Chadema wananchi wanawaandalia hukumu nzito | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Chadema wananchi wanawaandalia hukumu nzito

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Sangarara, Mar 24, 2012.

 1. Sangarara

  Sangarara JF-Expert Member

  #1
  Mar 24, 2012
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 13,048
  Likes Received: 554
  Trophy Points: 280
  Naomba kuweka mambo sawa kidogo.
  Kuna watu ambao wanaonyesha kila dalili za kuweweseka, ama kuchanganyikiwa au kupumbaa au kuwehuka au kufamiwa na mapepo na kuwa kama mapunguhani fulani hizi wameibuka siku za hivi karibuni na kukisakama CHAMA CHA DEMOCRASIA NA MAENDELEO katika mpangilio mzuri sana wa mbinu za kiushindani za kihayawani.

  Nimeonelea kuweka mambo sawa ili isijie ikaonekana watu wote ni wapungufu wa uelewa wa mambo ya ulimwengu huu hasa hapa nchini.

  Kwanza, na ieleweke wazi kwa viongozi wa CHADEMA kwamba, kuna viashiria vya kutosha kuthibitisha kwamba UMA wa watanzania umekwisha amua kukifanya kuwa chama tawala nchini. Maamuzi haya yamefanyika baada ya kupata uelewa kwamba matitizo yooote yanayotukabili watanzania yanachangiwa kwa kiwango kikubwa na uongozi mbovu wa kisiasa uliopo nchini na hivyo wamejawa na imani kubwa sana kwamba CHADEMA ndio mkombozi wao.

  Pili, wananchi wanatambua kwamba, serikali na chama kinachoiongoza kinafahamu maamuzi haya ya UMA wa watanzania na hivyo kiko tayari kufanya kitu chochote kile katika kuhakikisha kwamba mapenzi haya ya UMA hayatimiliki kwa namna yoyote ile, wananchi wanatambua kwamba ufanyaji kampeni wa kinyama unaofanywa na chama hiki kuanzia uchaguzi mkuu wa 2010 na chaguzi ndogo za igunga na sasa Arumeru Mashariki unalengo la kuwazuia wananchi wasitimize kwa matendo matakwa yao, wanatambua kwamba uharamia unaofanywa na tume ya uchaguzi kwa kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama nchini wa kubaridisha matokeo ya maamuzi ya wananchi juu ya viongozi waliowachagua ni muendelezo ya kuweweseka kwao na ishara za maamuzi ya wananchi dhidi yao, watanzania tunajua kwamba, mbinu zote chafu za kuwadhihaki, kuwapakazia na kuwapiga, kuwanyanyasa, kuwakamata na kuwafungulia mashtaka yasikuwa kuwa na maana yoyote ile katika mahakama zilizo chini yao ni muendelezo wa hujuma za serikali iliyo chini ya ccm dhidi ya matakwa ya wananchi.

  Tatu, kutokukata tamaa kwa wananchi na ongezeko kubwa la muamko wa kutaka mabadiriko linalothibitishwa na viashiria kadha wa kadha ni ushahidi kwamba, pamoja na hayo yote yaliyotajwa hapo juu, Imani ya wanchi kwa CHAMA CHA DEMOCRASIA NA MAENDELEO imekuwa ikiongezeka na kupanuka zaidi na zaidi katika jamii yote ya Jamhuri ya Muungano wa watanzania. Na hivyo basi, Hii inawapa viongozi wote wa CHADEMA jukumu la kutokukata tamaa kwa namna yoyote ile katika mapambano haya ambayo hakika wamekuwa vinara wa kuyasambaza kama moto nchini mwetu.

  Nne, Ukianzia na maamuzi waliyoyachukua watanzania kwenye uchaguzi wa Rais Mwaka 2010 hata baada ya kampeni chafu katika historia ya nchi yetu dhidi ya Mgombea Urais wa CHADEMA, DR SLAA NI ushahidi wa kutosha kwamba hakuna propaganda, ushawishi, uchafu, shirki na ghirza za namna yoyote zinaweza kubadirisha kiu ya mabariko iliyotanda nchini kwa mategemeo makubwa sana ya wanchi kwa viongozi na CHAMA CHA DEMOCRASIA NA MAENDELEO.

