CHADEMA wataka Makamba akamatwe kuhusiana na uchochezi wa sakata la UTEGA.

Ng'wamapalala

JF-Expert Member
Jun 9, 2011
6,808
6,500
Sakata la kikundi cha ushirika wa wakulima wa chai wa Jimbo la Bumbuli wilayani Lushoto Mkoa wa Tanga limeingia sura mpya baada ya watu mbalimbali kuunga mkono Mbunge wa Jimbo hilo, January Makamba afikishwe mahakamani kwa kuchochea uasi.

Wametaka serikali kumvua unaibu waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknorojia kwa kuwa kitendo hicho ni cha udhalirishaji wa serikali, jamii ya Watanzania na nchi kwa ujumla.

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimeeleza kusikitishwa na tukio hilo na kuitaka serikali itoe tamko haraka iwezekanavyo ili kurejesha hali ya amani badala ya hatari iliyotangazwa na baadhi ya watu wakiongozwa na mbunge wa jimbo hilo.

Ofisa wa chama hicho mkoa, Jonathan Bahweje, alisema kuwa kutokana na matokeo ya vurugu hizo zilizodaiwa kuchochewa na kiongozi huyo, Chadema inaunga mkono bodi ya UTEGA kutaka kumfikisha mahakamani mbunge huyo pamoja na kuitaka serikali ichukue hatua kali ikiwa ni pamoja na kumuondoa kwenye orodha yake ya manaibu waziri ili kulinda heshima ya nchi.

Bahweje ambaye pia ni mwanaharakati wa haki za binadamu ametoa siku saba kwa serikali kuhakikisha uasi huo unazimwa na shughuli kiwandani hapo kuendelea ili kumpunguzia hasara zisizo na ulazima mwekezaji huyo na siku 14 nyingine za kumchukulia hatua Makamba.

Alisema yeye kwa niaba ya chama Mkoa wa Tanga wanalaani vitendo vya kufungiwa nje kwa kufuli walinzi wa kiwanda hicho waliopo wawapo ndani ya kiwanda watu wanaojiita wawakilishi wa wakulima na kwamba hatua hiyo ni ukatiri na ni hatari na ukiukwaji mkubwa wa haki za binaadamu.

Alieleza kuwa kwa kuwa matukio yote ya kihalifu yanayofanywa na wakulima hao yanaelezwa kuwa ni utekelezaji wa maazimio ya mkutano baina yao na mbunge huyo ni wazi kuwa serikali imehusika na vurugu hizo na ili kujisafisha ni kumuwajibisha Makamba aliyeuitisha.

"Huyu bwana kwanza ni mvunjaji mkubwa wa demokrasia…ameshawahi kumhujumu aliyekuwa mwenyekiti wa serikali ya Kwekitui kwa tiketi ya Chadema ambaye alitoroka siku mbili tu baada ya Mbunge huyo kufanya ziara kijijini hapo…hii ni hujuma, hafai mtu huyu," alisema Bahweje.

Wakizungumza na NIPASHE kwa nyakati tofauti baadhi ya wakulima wa chai walisema kuwa hakuna ubishi juu ya uvurugu zinzoendelea baina ya muwekezaji wa kiwanda cha chai Mponde na wakulima zimebuniwa na Mbunge wa Jimbo hilo, January Makamba.

Baadhi ya wananchi ambao ni wakulima wa zao la chai Jimbo la Bumbuli, walidai kuwa chimbuko la mgogoro huo ni kutokana na masuala ya kisiasa na kwamba hauna tija yoyote.

Wakulima hao ambao ni wapigakura wa Makamba ambao walionekana kumgeuka, walieleza kuwa vurugu hizo zinawaathiri kwa kiwango kikubwa na kwamba wanalazimika kula mlo mmoja kwa siku baada ya kiwanda kuzuiwa kufanyakazi.

Walidai kuwa sababu ya vurugu hizo ni kutokana na mbunge huyo kutaka kuhakikisha kuwa sehemu zote muhimu anaweka wapambe wake ili kujiweka vizuri kwenye uchaguzi mkuu ujao.

Kwa hisani ya Nipashe.

Nipashe walileta habari nyingine pia ambayo inapatikana hapa,
http://www.ippmedia.com/frontend/index.php?l=55571
 
Siasa za Tanzania ni vulugu tupu. Ni hatari sana pale ubinafsi unapotangulizwa mbele katika kutoa huduma za msingi za kijamii.

Mtu akiangalia kutokea dirishani, hawezi kufahamu chanzo cha tatizo hili mpaka aingie ndani ya nyumba.

Hili vulugu na bifu la Makamba's na Sherukindo's kutoa kwenye msuguano wa ubunge linasababisha mpaka huduma ambazo zilikuwa zipatikane kwa wananchi zinakuwa hazipo au aghari kutegemea nani na yuko upande upi wa msuguano.

