Chadema wapanga kutarisha mandanono ya nchi nzima Dar.

abdulahsaf

JF-Expert Member
Aug 31, 2010
858
130



Chadema wagoma kuzungumza
Na Richard Makore
30th January 2011
Kamati Kuu ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), jana ilikutana Jijini Dar es Salaam kujadili masuala mbalimbali yanayohusu chama hicho ingawa hadi jioni viongozi wake waligoma kusema kilichojadiliwa.Habari za ndani zinasema Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimepanga kutarisha Mandamano ya Nchi mzima kuiondosha ccm ikiwa demand za Wtanzania walio wengi hazito sikilizwa.
Akizungumza na NIPASHE jana, Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa chama hicho, Erasto Tumbo alikiri kamati hiyo kujadili mambo mazito lakini alikataa kuyataja japo kwa kifupi.
Tumbo alisema moja ya agenda zilizowasilishwa jana na kujadiliwa ni pamoja na hali ya kisiasa hapa nchini na mikakati ya kazi ndani ya chama kwa mwaka huu.
Kamati hiyo jana ilijifungia ndani siku nzima ambapo baadhi ya wajumbe wake walipoulizwa na NIPASHE kuhusu kilichozungumzwa walikwepa kusema na kumuomba mwandishi avute subira hadi leo itakapotolewa taarifa rasmi ya chama.
Mkutano huo ulifunguliwa na mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe ambapo wajumbe mbalimbali wakiwemo baadhi ya wabunge walishiriki.
Awali taarifa zilisema moja ya agenda ya kikao hicho ilikuwa ni kupokea taarifa ya wazee wa chama hicho iliyochunguza mwenendo wa Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, Zitto Kabwe na baadhi ya wabunge wa chama hicho ambao hawakuhudhuria kikao cha kwanza cha Bunge la 10 mjini Dodoma mwaka jana ambapo Rais Kikwete alihutubia.
Zitto alionekana mwenye furaha na amani wakati akitoka ndani ya kikao hicho kwa ajili ya kupumzika nje huku wajumbe wengine wakiwa wanaendelea na kikao chao na muda mfupi alirejea tena kuungana na wenzake.
Itakumbukwa Zitto alinusurika kufukuzwa katika nafasi ya Unaibu Katibu Mku wa chama hicho kufuatia wabunge wenzake wa chama hicho kupiga kura ya kutokuwa na imani naye.
Habari zingine za awali zilibashiri kuwa huenda kikao hicho kitajadili pia tukio la wafuasi wa chama hicho kupambana na polisi mkoani Arusha Januari 5, mwaka huu ambapo watu watatu walipigwa risasi na kufariki dunia.
Chama cha democrasia na maendeleo (Chadema)

[caption id="attachment_27753" align="aligncenter" width="300" caption="Ccm enough kutawala nusu karne tunataka kuona mwanga mpya na matumaini mapya."]
 
chadema kutarisha maandamano nchi nzima Dar

aliyeelewa hichi kichwa cha habari na habari yake anieleweshe...maandamano ya nchi nzima yatafanyika dar au....?

habari ya uzushi hii....
 
chadema kutarisha maandamano nchi nzima Dar

aliyeelewa hichi kichwa cha habari na habari yake anieleweshe...maandamano ya nchi nzima yatafanyika dar au....?

habari ya uzushi hii....
Re: Chadema wapanga kutarisha mandanono ya nchi nzima Dar.
Huyu jamaa hana lolote anatubandikia picha zisizo na uhusiano ndio walewale wa siku zote wakurupukaji.
 
Hii sehemu waliyofanyia mkutano, ni statement pia.

Kama ni ofisini kwenu mchango wa kununua niru na rangi unahitajika kurekebisha huo ukuta.
 
Habari siielewi ndivyo kikao kilivyokuwa kwa maana kuandaa maandamano ilikuwa Agenda au hilo ni wazo la mwaandishi??
Mbona kama ni uzushi huo??
 
Nadhani Zitto amaeamua kujirudi, maana ameona alikokuwa anataka kwenda ni kubaya zaidi, sure Iam telling you CCM haina miaka mitanao ijayao, sasa Zitto kaona akiharibu huku kwetu ataenda wapi maana vinginevyo itabidi ajiunge na hivi vyama vya ovyo ovyo tu ambavyo Dr slaa aliviita
 



Chadema wagoma kuzungumza
Na Richard Makore
30th January 2011
Kamati Kuu ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), jana ilikutana Jijini Dar es Salaam kujadili masuala mbalimbali yanayohusu chama hicho ingawa hadi jioni viongozi wake waligoma kusema kilichojadiliwa.Habari za ndani zinasema Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimepanga kutarisha Mandamano ya Nchi mzima kuiondosha ccm ikiwa demand za Wtanzania walio wengi hazito sikilizwa.
Wakuu tusimpinge mleta mada,wakati yeye kwa nia nzuri amekuja kutujuza..., nadhani kuhusu hiyo habari ya maandamano nchi nzima ametoa hapo kwenye Bold... yeye alichofanya ni kunukuu NIPASHE
 
Chadema na viongozi wake waliokuwa kwenye mkutano waligoma kuongea na mwandishi wa habari. Sasa hizo habari za maandamano nchi nzima amezitoa wapi? Uzushi wa Mengi na waandishi wake uchwara wa Nipashe utamtokea puani siku moja!!! Mengi amezoea kufanya ufisadi na kukimbilia huruma za watanzania.... sasa kwa haya anayoyafanya ya uzushi wa wazi asitegemee tena huruma hizo!!!!
 
Hayo maandamano ya nchi nzima watayaratibu vipi? Radio is the most reliable medium, hawana. SMS is the second, wananchi wa kawaida hawana simu, umeme hakuna. Ngoja tusikie mikakati yao
 
Dah hizi habari zinanichanganya mara walikataa kuzungumza tena habari za ndani hii tukiita ni uzushi nadhani tutakuwa sahihi
 
Huyu jamaa hana lolote anatubandikia picha zisizo na uhusiano ndio walewale wa siku zote wakurupukaji.

Mtu akianza na title yenye errors za ajabu kama " Kutarisha mandanono" what else should you espect from the post? Its a sign kwamba kakurupuka au ni kilaza wa kutupwa.
 
Nivizuri kuandika habari uliyokuwa na uhakika naya sio unakuwa kama magazeti ya udaku angle na ulichokiandika ndani tofauti,
 
Back
Top Bottom