Chadema watishia kurudi kwa wananchi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Chadema watishia kurudi kwa wananchi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by FJM, Jun 17, 2011.

 1. F

  FJM JF-Expert Member

  #1
  Jun 17, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Chadema kimesema kuwa kama Serikali haitasikiliza hoja yao kuhusu posho watarudi kwa wananchi na kuandamana.

  Mbowe amesema hata Mpango wa Maendeleo wa Serikali wa miaka mitano umezungumzia suala la kupunguzwa kwa posho za safari na kusema kuwa hoja yao ni ya msingi na inazungumzika.

  "Ni bahati mbaya sana kusikia Waziri Mkuu anasema wasiochukua posho zitarudi Hazina, wakati Serikali anayoiongoza imeleta hoja hiyo hapa bungeni kwenye mpango wa maendeleo wa miaka mitano,"alisema Mbowe na kuongeza:

  "Mbunge kwa mwezi anapata zaidi ya Sh7 milioni, je ni watumishi wangapi katika nchi hii wanapata mshahara wa zaidi ya Sh1 milioni?"Alihoji.

  Alisema Waziri Mkuu anazungumzia suala hilo kama ni la wabunge pekee wakati wao wanazungumzia wananchi wote, kwani pesa hizo zitapelekwa kwenye shughuli mbalimbali za maendeleo.

  "Kama wasipobadilisha hizi posho tutakutana na wananchi kwenye maandamano,"alisema.
  Alisema posho wanayoilalamikia ni (sitting allowance) na kwamba kila mtu anahitaji mishahara mizuri na si mbunge pekee.

  Alisema kuzungumza bungeni na kukaa kwenye kamati ni kazi ya mbunge na kuhoji kwanini mbunge huyo alipwe kwa ajili ya kukaa tu. Mbowe alisema hivi sasa mapato mengi yanayokusanywa na Serikali yanaishia kwenye kulipana posho.

  Source: Mwananchi 17th June 2011
   
 2. KIMBURU

  KIMBURU JF-Expert Member

  #2
  Jun 17, 2011
  Joined: Jan 12, 2011
  Messages: 210
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Nimeshangaa sana kuona hata Pinda amepinda. Kweli CCM hakuna mwenye huruma na wananchi; nilijua Pinda atetea hili kumbe na yeye ndio walewale.

  Haiingii akilini kuona mtu analipwa milion 7 kwa mwezi halafu bado analilia posho ya vikao, eti anafanya kazi ngumu; wakati mwalimu anayeteseka na maisha magumu kijijini analipwa 150000 na hiyo posho ndio kwanza msamiati kwake. Halafu at the same time mnasema mnataka kupunguza gape kati ya aliyenacho na asiyenacho.


  Wabunge wetu wa CDM kazeni uzi sisi huku uraiani tunapima tu zipi pumba upi mchele, nani anatutetea na nani anajitetea. Mwisho wa siku itafahamika tu; na tukiona 2015 ni mbali tutajua chakufanya.
   
Loading...