Emma.
JF-Expert Member
- Jun 25, 2012
- 19,932
- 5,560
CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO (CHADEMA) tumepokea kwa masikitiko makubwa msiba wa Mhe Leticia Nyerere uliotokea nchini Marekani. Tunatoa pole kwa familia, ndugu, jamaa, na marafiki katika wakati huu mgumu wa kuondokewa na mpendwa wao. Mwenyezi Mungu awatie moyo wa ujasiri na subira katika wakati huu mgumu wa majonzi ya msiba huo.
Kama chama tutamkumbuka marehemu Leticia Nyerere kwa mchango wake na ushiriki wake wakati wote alipokuwa mwanachama wetu na akiwa miongoni mwa watu waliopata fursa za wabunge kupitia CHADEMA.
Bwana alitoa, bwana ametwaa jina la Bwana lihimidiwe.
Imetolewa leo, Jumanne 12.01.2016
Tumaini Makene