wa bunge hilo lililoingiliwa na wana muziki wanaovesika watoapo hoja.Huu ni mkanganyiko mwingine wa chama hicho ambapo viongozi wake wanajikanganya kwa yale wanayohubiri na yale wanayotenda na hii ni ishara ya kuanguka kwa chama hicho katika siku za usoni.Maana wahenga walisema kuwa"jahazi linapopoteza mwelekeo kinachofuata ni kuyumba na kuzama,ndivyo ilvyo kwa CHADEMA ya sasa.Je nyie wanamagwanda hamuoni mkanganyiko huo? unaobainisha unafiki wa viongo wenu.Kwanini mmekuwa viziwi,vipofu na mabubu kiasi hicho. Tafakarini ndugu zangu.Nimalizie kwa kusema kuwa "NO ONE CAN MAKE YOU BETTER WITHOUT YOUR OWN EFFORTS".
Narudia kusema wanaokimbilia bungeni hawana msaada wowote na wananchi zaidi ya kujineemesha wenyewe. Hivi si tunawajua wafanyabiashara wakubwa wa upinzani? mbona wao hawathubutu kusema mishahara yao iende kusaidia wapiga kura majimboni mwao kwa kuwa wao wapo kuwatumikia wananchi na wanatosheka na wanachokipata kwenye biashara zao? si tuna mawakili maarufu wanaosimamia makesi makubwa na wanalipwa vizuri? mbona hawapo tayari ku sacrifice mishahara yao ili ilipie watoto mayatima kwenye majimbo yao ada za shule? mil 7 zinaweza kulipia watoto wangapi wa shule za kata?
Ifike wakati tutambue wanasiasa wapo kwenye siasa kwa manufaa yao na kutafuta protections na sio kwa ajili ya kukutumikia wewe! wachache wana dhamira hizo lakini kipato ni masikini na hawana biashara yoyote ndio maana wanapigania hizo posho.
Kwanini mmekuwa viziwi,vipofu na mabubu kiasi hicho.