CHADEMA wanuna Zitto kwenda CUF

CHADEMA wanuna Zitto kwenda CUF

TataMadiba

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2014
Posts
9,868
Reaction score
5,753
Mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Zuber KABWE (CHADEMA) ameitia msukosuko na kuelekea kupasuka Kambi ya Umoja wa Katiba ya Wanachi(UKAWA) baada ya kupanda katika jukwaa la Mkutano wa hadhara ulioandaliwa na Chama cha Wananchi (CUF) mkoani Mtwara , chini ya Mwenyekiti wa CHAMA hicho, Prof. Ibrahim Harouna LIPUMBA. LIPUMBA anashutumiwa na CHADEMA kukiuka makubaliano ya UKAWA na kutaka kukigombanisha CHADEMA na wanachama wake kwani Kamati kuu ya CHDEMA ilishatoa maazimio yake kuwa ZITTO asipewe ushirikiano wowote ndani ya CHADEMA na mshirika yeyote wa CHADEMA vikiwemo vyama vya upinzani vinavyounda UKAWA. CHADEMA wanahoji kama itawapendeza CUF kuona FREEMAN MBOWE akizunguka na HAMAD RASHID kwenye majukwaa ya kisiasa.

Katika mkutano huo wa hadhara, ZITTO alimwamgia sifa Prof.Lipumba na kuonesha kuwa ni kiongozi anayefaa kuwatumikia Watanzania ikiwa watampa ridhaa.

Mytake: CHADEMA na CUF wanawatambua ZITTO KABWE na HAMAD RASHID kuwa ni wabunge wa MAHAKAMA kwa maana nyingine vyama hivyo haviwatabui kama wanachama wao na kwa maana hiyo wako huru kufanya siasa popote ilimradi tu hawafanyi hivyo kwa tiketi ya vyama vyao. Nini sasa sababu ya kauli hizi kutoka kwa CHADEMA? Ni uoga , ni wivu au ni nini?
attachment.php

Attachments

  • chadema20.jpg
    chadema20.jpg
    41.7 KB · Views: 4,308
kwani hapo tatizo ni liko wapi zito ni MP opposition hata kama wana kesi mahakamani. lipumba hakufanya kosa kumwalika na aliamini kumsaidia to clarify some issues ili watu waelewe. mimi nawashauri CDM musihesabu makosa mnayo ona zitto kafanya. kumbukeni wakati wa buzwagi scandal jinsi zitto alivyo fanya kazi ya kujenga chama na marq ngapi zitto aloweka rehani uhai wake kwa maslahi ya chama. Namwamini sana mbowe kuwa ni mtu mwenye hekima sana na ndo maana CDM mmefika hapo mlipo namshauri mbowe atafute namna yq kimaliza mgogoro huu kumfukuza zitto siyo solution hata kidogo
 
habari ilioyofichwa source inatosha kuitwa ni umbea, umbea mtupu, kwa maneno mengine mleta uzi ni mbea
 
Habari haina hata nukuu ya mtu ambaye ametoa hizo claims,,mwandishi kajitungia! Hawamtendei haki msomaji hasa yule asiye na media literacy,anapokea kama ilivyo
 
chadema wakue sasa hata na cuf vile vile wote washike silaha moja wapambane na ADUI yao mmoja tu CCM// hao akina zitto au hamad rashid warudishwe vyamani na kupewa majukumu kwa mipaka maalumu!
 
Last edited by a moderator:
Mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Zuber KABWE (CHADEMA) ameitia msukosuko na kuelekea kupasuka Kambi ya Umoja wa Katiba ya Wanachi(UKAWA) baada ya kupanda katika jukwaa la Mkutano wa hadhara ulioandaliwa na Chama cha Wananchi (CUF) mkoani Mtwara , chini ya Mwenyekiti wa CHAMA hicho, Prof. Ibrahim Harouna LIPUMBA. LIPUMBA anashutumiwa na CHADEMA kukiuka makubaliano ya UKAWA na kutaka kukigombanisha CHADEMA na wanachama wake kwani Kamati kuu ya CHDEMA ilishatoa maazimio yake kuwa ZITTO asipewe ushirikiano wowote ndani ya CHADEMA na mshirika yeyote wa CHADEMA vikiwemo vyama vya upinzani vinavyounda UKAWA. CHADEMA wanahoji kama itawapendeza CUF kuona FREEMAN MBOWE akizunguka na HAMAD RASHID kwenye majukwaa ya kisiasa.
Katika mkutano huo wa hadhara, ZITTO alimwamgia sifa Prof.Lipumba na kuonesha kuwa ni kiongozi anayefaa kuwatumikia Watanzania ikiwa watampa ridhaa.
Mytake: CHADEMA na CUF wanawatambua ZITTO KABWE na HAMAD RASHID kuwa ni wabunge wa MAHAKAMA kwa maana nyingine vyama hivyo haviwatabui kama wanachama wao na kwa maana hiyo wako huru kufanya siasa popote ilimradi tu hawafanyi hivyo kwa tiketi ya vyama vyao. Nini sasa sababu ya kauli hizi kutoka kwa CHADEMA? Ni uoga , ni wivu au ni nini?

View attachment 216631

Acha fitina
 
Wanachokifanya chadema ni kama mwanaume aliyemwacha mkewe then anaanza kumuonea wivu baada ya kuolewa na mume mwingine. Pia inaweza kuwa kinyume chake
 
Back
Top Bottom