CHADEMA: Watanzania puuzeni propaganda za udini...

only83

JF-Expert Member
Oct 15, 2010
5,343
2,525
Wabunge wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) wamewataka Watanzania kuondokana na propaganda zinazoenezwa na baadhi ya watu kwamba chama hicho ni cha waumini wa dini fulani na kwamba wanaoeneza uvumi huo wana ajenda yao ya kutaka kukidhoofisha kisiasa.

Wabunge hao wa viti maalum Suzan Lyimo, Grace Kihwelu na Mjumbe wa Kamati Kuu ya chama hicho, Hajjat Shida Salum walitoa kauli hiyo juzi wakati wa futari iliyoandaliwa kufuturisha wananchi wa jJiji la Dar es Salaam katika hafla iliyofanyika makao makuu ya chama hicho Kinondoni.

Kihwelu alisema Chadema ni chama cha watu wote na wala hakina uhusiano na dhehebu la dini fulani na ndiyo maana hata katika safu ya uongozi wa juu chama hicho nafasi zote nyeti zimeshikwa kwa idadi sawa kati ya Waislamu na Wakristo.

Kuhusu sensa, alisema viongozi wa dini waendelee kuwahamasisha waumini wao ili wajitokeze kwa ajili ya kushiriki zoezi hilo kwani ni jambo muhimu litakaloiwezesha nchi kuweka vizuri mipango yake ya maendeleo.

Kwa upande wake Lyimo alisema Chadema siyo chama cha kidini na kwamba wanaoeneza madai hayo wana ajenda yao binafsi hasa kutokana na chama hicho kuendelea kuungwa kwa kasi kubwa na Watanzania wengi.

Alisema ni jambo la ajabu katika karne hii kuna baadhi ya watu wanazungumzia suala la udini ambalo lilikuwa linapigwa vita na muasisi wa Taifa hili, Hayati Mwalimu Julius Nyerere.

Akizungumzia suala la sensa, alisema hakuna sababu kwa serikali kuogopa kuweka dodoso za la dini kwa kuwa siyo jambo baya kufahamu idadi ya Waislamu na Wakristo.

Naye Mjumbe Shida Salum ambaye pia ni mama mzazi wa Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe, alisema chama hicho kamwe hakitaruhusu suala la udini lijipenyeze kwasababu kilianzishwa kwa malengo ya kuwakomboa Watanzania wa aina zote bila kujali dini au makabila yao.

Hajat Shida aliwataka wananchi waendelee kukiuka mkono chama hicho ambacho kimekuwa pekee chenye mwelekeo wa kuwakombo kuelekea katika harakati za kupata maendeleo.

CHANZO: NIPASHE
 
CDM si ipuuze tu hizo tuhuma. Kuzijibu ni kujitetea. Kama hazipo zitaisha tu kimya kimya haina haja ya kuziongelea kwa kuzikanusha.
 
Kwenye timu nzima ya CDM kuna waislamu wangapi? Msitake kujisafisha na hicho kifutari njaa, CCM pekee ndio sio wadini lakini nyie ni wadini wakubwa, halafu kuna wachaga wangapi kwenye chama?
 
Kwenye timu nzima ya CDM kuna waislamu wangapi? Msitake kujisafisha na hicho kifutari njaa, CCM pekee ndio sio wadini lakini nyie ni wadini wakubwa, halafu kuna wachaga wangapi kwenye chama?

ccm mdini namba moja. Watanzania tulishawabaini
 
Ufafanuzi mzuri ila ukisema hata viongozi kitaifa kuna usawa kwa Dini hilo nalo kwangu ni Udini hutakiwa kuangalia ulinganifu ndipo usemee kuna udini au lah ila tu kwa kufuata misingi ya Haki na utendaji usiobagua ndipo tutafuta hiki kidudu dini. Peoplesssss power.

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Duh! kwa hiyo waliona futari wasitoe bure wakakandamiza na kamstari ka M4C ,Udini :eek2: ??? " action speaks louder than words"
 
Hakuna udini CDM

Ya wezekana hakuna udini lakini kwa kuwa cdm wanashida y madaraka, wako radhi kutumia njia yoyote kutimiza azima hiyo. Mathalani, kwa mujibu wa acc za CDM, wanatumia hela nyingi sana kuwahonga viongozi wa dini na makundi ambayo wanaamini kuwa yana wafuasi wengi, jina la misaada.
 
