Msimamo wangu.
Nimekuwa nikitafakari sana juu ya hili la Rukwa hadi mwenyekiti yule mzee kuamua kukaa pembeni maana yake ameumia kwa mbowe kukataa kufuata maoni ya chama huko Rukwa. Sasa basi, kwa kuwa nilitamani na ninaendelea kutamani mabadiliko, nilikuwa tayari kuipigia chadema bila kujali mapungufu yake ya wazi ambayo yalikuwa yakitolewa na wanachama hasa ya umungumtu wa Mbowe, nimeamua yafuatayo:-
1. Kuanzia sasa sitaipigia chadema kura yangu tena ktk uchaguzi wowote ule isipokuwa iwapo Mbowe ataachia madaraka ndani ya miaka mitatu kuelekea uchaguzi mkuu 2020. Akishindwa kuwajibika ndani ya muda huo, hata akiwajibika mfano 2019, sitowaunga mkono hadi 2020 ipite. Kura yangu imeondoka pia na ya watu kadhaa niliokuwa nawaaminisha umhimu wa mabadiliko ya mifumo ya kiutawala.
2. Sishawishiki kuunga chama chochote cha upinzani nje ya chadema. Wala siwazi juu ya mbadala wake. Hivyo sitaki kusikia cuf, nccr wala act wazalendo. wote hao sina imani nao hasa hao wazalendo sitaki kuwasikia kabisa. Aidha sitopig kura au nitaangalia mgombea wa ccm aliyesimamishwa. kama ni mtu bomba, nitampa huyo.
Uamuzi wangu umeathiriwa na mambo makubwa mawili lkn kubwa zaidi moja.
1. Kumpa mtu ubunge aliokuwa ameukataa kwa kuasi chama na kupigia kampeni vyama vingine. Wabunge wa namna hii ndo sawa na wale waliokuwa wakifanya kazi wakitokea USA kwa Obama. hawana msaada kwa chama. Pia tuhuma za Ruth Mollel naziunganisha hapa maana badala ya kuipa kambi ya upinzani nguvu, mnawaongezea ccm nguvu.
2. Mlichomfanyia Mtatiro. Kitendo cha Anatropia kuanza kampeni wakati kam ukawa mlisha mkabidhi jimbo mtatiro, ni usanii wa hali ya juu wa mbowe. Mlikuwa na nguvu ya kuzuia mapema. sasa jimbo liko ccm kwa uroho wenu halafu bado huyo Anatropia mmempa ubunge. Mimi hapana.
Kumbukeni, usaliti ni mbaya mno. Zzk na wenzake mliamua kuwatosa kwa sababu ya usaliti, lkn leo hii mnaamua kuwakumbatia wasaliti mkiwaacha watu hodari tena mkipuuza maoni ya viongozi wa wilaya, dhambi hiyo nanyi itawatafuna.
niishie hapa.