CHADEMA washindwa kulipa kodi ya nyumba, wafukuzwa ofisini!

Hivi huyu jamaa ilikuwaje hadi akapewa nafasi ya kugombea ubunge?
Kwa upeo wake hakustahili hata kugombea umonita wa darasa.
 
Mapenzi ya chama yakipitiliza yanakuwa mabaya sana,naona kila mwanachadema anatoa matusi tuh badala ya kujadili kama hilo ni la kweli ama la?tujiulize ni kwanin wamefeli kulipia hiyo kodi hali ya kuwa kila siku wakija kwenye mikutano tunawachangia pesa.jumlisha na ruzuku pia,sasa badala ya kuhoji uhalisia,tunamtukana mtoa mada kisa alishakwenda kwa mafisadi,sawa tunajua mtoa mada ni mchumia tumbo lakin je mada yenyewe ina uhalisia au haina uhalisia?
kama tukishajitosheleza kuwa ni propaganda kisha tumpuuze na kumdharau,ila kama ni uhalisia ipo haja ya kufikiri mara mbili mbili
 
kweli umeishiwa hoja, hivi ukiwa CCM unaambukizwa kuropoka na kutokuwa na hoja.
 
Inawezekana ruzuku nyingi zinatumika zaidi kuandaa mandamano na kuwanunua wanahabari ili wawaandike vizuri.
 
Ruziku ya wilaya ya kanda ya kaskazini,ni mara mbili ya mkoa mzima wa kanda zingine.
 
Ruzuku ya wilaya ya kanda ya kaskazini CHADEMA ni mara mbili ya mkoa mzima wa kanda zingine.
 
Hvi zilew Mil 3,265,700/= walizochangisha hapa Mbeya wakati Mbowe amekuja zimepelekwa wapi na zimefanya kazi gani?
Hakika wajinga ndio waliowao na kamchezo ka KEKUNDU!
 
Umbea umbea na vijembe ni tabia z kike ikitokea kwa upande wa kiume kuna hatar ya kupigwa kabaang,nenda lumumba ukatiwe fungu lako,nakupa siku 21 lazima ufumuliwe rinda na kinana
 
Nikiachana na mleta mada kama yeye binafsi, ni lazima viongozi wa mkoa wawajibike kupanga namna ya kupata fedha kwani ni aibu kwa hadhi ya mkoa kushindwa kulipia kiwango kidogo kama hicho.
 
Mwampamba, hulali unaiwaza CDM tu? Pole sana inaelekea ulikuwa unaipenda sana. Hata kwenye ndoa mambo haya hutokea. Mke anampenda sana mume wake lakini anatokea mlaghai na kumrubuni, matokeo yake anajuta kila siku na anatamani kurudi kwa mume lakini ndo haiwezekani tena. Vumilia tu huko uliko, maisha popote.
 
Anajishughulisha na nini jamani? Maana wewe na Shonza mmezusha mtafaruku kwa CCM vijana original wanaona meenda kuwazibia rizki

After all's being said and done, CHADEMA lipeni pango!
 
Kwanza kabisa napenda kutoa pole nyingi sana kwa watanzania wenzetu_wanaArusha kwa tukio lililowapata la kulipuliwa kanisa.Tuombe mungu,tudumishe amani na upendo miongoni mwetu.

Watanzania ni vigumu sana mchungaji/padri/sheikh kuhubiri neno la mungu bila kumtaja shetani.Chadema wanapokea ruzuku kutoka serikalini ambayo ni kodi ya watanzania wanyonge zaidi ya Milioni 300 kila mwezi.

CHADEMA WASHINDWA KULIPA KODI YA NYUMBA WAFUKUZWA OFISINI!!

*KISA DENI LA SH. 360,000 TU ZA PANGO!


DK, SLAA
MBEYA, Tanzania.
OFISI ya CHADEMA mkoa wa Mbeya, iliyopo eneo la Forest jijini hapa, imefungwa kutokana na Chama hicho kushindwa kulipa sh. 360,000 za deni la pango kwa muda mrefu sasa.

Imeelezwa kwamba mkataba wa awali wa CHADEMA, ulimalizika tangu mwezi Desemba mwaka jana, na jitihada za mmiliki wa chumba hicho, Eden Katininda, za kufuatilia malipo hadi sasa zimegonga mwamba.

Akizungumza leo Katininda amesema kabla ya kuchukua hatua za kufunga kufuli lake juu la lile la lilofungwa na CHADEMA, wiki mbili zilizopita alifanya jitihada kubwa za kudai deni lake bila mafanikio kutokana na uongozi kumpiga chenga.

Katininda alisema hata Katibu mkuu wa CHADEMA, Dk.Willbrod Slaa, alipofanya ziara yake mkoani Mbeya, hivi karibuni alikuwa tayari amefunga ofisi hiyo, na kuwa inaonyesha kiongozi huyo alipokelewa katika ofisi ya wilaya badala ya ile ya mkoa.

Kwa mujibu wa Katininda, aliwasiliana na Mwenyekiti wa chama hicho, mkoani hapa aliyemtaja kwa jina moja la Mwamboneke, wabunge David Silinde (Mbozi Magharibi) na yule wa viti maalum, Naomi Kaihula, lakini wote wamekuwa wanamzungusha.

Aliongeza alipomfuata mbunge Silinde na kumueleza kuhusu madai hayo, alimjibu asihofu kwani mara atakapofika Bungeni mjini Dodoma, atamtumia fedha hizo lakini kila akimpigia huwa hataki kupokea simu yake.

Alisema kwa upande wa mbunge viti maalumu wa CHADEMA, mkoani hapa Naomi, naye alimueleza kuhusu deni hilo, lakini alimjibu kuwa yeye hahusiki hivyo mmiliki (Katininda), awafuate aliowapangisha.

"Baada ya kuona napigwa chenga za mwili kiasi hiki, nilijaribu kuwasiliana na Dk.Slaa kwa simu yake ya mkononi, lakini naye hakupokea simu licha ya kujaribu mara kadhaa, ilikuwa inaita tu mpaka inakatika bila kupokelewa, hivyo ndipo nilipofikia uamuzi wa kufunga kufuli lingine juu ya lile la CHADEMA”, amesema Katininda.






Kwa akili hii si bure wewe unaweza kuwa mnazi hakika acha wengine nao wasema .Hivi kodi hoyo na maisha ya watanzania kuna mahusiano ? Mbona nasikia mwenye pango kakatazwa na serikali na ndiyo kampeni zenu za kuja na habari uchwara ?CCM wanadaiwa mangapi hadi roho za watanzania ?
 
pili pili usiyokula yakuwashia nini! uliamua mwenyewe kwa njaa zako kuondoka cdm, lakini kila ukiamka, ukiwaza ni cdm hivi cdm vile, labda nikuulize swali dogo ndugu Mtela Mwampamba ni jambo gani la maendeleo umewahi kufanya ndani ya ccm na ukastahili pongezi?
 
Last edited by a moderator:

Similar Discussions

Back
Top Bottom