Hakuna udini CDM

Kweli kabisa CDM hakuna udini Mkuu ila mbona migomo yote chadema wanaiunga mkono kasoro tu huu wa WAISLAM? Vp na kale kakauli cha Mch Msigwa? Halafu mkuu samahani nauliza Kwan Nassar alichaguliwa na Kanisa Pekee? Iweje arudi kanisani kutoa Shukran bila ya kwenda na sehemu nyingine? Haha Mkuu na vp kale kakauli cha MTEI kuhusu Tume ya Katiba?

KWELI KABISA MKUU CHADEMA SIO WADINI NAKUBALIANA NAWEWE 100%
 
Kwenye timu nzima ya CDM kuna waislamu wangapi? Msitake kujisafisha na hicho kifutari njaa, CCM pekee ndio sio wadini lakini nyie ni wadini wakubwa, halafu kuna wachaga wangapi kwenye chama?

AKILI ZA KUAMBIWA NA MASHEIKH HIZI... Acha kukurupuka

  1. Chama tawala Tanzania ni CCM na mwenyekiti wake ni Muislaam,
  2. Tanzania tunao Raisi wawili na wote ni Waislaam.
  3. Anayeunda serikali na kuiongoza ni Muislaam
  4. Anayewateua watendaji wakuu pamoja na Waziri Mkuu ni Muislaam.
  5. Tanzania tunao Makamu wa Raisi watatu na wote ni Waislaam.
  6. Jemadari Mkuu wa majeshi Tanzania ni Muislaam.
  7. Mkuu wa polisi Tanzania ni Muislaam.
  8. Mkuu wa Usalama wa Taifa ni Muislaam.
  9. Mkuu wa Mahakama Tanzania ni Muislaam.
  10. Ardhi yote ya Tanzania ni mali ya serikali inayoongozwa na Muislaam.
 
Nassari alisimama kanisani kumshuru Mungu wake,je ulitaka aingie msikitini? Wananch wote aliwashukuru jukwaani, special thanx kwa Mungu lazma aingie kanisani! UNAKUMBUKA TUSKER PROJECT FIRM 5? Huyu dada mshnd,RUTH MATETE amechukua kitika toka kwenye hela ya ushindi akapeleka kanisani km special thanx kwa Mungu,je alipigiwa kura na wakiristo pekee? Au mama anapopeleka kichanga chake kanisani kumshukuru Mungu,je ina maanisha hosp alihudumiwa na wauguz na madr wakiristo tu? Acheni propoganda!
 
hawa jamaa cjui wakoje bwn, wanaposema idara nyeti znaongozwa na wakiristo cjui tuwaeleweje? Hao waliotajwa hapo juu ni wakiristo? Je uislam au ukiristo ndo utakupeleka mbinguni pasipo matendo?
 
Nassari alisimama kanisani kumshuru Mungu wake,je ulitaka aingie msikitini? Wananch wote aliwashukuru jukwaani, special thanx kwa Mungu lazma aingie kanisani! UNAKUMBUKA TUSKER PROJECT FIRM 5? Huyu dada mshnd,RUTH MATETE amechukua kitika toka kwenye hela ya ushindi akapeleka kanisani km special thanx kwa Mungu,je alipigiwa kura na wakiristo pekee? Au mama anapopeleka kichanga chake kanisani kumshukuru Mungu,je ina maanisha hosp alihudumiwa na wauguz na madr wakiristo tu? Acheni propoganda!

Mkuu hawa Wenzetu Tatizo ni SHULE.. Wangekuwa wanaipa elimu kipaumbele Wangekuwa wanafikiria sawasawa na mara mbili mbili
 
Tena Pro-chadema hapa JF ndiuyo hawana udini kabisaaa wanaheshimu dini zote!!!safi sana chadema!!!
 
Kwenye timu nzima ya CDM kuna waislamu wangapi? Msitake kujisafisha na hicho kifutari njaa, CCM pekee ndio sio wadini lakini nyie ni wadini wakubwa, halafu kuna wachaga wangapi kwenye chama?