  Tano, Hivyo basi, wale wote ambao ama wamejitoa akili au wametumwa kufanya uchafuzi wa hali ya hewa kwa CHADEMA na viongizi wake wanapaswa kujua kwamba, wanachokifanya ni sawa sawa kabisa ni kujaribu kufungua kufuri bila funguo, hakuna Mwananchi hata mmoja anayeweza kudanganyika kwa kampeni za kishenzi na hoja zisizokuwa na mashiko,

  Hivi sasa watanzania mashtaka yetu yote ni dhidi ya serikali ya chama cha mapinduzi sababu ndicho chenye dhamana ya uongozi wa serikali yetu ambayo imeshindwa kabisa kabisa kufikia hata malengo ya Taifa letu kudai uhuru kutoka kwa mkoroni takrani miaka 50 iliyopita.Na kwamba tunawachukulia nyie viongozi wa CHADEMA kama malaika katika swala zima la uongozi mbovu wa nchi yetu.

  LAKINI MTAMBUE KITU KIMOJA, KWAMBA WAKATI TUTAWAONDOA CCM MADARAKANI HUKU TUKISHANGIRIA NA KURUKARUKA KWA FURAHA, ENDAPO MTAFANYA USALITI WA NAMNA YOYOTE ILE BAADA YA KUINGIA MADARAKANI MKAANZA KUENDESHA SERIKALI KATIKA NAMNA INAYOPINGANA NA MATARAJIO YETU WANANCHI ADHABU TUTAKATOWAPA ITASIKIKA MPAKA MASHARIKI ZA MBALI SABABU TUTAWAADHIBU HUKU TUKILIA NA KUTOA MACHOZI YA DAMU.
   
 2. JOB SEEKER

  JOB SEEKER Senior Member

  #2
  Mar 24, 2012
  Joined: Aug 1, 2011
  Messages: 145
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Masaburiiiiiiiiiiiiiii,umepotea zizi mkuuuuuuuuuuu
   
 3. P

  Pelege Senior Member

  #3
  Mar 24, 2012
  Joined: Mar 1, 2012
  Messages: 137
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hii vita ni ya kila mtanzania mwenye uchungu na nchi yake,ni heri ya vita inayotafuta haki na utu wa mwanadamu kuliko unyanyasaji wa Chama legelege cha CCM wanavyofanya kwa wananchi walio katika ardhi yao,Mungu mkubwa sisi tunaodai haki ya kweli tuna Mungu anayetupigania wao CCM wanapesa,askali,usalama wa Taifa unaowalinda!
   
 4. Fredrick Sanga

  Fredrick Sanga JF-Expert Member

  #4
  Mar 24, 2012
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 3,148
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Hii imekaa vizuri, kama ile ya Michael Sata.
   
 5. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #5
  Mar 24, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 445
  Trophy Points: 180
  CHADEMA inatawala kutoka kwenye mioyo ya watanzania wazalendo. kilichobaki ni kutawala nchi tu
   
 6. Losambo

  Losambo JF-Expert Member

  #6
  Mar 24, 2012
  Joined: Nov 8, 2011
  Messages: 2,623
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Seeker sijui unasiki for what? Naamini umeishia njiani baada ya utangulizi usioleweka wa mtoa mada.

  Lakini jamaa amezungumza ukweli sana. Siku CDM ikiingia madarakani najua haiwezi kuigeuza Tz kuwa nchi ya asali lakini ionyeshe uongozi wa haki na usawa ili tunaotawaliwa tulidhirike hata kama hali si shwari sana.
   
 7. odinyo

  odinyo JF-Expert Member

  #7
  Mar 24, 2012
  Joined: Feb 6, 2012
  Messages: 428
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 45
  Mkuu,

  massenge yako ni nzuri ila ni Riwayaaaaaaa.
   
 8. g

  greenstar JF-Expert Member

  #8
  Mar 24, 2012
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 390
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  hata SATA na OBAMA walitumia mbinu hizo hizo,lakini ukiingia madarakani ndipo utagundua mambo magumu kweli kweli.Kuwa RAIS au kuunda serikali si ishu ya kitoto au mambo ya mzaha,kuna masuala nyeti ambayo yanachangamoto kila siku.Mbwembe za nguvu ya UMMA imewagarimu LIBYA na MISRI hali imekuwa mbaya zaidi.Je na sisi tuige upuuzi huo? tutumie Demokrasia VIZURI bila JAZBA au kudharau manikio yaliyopatikana hata kama ni 1%.Leo hii CHADEMA ina wabunge 48 lakini majimbo ya mfano ni 3 tu toka waanze mbwembwe zao.Tunataka wajikiite kuyaboresha majimbo 45 ili tuwape dhamana na MAJIMBO mengine badala ya kuandamana na kuleta uchochezi kwa SERIKALI ishindwe kutimiza wajibu wao.IPO siku watanzania wataamua kuwapa kura za RAIS lakini si 2015....yaani baadaye sana.CCM bado ina hazina ya VIONGOZI ambao wana PROFILE za kiuongozi unaoheshimu utawala wa sheria.
   
