Siasa za Tanzania ni vulugu tupu. Ni hatari sana pale ubinafsi unapotangulizwa mbele katika kutoa huduma za msingi za kijamii.
Mtu akiangalia kutokea dirishani, hawezi kufahamu chanzo cha tatizo hili mpaka aingie ndani ya nyumba.
Hili vulugu na bifu la Makamba's na Sherukindo's kutoa kwenye msuguano wa ubunge linasababisha mpaka huduma ambazo zilikuwa zipatikane kwa wananchi zinakuwa hazipo au aghari kutegemea nani na yuko upande upi wa msuguano.
Kama ilivyo kwa wahariri wa Tanzania, ukifuatilia hata sababu ya gazeti la Nipashe kushupalia habari hii, lazima kutakuwa na maslahi binafsi kwa upande umoja.
Kama tujuavyo, tembo wakipigana, zinazoumia ni nyasi. Wananchi kwa sasa wanaumia kwa sababu ya ubinafsi wa hawa wanasiasa.
Huwezi kumkuta Sherukindo & co kapanda mahakamani au Makamba & co kupanda mahakamani bali watakaosota mahakamani na mahabusu ni walalahoi ambao wengi wao hawajui chanzo cha msingi cha huu mgogoro.
Ikumbukwe Sherukindo ndiye aliyebwagwa kwenye ubunge na Makamba Jr na sasa Sherukindo ni Mwenyekiti wa Umoja wa Wakulima wa Chai wa Usambara (UTEGA) ambapo kwa upande mmoja, amebeba lungu la kumpiga Makamba Jr kisiasa.
Ama kweli siasa za Tanzania siyo za wapita njia kama mimi.