Mi na bold tu mkuu usomeke vizuri, hata asiyetaka kukusoma akusome
 
Tena Pro-chadema hapa JF ndiuyo hawana udini kabisaaa wanaheshimu dini zote!!!safi sana chadema!!!

Mkuu si kweli ebu cheki comments za mwana cdm mmoja humu ambaye avatar yake ni kipete chenye sanam ya mtu katundikwa kwenye +, na mwingine avatar yake ni picha ya kitoto kimejichokea kimeshika tama nyuma yake kuna bendera ya cdm ....then uje uthibitishe kauli yako.
 
Mkuu hawa Wenzetu Tatizo ni SHULE.. Wangekuwa wanaipa elimu kipaumbele Wangekuwa wanafikiria sawasawa na mara mbili mbili

Mkuu hizi kauli zenu za kejeli na matusi huenda zinachangia sana kuvumisha hili jambo.Wenzenu wanaobserve hizi comments zenu then wanaconclude hisia zenu dhidi yao,hata siku moja hawatawaunga mkono,hebu tubadilike maana unaidhoofisha CDM kwa kauli kama hizi bila kujijua.
 
Mkuu si kweli ebu cheki comments za mwana cdm mmoja humu ambaye avatar yake ni kipete chenye sanam ya mtu katundikwa kwenye +, na mwingine avatar yake ni picha ya kitoto kimejichokea kimeshika tama nyuma yake kuna bendera ya cdm ....then uje uthibitishe kauli yako.
Mkuu lilikuwa fumbo hilo hawa wanajulikana sana humu !hawa pro chadema hapa JF ndiye wadini wakubwa wana kejeli Waislam sana hapa JF mara ooh hawajaenda shule,wala ubwawa, nk nk sasa sijui hawa amabo hawajenda shule au wala ubwabwa hawapigi kura?

Nilisha eleza kwenye thread nyingine kuwa kuna viongozi wengi wakuu wa chadema wana pita humu lakini hakuna hata mmoja wao amejaribu kukumea hizi dharau na dhihaka wanazo zifanya hawa wanachadema hapa JF,wakielezwa wadini chama chao kina dhihaki Waislam wanasema hizo propaganda za CCM,mwenye macho haambiwi ona , kejeli zote wanazo zifanya wanachadema hapa JF kwa Waislaam.

Hili halina mjadala Chadema waliyo wengi wana chuki sana na Waislam na Uislam mfano halisi unaanzia hapa JF tena si ajabu wengine wanajulikana wanajificha wanaona waelezee hisia zao hapa JF,lakini yule mchungaji mbunge wa Iringa ameshajiweka hadaharani kuwa yeye ni ant-Islam,

Hivi Mie siwaelewi hawa Chadema na haswa hawa wa JF hivi kama mna ndoto ya kutawala Tanzania hivi kwa akili yenu mtaweza kuwatawala bila ushirikiano wa Waislaam?

Hata kama mnadhani Waislaam, wapo minority nchini unafikiri uchache wao itawapa amani?Angalieni Waislam wapo minority nchi nyingi kwa mfano India kuna wakati kulikuwa na vita vikubwa kati ya Waislam na Wahindu,Phillipines,Burma,kuna kipindi huko Trinadan na Tobago Waislam waliteka bunge nzima kwa bunduki zote hizi choko choko za kidini.

Hivi nyie pro-chadema mliopo hapa JF wabaya wenu waamue kuanika hizi kejeli zenu kwa waislam wa kawaida waliopo huko mitaani mnadhani chama chenu kitajengeka?

Hizo kejeli zenu mnazo Wafanyia Waislaam CCM wanazipenda sana wanajua mnajikaanga kwa mafuta yenu wenyewe hamuwapi tabu za kuwamiliza mnajimaliza wenyewe.

Msijidanganye hata kidogo ya kuwa hiyo mikutano ya hadhara na watu wanaokuja kwenye mikutano ndiye ushindi wenu hao sio wapiga kura pekee kuna mamilioni ya wapiga kura ambao hawaji kwenye mikutano yenu ambao wapo mitaani na majumbani mwao ambao wengine mnawa kejeli na kuwadhihaki dini yao!

TIme will tell!Pro-Chadema mliopo hapa JF mnahitaji kujirekebisha kama mwakipenda chama chenu kama ni kweli nyie wafuasi wa ukweli wa chadema unless nyie mashabiki tu!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom