CHADEMA watafute mbinu nyingine kwani mbinu hii ya kuwachafua ma Dc imeshajulikana na itawapotezea

singidadodoma

JF-Expert Member
Nov 11, 2013
4,394
1,536
mahakama ya kadhi


MBINU CHAFU ZA UKAWA KUHUJUMU WAKUU WA WILAYA ZAFICHUKA.

Siku chache zilizopita kumetokea tabia ya kushambuliwa kwa maneno kwa baadhi ya wakuu wa wilaya kupitia vyombo vya habari ikiwemo magazeti yakionesha picha mbalimbali za wakuu wa wilaya na kuwakejeli, lakini pia baadhi ya wabunge na mameya na viongozi wengine wamekuwa wakionekana kuwakshfu na kuwadhalilisha wakuu wa wilaya. Hali hii ilishika kasi baada ya Rais kuonesha dalili za kuteuwa wakuu wa wilaya hivi karibuni. Wakuu wa wilaya kikatiba ni wawakilishi wa rais kwa ngazi ya wilaya na ndio wenyeviti wa usalama wa wilaya, kifupi ndio viongozi wakuu ngazi ya wilaya.

Katika uchunguzi uliofanyika wakuu wa wilaya wanaoandamwa sana ni Mh. Paul Makonda (Kinondoni) na Mh. Peter Kasesela (Iringa). Wiki iliyopita mbunge wa iringa Mh. Msigwa (CHADEMA) ameonekana akimkashfu mkuu wa wilaya kwa maelezo kuwa anaingilia kazi zake, lakini pia siku chache baada ya msigwa kumkashfu mkuu wa wilaya, tumemsikia pia meya wa Kinondoni Boniface Jacob (CHADEMA) akimkashfu mkuu wa wilaya kwa maelezo yale yale kwamba anaingilia majukumu yake.

Swali la kujiuliza;

kwanini wanaowakashfu wakuu wa wilaya wawe viongozi wa CHADEMA TU? Na pia kwanini waje na sababu moja tu ya kuingiliwa majukumu yao?? Je hapo mwanzo walikuwa hawaingiliwi majukumu yao?? Pia kwanini wale wakuu wa wilaya wanaoonekana wanawajibika sana na kuendana na kasi ya Rais ndio wanaoandamwa?? Je hakuna agenda ya siri hapa kwa Ukawa juu ya serikari ya awamu ya Tano?? Je, hii sio hasira ya uchaguzi baada ya CCM kushinda na UKAWA kushindwa?? Katika uchunguzi wa kina wa wachambuzi mbalimbali wa masuala ya kisiasa wameonesha kuwa hali hii inatokana na CHADEMA kukosa mbinu mbadala ya kukubalika tena kisiasa na hii imetokana na Rais Magufuli kukubalika sana kwa jamii kuliko mwanasiasa yeyote katika kipindi hichi, hali inayowatisha UKAWA kuwa wanaweza poteza ushawishi wa kisiasa na kushindwa vibaya uchaguzi ujao 2020. Lakini pia imegundulika kuwa UKAWA wamekutana katika vikao vya siri chini ya Mwenyekiti wao Mh. Freeman Mbowe na kukubalina kutumia mbinu hii ya kuwashughulikia wakuu wa wilaya ili kudhoofisha serikali ya awamu ya tano, hali hii imethibitika pale viongozi wa Ukawa wakianza ziara za kimya kimya mikoani kuanzia wiki iliyopita ili kuwachafua viongozi ngazi za wilaya. Juzi tu Mwenyekiti wa Chadema alienda Bukoba nako alianza kukosoa utendaji wa mkuu wa wilaya na wakurugenzi na kuonesha hawafai akishirikiana na Mbunge wa Bukoba Mh. Rwakatale.Huu ndio mkakati walionao sasa UKAWA juu ya serikali ya awamu ya Tano.

