CHADEMA watoa tamko kuhusu Virusi vya Corona

Moja kati ya Matamko Boora kabisa katika historia ya Tanzania, Big Up CDM
 
Nimesikiliza sekunde14 bando yangu imeniuma!
Uchafu mtupu! Eti serikari uzuie mikusanyiko makanisani na mashuleni!
Nahisi alikuwa kwenye kikao cha kusuruhisha ugonvi wa mbowe na wenzake hata hajasikia tangazo la PM.
 
..Tangazo la CDM linaonyesha weledi kuliko lile la serikali.
Mkuu Joka Kuu, kama Chadema imeonyesha weledi kuliko serikali, jee hii ina maana sasa Chadema imewiva kiasi kwamba sasa inaweza kuaminiwa na Watanzania kuongoza serikali?.
By the way, Chadema kila mtu ni msemaji wa chama?
P
 
LILE JUKWAA LA JF DOCTOR KAZI YAKE NI NINI?

Kwanini Thread za CORONA/COVID_19 zinaletwa Jukwaa la Siasa badala ya Jukwaa la JF Doctor?

Hii manayake Watanzania CCM/UPINZANI wanatumia Corona kana mtaji wa Kisiasa kwa kila Mmoja kuonesha umwamba wake.

Ni upumbavu Mtupu kwa hizi siasa uchwara.
 
CDM wasichoke kushauri Serikali hii na zile zijazo maana huo ni wajibu wao kama wapinzani.
 
Mkuu Joka Kuu, kama Chadema imeonyesha weledi kuliko serikali, jee hii ina maana sasa Chadema imewiva kiasi kwamba sasa inaweza kuaminiwa na Watanzania kuongoza serikali?.
By the way, Chadema kila mtu ni msemaji wa chama?
P

Hicho chama kimegeuka kuwa kikundi cha kupiga fedha za rudhuku mkuu p.
Mrema anaongea, Lema anaongea, mbowe yeye sasa anazidi kuhamasisha vikao.

Mi ninavyojua kazi ya chadema saivi nikutengeneza kesi nakupiga pesa kupitia mawakiri.
 
Ahsante sana CHADEMA..siku itafika nitachukua kadi
Mkuu Joka Kuu, kama Chadema imeonyesha weledi kuliko serikali, jee hii ina maana sasa Chadema imewiva kiasi kwamba sasa inaweza kuaminiwa na Watanzania kuongoza serikali?.
By the way, Chadema kila mtu ni msemaji wa chama?
P
Ni lini CCM iliaminiwa kuongoza watanzania?
 
Mimi sio mtaalamu wa kiswahili lakini neno lililotumika "tunataka" kidogo linaleta ukakasi kwa watu wenye uelewa wa chini badala yake wangetumia "tunashauri"

Ushauri wao niwamsingi ukichambuliwa vizuri na kufanyiwa kazi kwa haraka tutaweza kupunguza speed ya maambukuzi na kuendelea na shughli za maendeleo.

Asante mtoa mada umeeleweka.

Sent using Jamii Forums mobile app
Matumizi ya lugha kwa viongozi wetu sio jambo lakufuatilia sana maana kuna maneno yanatumika adi mtu unashtuka. Kwa mtazamo wangu sioni tatizo katika neno tunataka, hii ni kwa sababu ya jambo husika linalo zungumziwa. Lakini huo ni mtazamo wangu mimi kama mimi.
 
Hicho chama kimegeuka kuwa kikundi cha kupiga fedha za rudhuku mkuu p.
Mrema anaongea, Lema anaongea, mbowe yeye sasa anazidi kuhamasisha vikao.

Mi ninavyojua kazi ya chadema saivi nikutengeneza kesi nakupiga pesa kupitia mawakiri.
Alafu eti na wewe una haki sawa ya kutoa mawazo na kupiga kura ...aiseee inauma ila ndo hivyo
 
Back
Top Bottom