Kama ilivyo kwa wahariri wa Tanzania, ukifuatilia hata sababu ya gazeti la Nipashe kushupalia habari hii, lazima kutakuwa na maslahi binafsi kwa upande umoja.

Kama tujuavyo, tembo wakipigana, zinazoumia ni nyasi. Wananchi kwa sasa wanaumia kwa sababu ya ubinafsi wa hawa wanasiasa.

Huwezi kumkuta Sherukindo & co kapanda mahakamani au Makamba & co kupanda mahakamani bali watakaosota mahakamani na mahabusu ni walalahoi ambao wengi wao hawajui chanzo cha msingi cha huu mgogoro.

Ikumbukwe Sherukindo ndiye aliyebwagwa kwenye ubunge na Makamba Jr na sasa Sherukindo ni Mwenyekiti wa Umoja wa Wakulima wa Chai wa Usambara (UTEGA) ambapo kwa upande mmoja, amebeba lungu la kumpiga Makamba Jr kisiasa.

Ama kweli siasa za Tanzania siyo za wapita njia kama mimi.
 
Kama ilivyo kwa wahariri wa Tanzania, ukifuatilia hata sababu ya gazeti la Nipashe kushupalia habari hii, lazima kutakuwa na maslahi binafsi kwa upande umoja.

Hapo umenena! Gazeti la Nipashe na huyu Mwandishi inaelekea wana lao hapa. Habari hii sio tu ni ya kuokoteza maneno ya mitaani, ni wazi ina nia ya kuchonganisha wana CCM Bumbuli kwavile haipo balanced kabisa.

Kwanini Nipashe haielezei historia nzima ya tatizo la chai Bumbuli ambalo halikuanza leo wala jana? Matatizo ya kiwanda hichi hayakuja na January Makamba. Uongozi mbovu wa kiwanda kwa miaka mingi sasa na kutowalipa wakulima stahiki zao ndio chanzo kikuu.

Nilipata kusoma maelezo ya January Makamba kwenye Facebook yake kuhusu hili jambo - kwamba wananchi walishachoka kunyanyaswa na wala hawakushurutishwa "kuasi". Ni kwamba Mbunge mwenyewe alishindwa kuzuia uamuzi ambao wananchi wenyewe walichukua. Alisema kwa mara ya kwanza aliona "people's power" aliyokuwa anaisikia, kwahiyo ilibidi asimame na kufanya jitihada ya kuwatuliza wasifanye kakubwa zaidi. Wananchi walidai watalinda mali yao (yaani kiwanda) sio kweli kwamba kulitokea uharibifu wa mali na polisi walidhibitisha hili halikutokea. Ni gari moja tu lenye mzigo wa chai lililokuwa linaelekea kiwandani ambalo lilizuiliwa na wananchi na chai kumwagwa.

Mwisho wa siku tukisikia January Makamba na Mzee Shelukindo wamepatana na wanaelewana, sijui CHADEMA watatumia mbinu gani kuwagawa wana CCM Bumbuli? Hizi mbinu hazina mshiko. Wajipange vizuri katika majimbo mengine, labda watakuwa na nafasi huko, lakini Bumbuli wanapoteza muda wao. Makamba anakubalika sana.
 
Mwaka umepita sasa, wakulima hali mbaya Kiwanda bado kimefungwa wakulima wanahangaika umaskini umetamalaki. Mh Makamba unataka uraisi wakati changamoto za jimboni zinakushinda?
 
Mh Makamba usipojiangalia hii ishu ya kuwaingiza kingi wananchi wa Bumbuli itakunyima uraisi, haiwezekani chai inaharibika wananchi hali mbaya mbunge upo upo tu bila kuonyesha leadership yoyote.
 
Mh Makamba usipojiangalia hii ishu ya kuwaingiza kingi wananchi wa Bumbuli itakunyima uraisi, haiwezekani chai inaharibika wananchi hali mbaya mbunge upo upo tu bila kuonyesha leadership yoyote.

kijana unauwakika na unachokisema?bumbuli hakuna mgogolo wowote kwa sasa kama wanavyo dai wengine,ni chadema tu wanataka kumuaribia kijana wa watu status yake kwa jamii.
 
kijana unauwakika na unachokisema?bumbuli hakuna mgogolo wowote kwa sasa kama wanavyo dai wengine,ni chadema tu wanataka kumuaribia kijana wa watu status yake kwa jamii.
Hakuna mgogoro wa wanasiasa ila wananchi hawana sehemu ya kuuza chai baada ya huo mgogoro kusababisha kiwanda cha chai kufungwa zaidi ya mwaka sasa. Makamba aliongoza kufunga kiwanda but anashindwa kukifungua
 
tatizo lililopo ni muwekezaji mwenye kushindwa kukiendesha kiwanda wala si tatizo la january wala sherukindo,january alicho kifanya ni kutetea tu masilai ya wakulima hasa ktk manunuzi.
 
Back
Top Bottom