 9. democratic

  democratic JF-Expert Member

  #9
  Mar 24, 2012
  Joined: Nov 21, 2011
  Messages: 1,644
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  msg sent and delivered
   
 10. L

  Lamusumo JF-Expert Member

  #10
  Mar 24, 2012
  Joined: Mar 23, 2012
  Messages: 275
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hakika ujumbe uliotolewa mwanzisha mada ni mzito sana na haupaswi kupuuzwa na kila mtanzania anayeguswi ugumu wa maisha ambao chanzo chake kiko wazi kabsa.ukombozi upo karibu watz jukumu letu kuiunga mkono cdm
   
 11. WAHEED SUDAY

  WAHEED SUDAY JF-Expert Member

  #11
  Mar 24, 2012
  Joined: Jun 24, 2011
  Messages: 7,161
  Likes Received: 1,250
  Trophy Points: 280
  Asante mkuu kwa huu uzi
   
 12. Jumakidogo

  Jumakidogo R I P

  #12
  Mar 24, 2012
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 1,859
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Mkuu massenge ndiyo nini?
   
 13. Gwankaja Gwakilingo

  Gwankaja Gwakilingo JF-Expert Member

  #13
  Mar 24, 2012
  Joined: Jan 26, 2012
  Messages: 1,963
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  We mkali wakati wengi wanatazama leo wewe umetazama leo kesho kisha ukatazama na keshokutwa nimeikubali sana hii
   
 14. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #14
  Mar 24, 2012
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  MSIWE NA MASHAKA MIOYONI KWENU, chadema ni chama cha wananchi si chama cha mafisadi
   
 15. chitalula

  chitalula JF-Expert Member

  #15
  Mar 24, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 1,307
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  chadema tunawaamini sana, wasituangushe tafadhali
   
 16. TOWNSEND

  TOWNSEND JF-Expert Member

  #16
  Mar 24, 2012
  Joined: May 8, 2011
  Messages: 2,597
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  mimi liwalo na liwe hata aje kichaa nitampigia kura yangu kuliko hapa tulipo huu uongozi wa ccm hauna mpango wenyewe tu hawajui wanafanya nini kila mtu na lake kila kukicha huyu anasema hivi yule hivi hawawezi hata kubuni kiwanda cha bicycle au jembe la mkono
   
 17. B

  Bobuk JF-Expert Member

  #17
  Mar 24, 2012
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 5,876
  Likes Received: 481
  Trophy Points: 180
  Unaweza ukatutajia japo 5 tu ambayo ni HAZINA ya VIONGOZI wa CCM? Na wamefanya mambo gani ya kupigiwa mfano tangu wawe viongozi wa nchi hii? The ball is in your court.
   
 18. bepari1

  bepari1 Member

  #18
  Mar 24, 2012
  Joined: Sep 10, 2011
  Messages: 74
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 15
  You are real great thinker! Harakati hizi ziwe za kudumu na elimu izidi kutolewa kwa raia ili kufikia mageuzi ya kweli.bravo cdm.
   
 19. Sangarara

  Sangarara JF-Expert Member

  #19
  Mar 24, 2012
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 13,048
  Likes Received: 554
  Trophy Points: 280
  Ujumbe wangu ni mahususi kwa watu kama nyie
  Chadema hawezi kufanya mabadiriko katika jimbo hata moja sababu sio inayosimamia mgawanyo wa kodi katika nchi hii, Katika hayo majimbo chadema ni wawakilishi wa wananchi bungeni tu ambako kila kukicha tunashudia wanavyozomewa na kunyanyaswa pale wanaposimamia hoja zenye manufaa kwa wananchi.

  Hoja yangu inapinga kwa nguvu zote dhana ambayo watu kama nyie ambao Mwenyezi Mungu amewapatia akili za kufikiria na fursa ya kwenda shule lakini kwa makusudi mnazitumia katika kuwapotosha watanzania ambao wamekosa fursa ya kuzipanua bongo zao na kuwa na uwezo wa kupambanua mambo kutokana na uongozi legelege wa chama cha mapinduzi.

  Time to Judge CHADEMA has not yet come.
   
 20. M

  Mpanzi JF-Expert Member

  #20
  Mar 24, 2012
  Joined: Jan 11, 2011
  Messages: 767
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45
  1.Wassira
  2.Sofia Simba
  3.Komba
   
Loading...