Rai yangu;

Chadema watafute mbinu nyingine kwani mbinu hii imeshajulikana na itawapotezea kabisa nguvu ya kisiasa kwa viongozi wao waliobahatika kupata nafasi mbalimbali ikiwemo ubunge na umeya. Pia Chadema watambue kuwa siasa ya kusubili makosa ya mwingine upate umaarufu imepitwa na wakati, wasipolijua hilo watapotea kabisa kama TLP.

Pia , wakuu wa wilaya wasikatishwe tamaa na maneno ya wakosoaji, kwani ukiona watu wanakusema sana ujue wanatambua mchango wako, kwa hiyo wanachotakiwa kukifanya ni kusimamia ilani waliyopewa ya CCM ambayo ndio anayoisimamia Rais Magufuli na lazima wajue wanatakiwa waendane na kasi ya Rais ili wasije kuwa mizigo kwa serikali hii.

Mwisho;

Siasa sio uadui , tusitumie siasa kubomoa nchi yetu kwani hakuna haja ya kugombania fito wakati tunajenga nyumba moja. Tusitafute sifa nyepesi kwa kutumia kashfa kwa viongozi wengine, zama hizo zishapita, sasa kazi zako na uwezo wako kuwatumikia wananchi ndio utakubeba sio matusi na kejeli.

Mwanahalisi forum
 
Chadema wamebakia kuimba nyimbo ya Katiba mpya as if ikiletwa leo, kesho watanzania wataamka na mapesa chini ya vitanda vyao...
 
Wakuu wa wilaya hawana kazi bora hicho cheo kifutwe wakurugenzi wanatosha
 
Akiwa mbovu asisemwe? huyo Makonda unamwaona je wewe kwa akili zako.
 
Waache watapetape
Walikuwa na ajenda ya Zanzibari sasa imebuma
Wanatafuta wapi wapatie kick
 
Haya wahini fasta kupokea posho zenu. Mngekuwa mnapokea mishahara tungeomba mkatwe kodi.
 
Kasi ambayo ina madhara moja kwa moja kwa mwananchi ni kupanda kwa bei ya bidhaa kama sukari na umeme
 
Huku Arusha hata siwasikii tena....

Na kesho tunachagua mwenyekiti Wa ccm na katibu mwenezi mkoa Wa ARUSHA...
 
Hawa wakuu wa wilaya huwa wanapenda ubabe na dharau kisa wanauwezo wa kuamrisha polisi. Kumbuka yule aliyechapa walimu...haiwezekani,lazima wafanye kazi yao tena kwa nidhamu lasivyo ugomvi hautokwisha.
Kwanini umdhalilishe kiongozi/mtu kisa cheo? Tusitetee mambo yahovyo,demokrasia ni kufanyakazi kwa hekima na busara sio vitisho
 
Sina uhakika na suala la Kama wanatafuta kick. Utafiti huo umefanywa na nani Mkuu. Naona Kama ni muendelezo wa kupinga tuhuma zaidi ya kuuita utafiti
 
Hii kasi ya kuanzisha post za kuichafua chaedema tangu JK akumbushie zile nafasi 46 mmepagawa kweli kweli mnasahau hata kuongelea ya chama chenu mmebaki na ya jirani, kweli ahadi hii itawatoa nnya.
 
hahaha naona vijana wa lumumba mmekazana kuhangaika na ukawa kisa naona ni ile kauli ya kaka yenu kuwa magufuli awakumbuke kwasababu mliisaidia sana ccm kurudi madarakani... mnakazi a kuanzisha mauzi ya kimaandazi,,, mda wote huyu magu

sidhani kama hata anajua mambo ya mitandao ... msipoteze mb zenu buree katafteni kazi mfanye kama ikibidi muwape wake zenu mimba ,ama mpewe mimba mzae kwa wingi kwa sasa elimu ni bure japo nyie mmeikosa wanenu wataipata
mzee wa ekotike hatunaye tena.... acheni kuhangaika na ukawa
 
Back
Top Bottom