PreGE2025 CHADEMA warudisheni wabunge 19 mjenge Chama

PreGE2025 CHADEMA warudisheni wabunge 19 mjenge Chama

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Chadema muwe waangalifu na hao wanayotaka kurudi chama I, wengi wao wakisema wakina Mdee na kundi lake ni hatari kwa ustawi wa chama kwani wote ni mapandikizi ya ccm!! Akieemo huyo mzee anaitwa Shibuda!!
Ni lazima kuwa huja vizuri ; ccm inawapa Gia debe covid 19 muwarudishe ili wako hukumu chama!!
Uko sahihi kabisa.
 
Chadema muwe waangalifu na hao wanaotaka kurudi chamani wengi wao wakiwemo wakina Mdee na kundi lake ni hatari kwa ustawi wa chama kwani wote ni mapandikizi ya ccm!! Akiwemo huyo mzee anaitwa Shibuda!!
Ni lazima kuwachuja vizuri ; ccm inawapigia debe covid 19 muwarudishe ili waje kuhujumu chama!! Chonde chonde msiingie kwenye mtego wa ccm.
Hao wote walikuwa Chadema kwani kuondoka na kisha kurudi tena kuna shida gani pengine walikimbia uongozi uliopita au mazingira ya kisiasa yalikuwa mabaya, wachunguze case by case. chama ni watu. Tusidanganyane. Kwenye club za mipira watu huhama na kurudi vivyo hivyo siasa. politics is complex and dynamic game.
 
Kutokana na hali na mazingira mapya ya kisiasa ninashauri wale wabunge 19 warudishwe kujenga chama na kuongeza ushawishi kuelekea uchaguzi Mkuu kwa misngi ifuatavyo

1. Wabunge hawa pamoja na makosa waliyoyafanya lakini hawakuibagaza chadema wao waliendelea kujitetea uwemo wao bungeni na kutimiza majukumu ya kibunge.

2.kwenye siasa ni namna ya kucheza draft hakuna adui wa kudumu na rafiki wa kudumu.

3. waliondoka katika mazingira ya uongozi wa zamani uongozi wa chadema umebadilika na maono mapya. ni kipindi cha kujenga upya chama kwa kuwarejesha pia walikengeuka

4. Mara kadhaa wamekitetea chama bungeni rejeeni kauli za Bulaya na Mdee

5. So far hata wakirudi watabaki kuwa wanachama wa kawaida uchaguzi umekwisha kwenye maeneo yote. Hawana maamuzi ya kiuongozi hivyo watapimwa upya wakiwa wanachama wa kawaida

6. Naamini bado wana damu ya ki-chadema na wamekitumikia muda mrefu. Wapewe nafasi ya kuomba radhi kwa yaliyotokea na kisha washiriki kwenye ujenzi wa chama. Mabadiliko ya uongozi ndani ya Chadema kwa sasa yatumike kurejesha wote waliokikimbia chama kwa sababu mbalimbali. Hii ni siasa na siasa ni sayansi.
Once a snitch always a snitch, sikubaliani na nyie COVID-19 kurudi bungeni na sababu ulizozitumia zote ni rubbish. Walikuwa bungeni kuendelea kusaliti msimamo wa chama chao kwa sababu tofauti kabisa na ulizoziorodhesha.
-Walikuwepo bungeni si kwa kuiwakilisha CHADEMA bali kwa maslahi yao binafsi(mishahara + marupurupu) kwani walikwenda kinyume na matakwa na msimamo wa chama chao.
-Walibaki bungeni kwa maelekezo ya Ndugai na hayo maelekezo ilikuwa ni kutii na kutekeleza amri ya Mwendakuzimu so literally walikuwa wakimuwakilisha huyo Mwendakuzimu kwa faida za kisiasa ili internationally iaminike kuwa bunge lina wabunge wa opposition.
NB: Sababu pekee ambayo ningeweza kukubalia kuwa wapokewe tena ndani ya CHADEMA ni kuwa kama msaliti mkuu Slaa amepokewa kundini licha ya kuwa alisaliti chama katika kipindi kilichokuwa very critical na akawa akikipiga vita 'live' kipindi alipoonyesha rangi zake halisi na kuwa chawa wa Mwendakuzimu basi hata wao wafikiriwe au jambo lao lijadiliwe ikibidi katika mkutano mkuu wapewe nafasi ya kuhojiwa(kuulizwa maswali) ila hata Slaa apitie process hiyo kwa faida ya afya ya CHADEMA. Kuwa na mamluki ni jambo hatari sana kwa hauwezi kujua exactly plans zake ni zipi. Wahenga 'weupe' walinena "once bitten twice shy", CHADEMA wataonekana hawana akili kabisa kama Slaa(with his unstable mental balance) atawageuka tena muda wowote atakapotengeneza sababu za kugeuka harakati japo kuwa na msaliti mmoja ndani ya chama ni tofauti na kuwa na kundi kubwa la wasaliti.

Kilichomrahisia Slaa licha ya kuwa ni snitch na hapaswi kupewa nafasi ni urafiki wake na Maria Sarungi ukizingatia kwa sasa Maria is very influential ndani ya CHADEMA.
Kwa maoni yangu binafsi COVID-19 pamoja na Slaa ni time bomb linaloweza kuwalipukia CHADEMA wakati wowote kama watapokelewa tena.

--The funny fact ni kwamba CCM ndiyo wanaolialia kuwa COVID-19 warudishiwe CHADEMA hapo kila mwenye akili timamu atajiuliza kulikoni?
 
warejeshwe on merits mmoja mmoja.
At least point yako inajadilika, yaani wapitie chujio kali la CHADEMA mmoja mmoja(this should include the most notorious snitch of them all mzee Slaa) watakao faulu wawekwe mbele ya mkutano mkuu wahojiwe publicly ikibidi iwe live on TV then ikibidi public opinion iwe ndiyo hakimu wao.
It's so painful when you think that those snitches were cooperating with Magu kipindi ambacho Lissu alishambuliwa na Saanane aliuawa and here I insist aliuawa na si kwamba alipotezwa as if there chances kwamba anaweza akapatikana.
 
Hao wote walikuwa Chadema kwani kuondoka na kisha kurudi tena kuna shida gani pengine walikimbia uongozi uliopita au mazingira ya kisiasa yalikuwa mabaya, wachunguze case by case. chama ni watu. Tusidanganyane. Kwenye club za mipira watu huhama na kurudi vivyo hivyo siasa. politics is complex and dynamic game.
Kufananisha chama cha siasa na vilabu vya mpira ni upopoma!! Kuwarudisha covid 19 jinsi walivyo Tumika kukisaliti chama kwa vipande vya silver ni kuua Chadema mpya!! Adui wa Chadema aliewashawishi Bado yupo na hata hivyo Chadema ina wanawake wengi wenye nguvu kuweza kukiwakilisha!
 
Back
Top Bottom